CCM imeshindwa kumuua Lissu kwa risasi, imeamua kumuua kupitia mahakama

CCM imeshindwa kumuua Lissu kwa risasi, imeamua kumuua kupitia mahakama

Kuita hii ni njama ya CCM sio sawa. Balozi wa CCM mtaani kwako naye anamshtaki Lissu kwa uhaini? Ibaki kuwa hii ni njama ya watu wachache kwa maslahi yao wenyewe.

Nakubaliana na ww kuwa dalili ya mvua ni mawingu. Kama kwenye kila hoja upande wa mashtaka umeshinda, ni wazi kuwa hata kesi ya msingi Jamhuri watashinda.

Hukumu ya kumnyonga ikitoka, biashara ya Lissu ndio itakuwa imeishia hapo. Hatawasipotekeleza adhabu ya kumyonga watamwacha aozee deathrow maisha yake yate.

Hili litakuwa ni anguko kubwa kabisa la haki za binadamu, uhuru wa maoni na democracy ya ushindani wa vyama vingi.

Mpaka Sasa Lissu yupo deathrow. Nimesema ni CCM kwa minajili ya kwamba wao ndio wenye serikali.
 
Hii Nchi inahitaji ukombozi mwingine tukiacha ule tuliopata kutoka klwa Mzungu,
Wananchi tunaona dhuluma na uonevu lakini tunaishia kulalamika tu bila kuchukua hatua yoyote,
Vyama vya upinzani vinafurahia kuiona chadema kwenye mkwamo wa kisiasa na wao wanaichukua kama fursa ya kukwea kisiasa,kumbe wangeungana na kususa wote uchaguzi Reforms zingefanyika tu kwani ccm isingekuwa na uwezo wa kufanya uchaguzi wao wenyewe,
Wananchi tumebakia kimya ,hakuna haki za binadamu wala taasisi za kiraia zinazopaza sauti.
Leo Lissu kabaki mwenyewe bila mtetezi,Tuna safari ndefu sana,ingekuwa Kenya mpinzani kafanyiwa hivi ni maandamano mwanzo mwisho mpaka kieleweke,

Umeongea jambo la msingi Sana. Vyama vya upinzani vimepoteza golden chance ya kufanya reforms za maana.
 
Kwa jinsi mahakama ya kisutu kwenye kesi ya Lissu inavyoendeshwa ni kwamba inaendeshwa kwa maelekezo ya serikali ya CCM.

CCM huko nyuma walipanga kumuua kwa risasi 16 ila Lissu akapona. Sasa naona wamejipanga kumuua kwa kupitia mahakama. Kuna kila dalili maamuzi yameshapangwa ni mahakimu na majaji wa kesi hiyo kutekeleza.

Sababu zinazonifanya niamini ya kwamba CCM kupitia mahakama zake imedhamilia mumnyonga Lissu ni yafuatayo.

1. Kwanza, Hakimu kukubali kila ombi la upande wa mashtaka hata halikiwepo. Nimeshangaa Leo Wakili wa serikali anamuomba Hakimu atoe Amri kabla ya Rulling na kweli Hakimu akatoa Amri kabla ya Rulling.

2. Pili, kukubali kuficha mashahidi baadala ya kuwalinda. Yani mahakama imeamua kuwa na mashahidi ambao hawatajulikana kwa majina. Yote hii ni kutengeneza mashahidi wa uongo watakao kuja kutoa ushahidi wa uongo na wa kutunga ili mahakama imnyonge Lissu kwa kutumia mashahidi wa mchongo.

3. Tatu, kesi kusikiliza gizani. Kwa amri ya mahakama Kuu ni kwamba kesi ya Lissu haitakiwi kurushwa au kuchapishwa na chombo chochote Cha habari. Hii itakuwa kesi ya kwanza ya uhaini kutochapishwa popote. Maana yake hata waliopo mahakamani hawaruhusiwi kuandika chochote kuhusu hiyo kesi. Maana ni kwamba hata kama mahakama imekosea.

Hivyo basi nikiri ya kwamba kwa Sasa serikali ya CCM imedhamilia kumnyomga Lissu hata iweje.
Vyovyote watakavyo fanya ila tambua watesi wake nao watakufa hawata ishi milele,tena watadhihakiwa wafapo.
 
Back
Top Bottom