CCM inaweza kutuambia nani aliwaua waliouawa Oktoba 29?

CCM inaweza kutuambia nani aliwaua waliouawa Oktoba 29?

Msemaji wa serikali atawajuaje wauaji kama hata serikali yenyewe haiwajui?, ndio maana imeunda tume!, subirieni taarifa ya tume, mtawajua, mbona mna haraka na kuweweseka hivi?.
P
We jamaa huwa unatoa vituko aidha kwa kutokujua au una tabia hiyo damuni.
-walioandamana wametajwa.
-waliowahonga elfu tatutatu waandamane tumeambiwa walitoka nje ya nchi.
-umri wa walioandamana (kuanzia miaka 5 kuendelea)umetajwa.
-nguvu iliyotumika imeainishwa.
Sasa,kama walionwa hadi wanavyoandamana,ilikuwaje wauaji wasionwe?Au uonaji uliishia kwa waandamanaji tu?Au wauaji hawakuonekana kwa sababu walikuwa katika hali ya upepo walivuma na kupotea?
 
Kama uelewa wako ni mdogo ni kosa langu?
Hakuna cha uelewa mdogo, unaogopa tu kunyoosha maelezo ya kuwa Samia ni serial killer, ameua maelfu ya Watanganyika in a span of three days regardless justifications mtakazokuja nazo. Simple and plain.
 
Viongozi waandamizi wa CCM wanazunguka nchi nzima pamoja na mambo mengine wanatoa shutuma kwamba kuna watu walihamasisha vijana wa kitanzania kuandamana Oktoba 29 mwaka 2025.

Viongozi hao wa CCM husema vijana hao walivutishwa bangi na kupewa hela ili waandamane.

Na kwenye mikutano yao hiyo huelezea kwa kina jinsi vijana hao walivyochoma majengo, vituo vya mafuta na magari.

Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.

Ina maana viongozi wa CCM wanajua kulikuwa na maandamano na uharibifu wa mali ila hawajui kama kuna watu waliuawa na ni kina nani waliowaua watu hao?​
Hakuna Maridhiano mpaka waliohusika kuua ndugu zetu oct 29 na waliohusika kuwateka na kuwaua kina Polepole,soka,kibao,mdude na wenzao wote wanakamatwa na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria.

Kama hawajui wawaite Scotland Yard waje kuwasaidia kuwabaini na kuwatia mikononi na kuwapeleka kwa PILATO.
 
Vyombo vya dola ambavho

Nimeishajibu. Kama wewe hujapata jibu sio tatizo langu. Ila ujue tu, nchi hii italindwa kwa gharama yoyote ile dhidi ya watu wasio itakia mema na amani, hata kwa kutoa uhai wa watu hao waovu! Ushanfahamu?
Wezi nyie mshazoea kuiba chaguzi na rasilimali hamwezi kukubali mabadiliko hadi mlazimishwe.
 
We jamaa huwa unatoa vituko aidha kwa kutokujua au una tabia hiyo damuni.
Sasa,kama walionwa hadi wanavyoandamana,ilikuwaje wauaji wasionwe?Au uonaji uliishia kwa waandamanaji tu?Au wauaji hawakuonekana kwa sababu walikuwa katika hali ya upepo walivuma na kupotea?
Mkuu, Moise, Moisemusajiografii , mimi ni miongoni mwa members humu ambao tumeandika sana kuhusu hili jambo.
Kwanza hebu soma nyuzi zangu hizi mbili halafu uniambie umeelewa nini.
1. Ili Haki Itendeke, Sio Tuu Itendeke, Bali ni Lazima Ionekane Imetendeka!, Kama Tumewashitaki Waandamanaji, Pia Tuwashitaki na Wauaji!
2.Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!
P
 
Wezi nyie mshazoea kuiba chaguzi na rasilimali hamwezi kukubali mabadiliko hadi mlazimishwe.
Nchi Kuna mbwa wa kulazimisha mabadiliko? Na kama wapo mbona hawajayafanya? Au mnasubiri wengine ndio wafanye mabadiliko?
 
Nchi Kuna mbwa wa kulazimisha mabadiliko? Na kama wapo mbona hawajayafanya? Au mnasubiri wengine ndio wafanye mabadiliko?
Yule mwingine aliita watu nguchiro wewe unaita watu mbwa... Watu wa fani ya saikolojia husema hii ni ishara ya mwanzo wa mwisho.
 
Yule mwingine aliita watu nguchiro wewe unaita watu mbwa... Watu wa fani ya saikolojia husema hii ni ishara ya mwanzo wa mwisho.
Na sio mbwa tu. Nyumbu!!!
Yule mwingine aliita watu nguchiro wewe unaita watu mbwa... Watu wa fani ya saikolojia husema hii ni ishara ya mwanzo wa mwisho.
Sio mbwa tu. Nyumbu kabisa!
 
Lakini mpaka sasa sijaona hata kiongozi mmoja wa CCM aliyesema hadharani ni nani hasa aliyewaua wale vijana waliokuwa wanaandamana.
Hakuna hata anayeliongelea hilo, huu unyama utalipwa siku moja.
 
Ccm ni chama Dola
Japo ni kweli CCM ni chama dola, https://www.jamiiforums.com/threads...ala-dola-ccm-ni-chama-dola-ccm-ni-dola.36662/ kwasababu Mwenyekiti wa CCM, ndie Mkuu wa nchi, head of state, mkuu wa serikali, head of the government na CinC, Amiri jeshi mkuu, lakini maamuzi ya kichama, anayafanya kupitia vikao, ila maamuzi ya kiserikali, anayafanya yeye kama yeye, hivyo msifungamanishe maamuzi ya rais kama mkuu wa nchi na maamuzi ya rais kama mwenyekiti wa CCM ni vitu viwili tofauti.

P.
 
Nani kakuambia...?
Huu ndio uzuri wa jf na ndio faida kuu ya jf, wale waliobahatika kujua vitu fulani, wanawaelimisha na wengine wasiojua.

Kazi ya chama ni kuandaa ila yake ya uchahuzi na kuinadi,
Chama kinashinda, kinakuwa ndio chama tawala, kinaongoza serikali kisiasa tuu kupitia utekelezaji wa ilani yake, lakini watekelezaji wa ilani ni serikali.
CCM haina mamlaka yoyote ya kuamua, hata kumuamuru polisi kama yule.
Rais wa JMT ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, anapotoa executive orders, anatoa kama rais wa JMT na sio kama Mwenyekiti wa CCM, hivyo CCM kama chama, hakiwajibiki na matendo ya Mwenyekiti wake anayoyatenda kama rais wa JMT.

Mwenyekiti wa CCM ni kiongozi wa kisiasa tuu, lakini rais wa nchi ni mkuu wa dola!. Usiwalinganishe!.
P
 
Back
Top Bottom