Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 11,640
- 24,066
Kuna jamaa mmoja ni pro_Ccm ni mzee mtu mzima alituambia tutakufa wote hii KarneSuala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.
Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania.
Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa kutwajulisha wenye nchi juu ya rasilimali kubwa na zinazotaka kubinafsihwa kwa kampuni ya kutoka Dubai DP World.
Suala si kubinafsisha tu, suala ni mustakabali mzima wa kisiasa, na kushindwa kwa serikali kuelezea kwa maneno mepesi na yanayoeleweka juu ya ubinafsishaji huu wa Bandari zetu.
Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali. Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.
Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.
Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wanannchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.
CCM haito Toka madarakani hayo sio maneno yangu ni ya mzee mmoja Mwana CCM kindaki ndaki....