secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,984
- 51,055
Umesema anayepigiwa (mchakato). Tayari Nchimbi ameshapigiwa.Hapana sio lazima
Lakini mfumo unamtaka anae pigiwa awe ndani ya chama Cha siasa,
Yani mwanachama anae wakilisha chama chake.
Sahihisho dogo. HATUKUWA HAGUA. 29 October watu walijifungia ndani wasijefia barabarani. Hakuna aleyeenda kupiga kura.Hiki kilichofanyika kwa Nchimbi ni ushahidi tosha tuna katiba mbovu na iliyopitwa na wakati. Haiwezekani mtu aliyechaguliwa na wapiga kura milioni 31+ ashinikizwe kujiuzulu na watu wachache tu ndani ya chama cha siasa.
Kwa hiyo kumbe hata kama angejiuzuru kwa hiyari yake mwenyewe lakini lazima Chama chake kipeleke suala hilo Bungeni ili Bunge lipige kura ya kukubaliana au kutokubaliana nae,yaani kwa maana hiyo Raisi si yeye tu mwenye mamlaka ya kujiamulia kumtoa Makamu wake kwa utashi wake tu bila idhini ya Bunge?Famahamuni haya fika.
Mfumo wetu wa Uraisi ulioanza mwaka 1995 wa mgombea mwenza tumeuiga kutokea nchi ya Marekani, ambapo Raisi na Makamu wake wanateuliwa kwa pamoja, na wanaanza kazi siku moja. Hivyo kinga ambayo anaipata Raisi ndiyo hiyo-hiyo anaipata Makamu wake. Kitaalamu hii tunaiita Functional Immunity (From Civil & Criminal Proceedings).
Emmanuel Nchimbi, unaweza usimpende lakini analindwa na katiba kama ambavyo Raisi Samia alilindwa na Katiba mwaka 2021 wakati akiwa Makamu wa Raisi asiyekuwa anaifahamu hatma yake. Wengi hatukutaka Raisi Samia awe Raisi, lakini Kikwete na Mabeyo ndiyo walimfanya Samia akawa Raisi. Wengi hatukupinga wala kulalamika kwasababu lilifanyika kikatiba.
SASA BASI, nchini Tanzania kuna haya yafuatayo ambayo yako bayana kabisa:
MOSI, Mamlaka ya nidhani (Disciplinary Authority) ya Raisi na Makamu wake ni Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siyo Msajili wa vyama, siyo Jaji Mkuu, siyo Jeshi na wala siyo NEC ya CCM. Makamu wa Raisi hata kama Raisi hampendi anatakiwa apeleke mashitaka kwenye chama, halafu chama wapeleke mashitaka hayo bungeni ambako wataanzisha mchakato wa kumvua nafasi makamu wa Raisi (A motion of Impeachment), ambao utaishia na azimio maalumu ya kuthibitisha kwamba makamu atolewe au asitolewe (A Resolution Confirming Impeachment).
NEC ya CCM kumvua uanachama Makamu wa Raisi Emmanuel Nchimbi, ambaye kwa barua yake amesema ataondoka kwenye nafasi yake ifikapo tarehe 4 Septemba 2026 ni UHAINI. CCM imepoka madaraka ya Bunge na kutikisa taasisi ya Uraisi.
Fahamuni fika, kwamba leo hii akifariki Raisi Samia kabla ya tarehe 4 Septemba 2026, Raisi wetu atakuwa ni Dr. Emmanuel Nchimbi na siyo mtu mwingine. Hivyo ambacho mnakifanya sasa ni uhuni utakaokuja kuwatokea puani siku siyo nyingi, maana mshajenga mfano mbaya (A Bad Precedent)
PILI, Kinga ya Raisi ndiyo kinga ya Makamu Wake. Raisi na Makamu hawawezi kushitakiwa popote pale. Lengo la kumpa Raisi na Makamu wake kinga ni kuhakikisha ofisi ya Raisi inathibitika ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu makubwa ya kitaifa. Hivyo madai yote dhidi ya Raisi na Makamu ni lazima yapitie bungeni kwanza. Mtu hawezi kuamka tu akasema leo hii hatumpendi fulani basi tumvue uanachama ili apoteze nafasi yake ya Uraisi au Umakamu. Kama hili litakuwa linafanyika, hatutakuwa na nchi bali gulio ya washenzi, ambapo kila muhuni anaamka tu na anamuondoa Raisi akijisikia.
