Ni mbinu gani ambayo CCM wataitumia kutengua maamuzi ya wachache kwenye kikao cha kustukiziwa kuingizwa kwa agenda ya uteuzi wa jina la mgombea Urais ilihali hata meza kuu haikuwa na agenda hiyo?
Sauti iliyosikika ikiwataka wajumbe wa NEC kupitisha majina ya wagombea Urais inajulikana kabisa, na ndani yake ikiwa na maslahi ya upande ya watu wachache
Sasa kwa yanayoendelea, wandamizi na wakongwe ndani ya ccm wanajuta huku wakiulizana wafanye nini kutengua maamzi hayo!
Na au tutegemee usemi alilolitumia Rais Msataafu JK kuwa, mambo yakiwa mabaya zaidi, watamng'oa? Mpaka muda huu unadhani mambo mabaya chini ya uongozi wake hajafikia kiwango cha yeye kung'olewa na wana ccm?
Kusema kwamba mambo hajawa mabaya ni kujidanganya,, CCM ni kubwa ina watu wengi weledi, wana ccm msiache haya mambo yaharibu chama chenu