CCM inahitaji pongezi nchi hii, tulipotoka tunapajua wenyewe. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni

Mleta mada analinganisha Tanzania ilivyo sasa na huko zamani na kuhitimisha kuwa serikali ya chama cha mapinduzi imefanya kazi kubwa sana kwamba hali ilivyo sasa ni juhudi za ccm hivyo tuipongeze, sasa najiuliza kama Tanzania ilivyo sasa ccm wanahitaji kupongezwa je vp Tanzania ingekuwa endapo ccm isingekuwa imefanya vizuri kwa mtazamo wa mleta mada?

Kwa sababu zipo nchi ambazo zina umri sawa na sisi ila zimetupita mbali sana kimaendeleo bila ya shaka nao kama wasingefanya juhudi basi wangekuwa kama sisi maana tulikuwa wote sawa, ila sisi tunajilinganisha sisi wenyewe et tulipotoka na tulipo kwa miaka yote 60 na kujiona tumefanya makubwa sana.

Rais Samia anasema tusijilinganishe na nchi za wenzetu huko zilizoendelea zenye miaka zaidi ya 200, sawa ila mbona hata nchi zenye miaka sawa na sisi pia zimetupita mbali kimaendeleo?

Kwa mitazamo ya mleta mada anataka kuzidi kudumaza akili zetu kujiona tunaenda sawa na wakati katika maendeleo, miaka 60 ya kujitawala bado tu watu wanakosa hata maji safi ya kunywa na wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati achilia mbali ubovu wa elimu yenyewe halafu mtu anataka tupongezane kwa hali hiyo sasa kinyume chake ndio hali ingekuwaje?
 
Mada hii nzuri mno
Mimim naanzia hapa. Kwako kwa kukuunga mkono.
Pia namuunga mkono
Nelson Jacob lushasi.
CCM imezeeka sana kkifikra na haiwezi tatua matatizo ya nchi hii.
Ina fikra za kiukombozi zaidi kuliko za kisasa.
Kinahitajika Chama Kingine chenye muono chanya.
 
CCM ndio sababu ya Ufukara wetu, niheri tungeendelea kutawaliwa na wakoloni
Mkoloni angeendelea kuitawala hii nchi Tanzania ingekuwa first world country Leo , alaaniwe Nyerere na vibaraka wake wanyonya damu ,uchu tu wa madaraka kwa ubinafsi wao ili kuneemdzha matumbo na familia zao
 
CCM ndio inatakiwa itushukuru sisi Wananchi.

Kupitia Sisi Viongozi wa CCM wameneemeka, Watoto wao mpaka Vijukuu na Vitukuu future yao ni Bright.
 

Mimi kwa kukuunga mkono UHURU JR
Naitazama Zanzibar nchi yangu, jinsi ilivyorudishwa nyuma na CCM kwa miaka hiyo 60 ni (Umasikini, Maradhi, na Ajira) Mambo haya makuu bado ni kitendawili hapa kwetu.

Zanzibar Imezungukwa na bahari ,lakini kwetu imekuwa kama Laana CCM wameshindwa kuinufaisha nchi kwa bahari.

Zanzibar ina rasilimali ya Mafuta na Gesi ,CCM wameshindwa kuchimba. Zanzibar ina Population Ndogo mno lakini hakuwa faraja kwa kuwa kwetu kidongo na wingi wa rasilimali, CCM imeshindwa kutumua Mwanya huu.

Mtaendelea kisifu kwa lipi? Wanashindwa kuleta maendeleo Edelevu badala yake wametuzamisha kwenye Klimo cha mwani huku wakiua kile cha Karafuu.
 
Mkoloni mwingereza alikuwa ni bora mara 1000 zaidi ya mkoloni nyapara ,muuaji na mnyonya damu ccm
 
CCM wamechelewa,

CCM walitakiwa waanzishe na kukiimarisha chama kinzani tangu 1977, mwaka 1992 wangeweza pia.

Wangeanzisha chama na kukipa nguvu chini Kwa chini na kukipa nguvu.

Chama hicho kingefanyika mbadala baada ya kuiua CCM,

CCM imezeeka, Vyama vya upinzani havina HOJA nzito saaana, wanapata uungwaji mkono sababu tu ya kuchokwa CCM.

CCM imebaki pekee chama kikongwe kilicho hai.

Walijaribu kujivua GAMBA, lilipofika kiunoni likangangania,

CCM must die,

Na KATIBA mpya ndo tiketi ya mwisho kuiua CCM,

Tukishindwa kuiua CCM Kwa HOJA ya KATIBA mpya, basi haitotoka kamwe.
 
Unaongea kisiasa au kama msomi
 
Unaongea kisiasa au kisomi mdogo wangu
 
Miaka hiyo ya 1960 tujilinganishe ni zile Nchi tulizokuwanazo sawa !!
 
Pongezi kwa kuleta gongo na kamari?
Bwana Mshana , nakukubali sana mkuu.
Tazama Kuhusu Huu Muungano , CCM wameunda Tume zaidi ya 3 na kupewa maoni chanya ya kuleta Serikali 3 ,lakini wao bado wanangangania 2 kelekea moja.

Walipoungana walisema wanataka kuleta Umoja wa Afrika.
lakini tazama katiba waliyoiandika haikuweka mwanya wa nchi nyingine kujiunga na Muungano huu.
Huii nikunesha kufeli kwa azma yao hii kama ilivyofeli Ujamaa wa Nyerere.
 
Tutajie hayo mafanikio ya kujivunia na mapungufu yenu mpaka Sasa.
 
Mkoloni angeendelea kuitawala hii nchi Tanzania ingekuwa first world country Leo , alaaniwe Nyerere na vibaraka wake wanyonya damu ,uchu tu wa madaraka kwa ubinafsi wao ili kuneemdzha matumbo na familia zao
Una hakika na uyasemayo mdogo wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…