========================================================================
JAMBO LOLOTE BAYA, likimtokea Makamu Wa Raisi, Dr.Emmanuel Nchimbi kipindi hiki hata baada ya kuachia nafasi, sisi tutalichukulia hili kama UHAINI. Kinara wa huo uhaini ni Dr. Asha Rose Migiro na wengine. Mlipoka madaraka ya bunge kwa kuifanya CCM ivumbe Ibara ya 50 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na kwasababu mshaonesha nia ovu, hata baada ya 4 Septemba 2026, tutaangalia kwamba lolote litakalotokea kwa Dr.Emmanuel Nchimbi halikuanzia bungeni, hivyo ulikuwa ni UHAINI usio na uhalali.
JINAI haiozi, wote mliohusika na hili sakata, ombeni sana MUNGU hata siku moja asiingie mtu mwendawazimu kwasababu mtanyongwa na kupigwa risasi barabarani kama wanyama. Hili wala haliitaji ushahidi, tumeona mkivunja katiba waziwazi na kufanya mambo ambayo yanatishia usalama wa Makamu wa Raisi.
========================================================================
Wajinga wengi watatoa mfano wa kuondolewa kwa Aboud Jumbe Mwinyi, lakini ukweli ni kwambwa mwaka 1984, Mwinyi alikuwa Makamu wa Pili wa Raisi, ambaye aliongoza Zanzibar iliyokuwa haina hata KATIBA yake. Tena kubwa zaidi ni kwamba alikuwa anateuliwa na Wazanzibari tu, siyo watanzia wote.
Hili la sasa litasababisha matatizo makubwa mnoooo siku za karibuni.
=========================================================================
Wiki chache zilizopita wanasheria wa Tanzania wameenda ICC wakiongozwa na mwanasheria mkubwa ambaye jina lake hatutalitaja hapa. Kinachoendelea huko duniani ni kibaya na hata hii tume ya pili haitaweza kukizuia.
Binafsi huwa nasema hivi: NI SUALA LA MUDA TU..........
Anapoteza sifa ya kuwa kwenye nafasi husika au ya kugombea nafasi? Maana kugombea nafasi vs umeipata nafasi ni vitu viwili tofauti.
Katiba inasemaje? Kama hujui Sema sijui mkuu usifanye spinning. It's ok kutokujua, hata mimi sijui ndo maana nauliza.
Mfano: Ili kupata kazi lazima uwe na wadhamini, ila ukishapata hiyo kazi nafasi ya mdhamini kwenye kukuondoa kazini ni finyu. Huu mfano nimekupa ili unielewe ninachouliza kuhusu kugombea nafasi na kuwepo kwenye nafasi.
Iko siku...They just don't care❗
Kwa hiyo kumbe hata kama angejiuzuru kwa hiyari yake mwenyewe lakini lazima Chama chake kipeleke suala hilo Bungeni ili Bunge lipige kura ya kukubaliana au kutokubaliana nae,yaani kwa maana hiyo Raisi si yeye tu mwenye mamlaka ya kujiamulia kumtoa Makamu wake kwa utashi wake tu bila idhini ya Bunge?
Duh. Okey.Katiba ya Kiingereza na Katiba ya Kiswahili zimekinzana!
Hazijakinzana tu kitafasiri ndogo (Clerical Difference) ambapo tungesema Katiba ya Kiswahili itashinda, bali zimekinzana kimaudhui (Thematic Differences).
Katiba ya Kiswahili inasema kugombea na kushika kiti, huku katiba ya Kiingereza ikisema kugombea peke yake ikizungumzia sifa za kugombea.
