Ndalilo
JF-Expert Member
- Jan 30, 2013
- 3,343
- 7,516
Wale mapapaa wa kuchop money naona wameanza tena, nimeoneshwa clip ya mdada mbongo movie, sijui ni Uwoya, akimwaga money...kuna hotel nasikia imefunguliwa Tbt, ilishindikana kwa miaka 5 iliyopita.Wacha sahizi wapewe uhuru wa kuropoka na kuandika upuuzi juu ya serikali huku serikalini watu wakijipigia mipunga na kupotezea miradi ya maendeleo 😂😂😂 watakuja kuelewa somo vizuri nk swala la muda tu!
Mungi akitujaliwa, mwakani tutafuturishana sana, ma-birthday location yakufa mtu, tutaanza kuimba majina ya wale wale tena, sijui Mwamvita, mara Riz1, mara n.k
Dizaini hiyo na chawa wao ndo wenye access na mitandao kuliko ndugu zangu kule Nanjilinji ambao ndio wanapanga foleni kupiga kura, wanapanga foleni kusubiri panadol, wanapanga foleni kuandikisha mtoto shule, wanapanga foleni kuchota maji kisimani, wanapanga foleni kupata pembejeo, walioundiwa TASAF na bado wanapewa walio masaki, pesa za visima vyao zinaishia kwa wanaotaka mzunguko wa pesa mtaani n.k
CAG alisema kati ya 27bn zilizokusanya na jiji, 3bn pekee ndo zimeenda/kuhesabiwa benki, zaidi na POS machine 80s zilizotumika kukusanya pesa hizo eti zimepotea, leo nimesikia tena kuwa POS za makusanyo za jiji lenu la Dar, zaidi ya 500 eti zimepotea, hawasemi zimepotea na pesa kiasi gani...hawa ndo wanataka mzunguko wa pesa mtaani.
Ni heri kusiwe na mzunguko wa pesa mtaani ila heshima ya shule za serikali ikarudi, kwamba ukisoma binafsi unaonekana kilaza, hizi ndo shule ndugu zangu wengi, 80% wanazimudu, pesa isiwepo mtaani ila nipate huduma bora hospitali, sio ubinafsi wa kuwa chawa kuishi kama Bashite kwa gharama za maisha ya walio wengi masikini.
Nani wakuchukua hatua? Mama anaupiga mwingi, KAZI IENDELEE