Tatizo kubwa hapa si maandamano pekee, bali mfumo mzima wa uchaguzi na utawala. Tume huru ya uchaguzi ilipaswa kulinda uadilifu wa uchaguzi na demokrasia, lakini ilitangaza ushindi wa Samia wa 98.8% wakati vituo vingi vya kupigia kura vilikuwa vimechomwa au kuvurugwa. Hata kama mtu anaunga mkono CCM, ni lazima ajiulize: uchaguzi wenye uadilifu unapimwaje kama mazingira ya kupiga kura yenyewe yaliharibiwa kwa kiwango hicho?
Na Bunge ambalo karibu 100% linatawaliwa na CCM haliwezi kuwa chombo cha kutosha cha kuchunguza kwa uhuru nani alihusika na vurugu na vifo. Hapo ndipo tunahitaji taasisi huru, si taasisi ambazo zinaweza kuwa na mgongano wa maslahi.
Kwa mtazamo wangu, Katiba Mpya ni sehemu muhimu ya suluhisho. Serikali yenyewe inajua kwamba bila mabadiliko ya msingi ya kikatiba, ni vigumu kujenga governance yenye checks and balances za kweli. Leo CCM inaendelea kuishi kwa kutegemea zaidi nguvu ya vyombo vya ulinzi na usalama, huku viongozi wa upinzani wakikabiliwa na vitisho, mateso na mashinikizo ya kisiasa.
Na kama mahakama nayo itaonekana kucheza upande wa chama tawala katika kesi zinazowahusu viongozi wa upinzani, basi tatizo linakuwa kubwa zaidi. Hebu fikiria nchi ambayo wananchi hawawezi kuwa na uhakika kwamba Tume ya Uchaguzi ni huru, Bunge ni huru, mahakama ni huru, na vyombo vya dola vinaweza kutumika dhidi ya wapinzani.
Hapo hatuzungumzii tena CCM vs CHADEMA. Tunazungumzia aina ya nchi tunayotaka Tanzania iwe. Serikali inaweza kushinda uchaguzi, lakini taasisi huru ndizo zinazolinda demokrasia. Bila Katiba yenye kuweka checks and balances za kweli, hata chama kizuri kikipewa nguvu zote kinaweza kuanza kuitumia vibaya.
View: https://youtu.be/cBl8xuayJUo?si=UwuGpCdNaTImT3Cd