CCM inaweza kutuambia nani aliwaua waliouawa Oktoba 29?

CCM inaweza kutuambia nani aliwaua waliouawa Oktoba 29?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Viongozi waandamizi wa CCM wanazunguka nchi nzima pamoja na mambo mengine wanatoa shutuma kwamba kuna watu walihamasisha vijana wa kitanzania kuandamana Oktoba 29 mwaka 2025.

Viongozi hao wa CCM husema vijana hao walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane.

Na kwenye mikutano yao hiyo huelezea kwa kina jinsi vijana hao walivyochoma majengo, vituo vya mafuta na magari.

Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.

Ina maana viongozi wa CCM wanajua kulikuwa na maandamano na uharibifu wa mali ila hawajui kama kuna watu waliuawa na ni kina nani waliowaua watu hao?​
 
Huyo ka Spagghett ashachanganyikiwa mpaka Masihi anashindwa kuelewa atamtoaje mapepo ya Lumumba!
 

Attachments

  • 1786437840776.jpg
    1786437840776.jpg
    55.7 KB · Views: 10
Viongozi waandamizi wa CCM wanazunguka nchi nzima pamoja na mambo mengine wanatoa shutuma kwamba kuna watu walihamasisha vijana wa kitanzania kuandamana Oktoba 29 mwaka 2025.

Viongozi hao wa CCM husema vijana hao walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane.

Na kwenye mikutano yao hiyo huelezea kwa kina jinsi vijana hao walivyochoma majengo, vituo vya mafuta na magari.

Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.

Ina maana viongozi wa CCM wanajua kulikuwa na maandamano na uharibifu wa mali ila hawajui kama kuna watu waliuawa na ni kina nani waliowaua watu hao?​

Ukiwa una D mbili utaelewa kuwa Katambi ametusanua.

Waliopewa pesa na Kuvuta bangi sio walioandamana na kuuliwa. Bali ni wale mapolisi.
Hainijii akilini Polisi uone Mmama anakimbilia ndan , kakugeuzia mgongo alaf ww una mshoot. Tena sio mguuni. Ni mgongoni ili umuue.

Uone mtoto wa miaka 7 katumwa dukan alaf umpige risasi ya Tumboni.

Uone mtu ndan ya nyumba na ina geti lake alaf umpige risasi ya Kichwa.

Waliovuta bangi ni wao. Na yamkini waliahidiwa kila ukiua una Bonus.
 
Waliopewa pesa na Kuvuta bangi sio walioandamana na kuuliwa. Bali ni wale mapolisi.
Hainijii akilini Polisi uone Mmama anakimbilia ndani...
Lakini hakuna mahali viongozi wa CCM wamewahi kusema kuwa walioua waandamanaji ni polisi.

Inaonesha hata machawa wao humu JF hawajui nani aliwaua wale waandamanaji. Maana kama wengewajua wangeshawataja.
 
Tatizo kubwa hapa si maandamano pekee, bali mfumo mzima wa uchaguzi na utawala. Tume huru ya uchaguzi ilipaswa kulinda uadilifu wa uchaguzi na demokrasia, lakini ilitangaza ushindi wa Samia wa 98.8% wakati vituo vingi vya kupigia kura vilikuwa vimechomwa au kuvurugwa. Hata kama mtu anaunga mkono CCM, ni lazima ajiulize: uchaguzi wenye uadilifu unapimwaje kama mazingira ya kupiga kura yenyewe yaliharibiwa kwa kiwango hicho?

Na Bunge ambalo karibu 100% linatawaliwa na CCM haliwezi kuwa chombo cha kutosha cha kuchunguza kwa uhuru nani alihusika na vurugu na vifo. Hapo ndipo tunahitaji taasisi huru, si taasisi ambazo zinaweza kuwa na mgongano wa maslahi.

Kwa mtazamo wangu, Katiba Mpya ni sehemu muhimu ya suluhisho. Serikali yenyewe inajua kwamba bila mabadiliko ya msingi ya kikatiba, ni vigumu kujenga governance yenye checks and balances za kweli. Leo CCM inaendelea kuishi kwa kutegemea zaidi nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama, huku viongozi wa upinzani wakikabiliwa na vitisho, mateso na mashinikizo ya kisiasa.

Na kama mahakama nayo itaonekana kucheza upande wa chama tawala katika kesi zinazowahusu viongozi wa upinzani, basi tatizo linakuwa kubwa zaidi. Hebu fikiria nchi ambayo wananchi hawawezi kuwa na uhakika kwamba Tume ya Uchaguzi ni huru, Bunge ni huru, mahakama ni huru, na vyombo vya dola vinaweza kutumika dhidi ya wapinzani.

Hapo hatuzungumzii tena CCM vs CHADEMA. Tunazungumzia aina ya nchi tunayotaka Tanzania iwe. Serikali inaweza kushinda uchaguzi, lakini taasisi huru ndizo zinazolinda demokrasia. Bila Katiba yenye kuweka checks and balances za kweli, hata chama kizuri kikipewa nguvu zote kinaweza kuanza kuitumia vibaya.


View: https://youtu.be/cBl8xuayJUo?si=UwuGpCdNaTImT3Cd
 
Viongozi waandamizi wa CCM wanazunguka nchi nzima pamoja na mambo mengine wanatoa shutuma kwamba kuna watu walihamasisha vijana wa kitanzania kuandamana Oktoba 29 mwaka 2025.

Viongozi hao wa CCM husema vijana hao walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane.

Na kwenye mikutano yao hiyo huelezea kwa kina jinsi vijana hao walivyochoma majengo, vituo vya mafuta na magari.

Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.

Ina maana viongozi wa CCM wanajua kulikuwa na maandamano na uharibifu wa mali ila hawajui kama kuna watu waliuawa na ni kina nani waliowaua watu hao?​
Vijana wale hawakuwa wanaamdamana, bali walikuwa wanafanya fujo na vurugu ili nchi iingie kwenye machafuko. Walichokipata walistahili!
 
Back
Top Bottom