CCM inaweza kutuambia nani aliwaua waliouawa Oktoba 29?

Viongozi waandamizi wa CCM wanazunguka nchi nzima pamoja na mambo mengine wanatoa shutuma kwamba kuna watu walihamasisha vijana wa kitanzania kuandamana Oktoba 29 mwaka 2025.

Viongozi hao wa CCM husema vijana hao walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane.

Na kwenye mikutano yao hiyo huelezea kwa kina jinsi vijana hao walivyochoma majengo, vituo vya mafuta na magari.

Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.

Ina maana viongozi wa CCM wanajua kulikuwa na maandamano na uharibifu wa mali ila hawajui kama kuna watu waliuawa na ni kina nani waliowaua watu hao?​
Very difficulty qns
 
Ndugu yangu Aleni. Allen Kilewella , jifunze kutenganisha chama na serikali, CCM watajuaje nani aliteua nani kama hata serikali yenyewe haijui ndio maana imeunda tume kuchunguza.

Acheni kuionea CCM kwa makosa ya serikali, CCM ni chama na serikali ni dola, ni vitu viwili tofauti.
P
 
Sasa Pasco gari likigonga mtu analaumiwa dereva au gari?

Serikali yetu ni sawa na gari na CCM ndiyo dereva wake kwa sasa. Kwa yaliyotokea kama CCM haijui kuna faida gani yenyewe kendelea kuwa madarakani?

Mbona kwenye kujenga barabara hamsemi ni Serikali imejenga badala yake hutuambia ni utekelezaji wa Ilani ya CCM?
 
Vyovyote iwavyo,kwa utetezi wa chama chako na kuzungusha jibu ligeuke swali.Kwani msemaji wa serikali ni nani?Anashindwa nini kuwataja wauaji!?
 
Hofu yangu pengine Kuna kitu umetumia sasa sijui
ni kimiminika ❗️

au msokoto wa Majani na kokwa zake❗️
Sababu mado yako
inafikirisha kiwepesi🦘

Umejibiwa bado utaki jibu‼️
 
Umejibiwa bado utaki jibu‼️
Jibu halifanani na swali. Pasco kapuyanga kimakusudi.

Serikali haijiendeshi bali huendeshwa na chama cha siasa na chama hicho kwa sasa ni CCM.

Kama CCM wanaweza kuzunguka nchi nzima na kusema kuna watu walilipwa kushawishi wengine kuandamana, inakuwaje CCM ishindwe kujua walioua waliokuwa wanaandamana?

Na kumbuka mara zote wana CCM wengi hutumia nyadhifa zao za kiserikali kutoa shutuma hizo. Sasa inakuwaje kwenye kutaja nani aliyeua waandamanaji mnataka Serikali itenganishwe na CCM?

ndugu yangu Pascal Mayalla unadhani kati ya CCM na Serikali nani anayejua ni kina nani waliua watu Oktoba 29?
 
Mlidhani miundombinu aina mwenyewe
Wkt mnalalamika Serikali kukopa zaidi
Ayo mapesa ndio yamewekezwa mule

Siku nyengine mkiwa na hasira
kwanza muanze kuchoma magodoro ya Wazazi wenu✅️

kisha nyumba za wazazi wenu✅️

mtabaki salama kwa %100
Lkn Miundombinu ya Serikali ni Hatari Hatari Hatari Hatari 💥💥
 
Viongozi waandamizi wa CCM wanazunguka nchi nzima pamoja na mambo mengine wanatoa shutuma kwamba kuna watu walihamasisha vijana wa kitanzania kuandamana Oktoba 29 mwaka 2025.

Viongozi hao wa CCM husema vijana hao walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane.

Na kwenye mikutano yao hiyo huelezea kwa kina jinsi vijana hao walivyochoma majengo, vituo vya mafuta na magari.

Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.

Ina maana viongozi wa CCM wanajua kulikuwa na maandamano na uharibifu wa mali ila hawajui kama kuna watu waliuawa na ni kina nani waliowaua watu hao?​
Hao waliowashawishi watu wafanye fujo kuvuruga uchaguzi mpaka watoto wa watu wakafa juzi wamekaa Ikilu na kupata lanch na raisi

Msipo jitambua mtakufa sana
 
Jibu halifanani na swali. Pasco kapuyanga kimakusudi.

Serikali haijiendeshi bali huendeshwa na chama cha siasa na chama hicho kwa sasa ni CCM.

Kama CCM wanaweza kuzunguka nchi nzima na kusema kuna watu walilipwa kushawishi wengine kuandamana, inakuwaje CCM ishindwe kujua walioua waliokuwa wanaandamana?

Na kumbuka mara zote wana CCM wengi hutumia nyadhifa zao za kiserikali kutoa shutuma hizo. Sasa inakuwaje kwenye kutaja nani aliyeua waandamanaji mnataka Serikali itenganishwe na CCM?

ndugu yangu Pascal Mayalla unadhani kati ya CCM na Serikali nani anayejua ni kina nani waliua watu Oktoba 29?

Pamoja na kwamba mlengwa kaka yangu Pascal👈
lkn namm nikipata muda nitajibu hoja yko✍️
 
Vyovyote iwavyo,kwa utetezi wa chama chako na kuzungusha jibu ligeuke swali.Kwani msemaji wa serikali ni nani?Anashindwa nini kuwataja wauaji!?
Msemaji wa serikali atawajuaje wauaji kama hata serikali yenyewe haiwajui?, ndio maana imeunda tume!, subirieni taarifa ya tume, mtawajua, mbona mna haraka na kuweweseka hivi?.

Ila inajua watu walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane... Kwani Serikali haijui kilichotokea kwenye maandamano?

Pasco😀😃
 
Ni chama gani kinachoendesha Serikali yetu kwa sasa? Kama kila siku CCM wanasema kuna watu walihamasisha watu kuandamana... Inakuwaje CCM hao hao hawajui walioua walioandamana?
Makosa yanatazamwa na chama cha siasa kumbe?
 
Back
Top Bottom