Hivi kwa nini waislamu wa JF ni wadini na wapumbavu sana? Nauliza hivi kwa sababu kuna waislamu wengi tu wako very smart ila miislamu ya humu JF ni mipumbavu sana na imejaa udini vibaya mno, why? Nina marafiki wengi tu waislamu lakini wako njema kichwani na hawana ujinga kama haya majamaa ya humu JF. Naomba jibu wewe mpumbavu KERATO MOMBAAUmeandika takataka... Tena uvundo uliooza
1. Rais Samia hajamuondoa nchimbi uVP, Bali nchimbi ndiye alibandika huko instagram na akampa mh rais taarifa.
-hivyo mh. rais alithibitisha maamzi ya nchimbi (soma katiba kinukamto wewe)
2. sifa mojawapo ya kuwa makamu wa rais ni lazima uwe mwanachama wa chama cha kisiasa, alipofukuzwa uachama tayari muda huo huo alikoma kuwa VP, na hatua hyo ilifuta notis yake ya hadi tarehe 4 sept.
-hapa hakuna mutual agreement (ni tofauti kabisa na alivyoondoka mh mpango)
3. mlitaka kumtumia VP kama mashine ya kuendeleza uanaharakati ikulu, hyo imekula kwenu.
4. ikulu ina utaratibu wake, si ombi ni lazima VP awe mtii kwa bosi wake na chama chake kilichompa ridhaa.
-ikulu si makao makuu ya tecdema kwamba kila ndezi anaweza fanya harakati.
5. Hata asingejiuzulu, kwa mwenendo wake lazima angevuliwa uanachama, na hapo lazima angeachia uVP.
Kwa hiyo sababu zilizowafanya wamuondoe sio za kinidhamu ndio maana hawakumpeleka Bungeni wakaamua wamuadhibu kichamaa,ina maana kumbe chama ni overpower hata kwa mamlaka za Uraisi?Hapana!
Mashauri ya kinidhamu tu ndiyo yanapelekwa bungeni.
mistari yako miwili ya mwisho inanichanganya mkuuTo contest vs To Hold....
Which is Which ???
Katiba mbili zinakinzana!
Hivyo hapa katiba ya Kiswahili ndiyo halali......!
Kushika na Kugombea ni vitu viwili tofauti kabisaaa.........!
Alisemaga ni kijitabu lakini hicho kijitabu ndo kilimuweka pale na ndo kinamlinda na hayo yote ayafanyayo asiguswe. Akiguswa watarejea kwenye hicho kijitabu. Sijui kwanini alidharau katiba inayomlinda na kumpa umungu mtu.Hili katiba linampa mtu moja nguvu ya kuwanyongea wenzake halafu yeye yupo "SAFE" aguswi.
Huyu mtu anaweza kuuwa wote likataka kubaki yeye tu Tanzania
Nina maswali machache..Naona mwanasheria mkuu wa serikali anasema hapa kuwa" Nafasi ya Makamu wa Rais ilikoma baada ya nchimbi kuvuliwa uanachama."
Tafsiri yake kumbe chama linaweza kutoa maelekezo kwa serikali, ndio maana kunatakiwa kuwa na mipaka ya wazi kati ya chama na serikali, haya mambo yasipopata ufumbuzi wa haraka yataleta shida sana.
Hilo ni sahihi kabisa kwa sababu yule mtu nMakamu wa Raisi akishapelekwa kwenye uchaguzi mkuu na kupita, basi CCM haina nguvu dhidi yake kwa namna yoyote ile. Sababu ni za kisheria kabisa na ziko dhahiri:
Mosi, makamu wa Raisi ni mtumishi wa ummah siyo mtumishi wa CCM.
Pili, makamu wa Raisi anateuliwa na watanzania siyo CCM.
Tatu, makamu wa Raisi anaongoza nchi ya Tanzania siyo nchi ya CCM.
Kwa hiyo sababu zilizowafanya wamuondoe sio za kinidhamu ndio maana hawakumpeleka Bungeni wakaamua wamuadhibu kichamaa,ina maana kumbe chama ni overpower hata kwa mamlaka za Uraisi?
Duh. Okey.
mistari yako miwili ya mwisho inanichanganya mkuu