CCM imekosa vijana wenye sifa mpaka kumpa kazi Mzee Kinana mwenye miaka 71?

CCM imekosa vijana wenye sifa mpaka kumpa kazi Mzee Kinana mwenye miaka 71?

Habari Wana JF,

Moja kwa moja kwenye mada. Hivi kwa ukongwe wa chama hiki, ni sahihi kuweka Makamu Mwenyekiti wa umri wa miaka 71?. Ina maana chama hakiandai vijana wa kuendeleza chama siku za usoni?

Karibuni tujadili.
Wasiwasi wangu ni kuwa tunarudi kile kipindi ukiwa umevaa shati au dela la kijani hata kama umenunua mtumbani tulikuwa tunazomewa ukiwa umelivaa mitaani.
 
Ninachoona ni kuwa CCM itarudi kwenye makundi na mpasuko baada ya muda si mrefu.

Huyu mama angefanya vizuri sana iwapo angeunda CCM na serikali ya kwakwe iwapo alikuwa hataki kuendeleza iliyoachwa na aliyekuwa mkuu wake wa kazi, kuliko kuokoteza CCM na serikali ya Kikwete ambayo ilikuwa na sifa kubwa sana ya makundi wakiyaita mtandao, na ufisadi uliopelekea ile list of shame!
 
Ninachoona ni kuwa CCM itarudi kwenye makundi na mpasuko baada ya muda si mrefu. Huyu mama angefanya vizuri sana iwapo angeunda CCM na serikali ya kwakwe iwapo alikuwa hataki kuendeleza iliyoachwa na aliyekuwa mkuu wake wa kazi kuliko kuokoteza CCM na serikali ya Kikwete ambayo ilikuwa na sifa kubwa sana ya makundi wakiyaita mtandao, na ufisadi uliopelekea ile list of shame!

Nikweli TLS walimshauri avunje Baraza la mawaziri.

Lakini yeye kaweka viraka, yajayo yanafurahisha.
 
Habari Wana JF,

Moja kwa moja kwenye mada. Hivi kwa ukongwe wa chama hiki, ni sahihi kuweka Makamu Mwenyekiti wa umri wa miaka 71?. Ina maana chama hakiandai vijana wa kuendeleza chama siku za usoni?

Karibuni tujadili.
Achana na umri ndugu.

Utasemaje kuhusu Biden naye?
 
Nikweli TLS walimshauri avunje Baraza la mawaziri.Lakini yeye kaweka viraka.yajayo yanafurahisha.
Ushauri wa TLS ulikuwa na makosa sana kwani wao walimchukulia kama vile ni rais aliyeapishwa baada ya uchaguzi hivyo alitakiwa aunde serikali mpya kutokana na wabunge wapya waliochaguliwa kwenye bunge jipya.

Walisahau kuwa yeye aliapishwa kuwa rais kutokana na nafasi aliyokuwa nayo serikalini kama makamu wa rais ili kuendeleza serikali iliyokuwapo kutoka kwenye bunge lile lile. Ndiyo maana mara baada ya kuapishwa, kikao chake cha kwanza hukifanya na baraza la mawaziri alilorithi.

Hata hivyo, baada ya kushika ofisi anakuwa na powers kufanya reshufle kwa namna yoyote kama anavyofanya sasa. Anatakiwa kutumia powers hizo kusuka serikali yake upya kwa flavor yake mwenyewe, siyo kama ambayo TLS walivyokuwa wanataka kumpotosha.

Ila sasa kama flavor yake ni ile ya Kikwete, basi hapo kuna tatizo.

Anaanza kuzipa nguvu zile conspiracy theories zilizoenea baada ya kifo cha Magufuli kuwa aliuwawa makusudi.
 
Ninachoona ni kuwa CCM itarudi kwenye makundi na mpasuko baada ya muda si mrefu. Huyu mama angefanya vizuri sana iwapo angeunda CCM na serikali ya kwakwe iwapo alikuwa hataki kuendeleza iliyoachwa na aliyekuwa mkuu wake wa kazi kuliko kuokoteza CCM na serikali ya Kikwete ambayo ilikuwa na sifa kubwa sana ya makundi wakiyaita mtandao, na ufisadi uliopelekea ile list of shame!

Unadhani rahisi mkuu uunde kila kitu upya. Unawatoa wapi?

Yeye mwenyewe sio mpya. Kuongoza Nchi sio majaribio.

This is Tanzania not America ambapo system ya mambo mengine inabaki na haijalishi nani yupo madarakani.
 
Ushauri wa TLS ulikuwa na makosa sana kwani wao walimchukulia kama vile ni rais aliyeapishwa baada ya uchaguzi hivyo alitakiwa aunde serikali mpya kutokana na wabunge wapya waliochaguliwa kwenye bunge jipya. Walisahau kuwa yeye aliapishwa kuwa rais kutokana na nafasi aliyokuwa nayo serikalini kama makamu wa rais ili kuendeleza serikali iliyokuwapo kutoka kwenye bunge lile lile. Ndiyo maana mara baada ya kuapishwa, kikao chake cha kwanza hukifanya na baraza la mawaziri alilorithi.

Hata hivyo, baada ya kushika ofisi anakuwa na powers kufanya reshufle kwa namna yoyote kama anavyofanya sasa. Anatakiwa kutumia powers hizo kusuka serikali yake upya kwa flavor yake mwenyewe, siyo kama ambayo TLS walivyokuwa wanataka kumpotosha. Ila sasa kama flavor yake ni ile ya Kikwete, basi hapo kuna tatizo. Anaanza kuzipa nguvu zile conspiracy theories zilizoenea baada ya kifo cha Magufuli kuwa aliuwawa makusudi.

Nimekuelewa mtaalam Asante Sana.
 
Unadhani rahisi mkuu uunde kila kitu upya. Unawatoa wapi? Yeye mwenyewe sio mpya. Kuongoza Nchi sio majaribio. This is Tanzania not America ambapo system ya mambo mengine inabaki na haijalishi nani yupo madarakani.

Kwa haya yanayotokea je Kuna umuhimu wa Katiba mpya?.
 
Sasa vijana wenyewe kama Happi, sabaya, makonda, pole pole bora wazee wajifie madarakani.

Sio kama hawapo wapo ila wakipewa madaraka ubadilika, binafsi sielewi.
 
Tena kwa kuwalipa fedha nene na kuwapa vyeo
🤣

20220327_135442.jpg
 
Kile cheo kinahitaji mtu mzima na busara zake...hata Mh.Magufuli alifanya yote lakin pale alimuacha Mangula
 
Wasiwasi wangu ni kuwa tunarudi kile kipindi ukiwa umevaa shati au dela la kijani hata kama umenunua mtumbani tulikuwa tunazomewa ukiwa umelivaa mitaani.
Usisahau Kuna kipindi kilipita pia cha kukamatwa kwa kumsema raisi vibaya.

Kipindi ambacho marufuku ya kuongea siasa kwenye daladala ilikuwepo.

Uhuru wa kuzomea bila kukamatana ukiwepo ni sawa japo si busara kuzomeana.
 
Back
Top Bottom