Nimefurahi kuona kwamba wapo walioamua kulipigania hili jambo kwa njia tofauti, wapo walioamua kupambana mitandaoni, wapo walioamua kwenda mahakamani, na wapo walioandamana.
Hizo zote zimekuwa ni njia za watanganyika kufikisha ujumbe wao, kwamba hawajaridhishwa na ubovu wa ule mkataba, ulioamua kuzitoa sadaka bandari zetu zote ndani ya Tanganyika.
Mwisho wa siku naamini jambo moja, kama Samia ataendelea kuziba masikio, asisikie hizi sauti zote zinazomtaka atuondoe kwenye ule mkataba, basi atambue, siku inakuja, makundi hayo matatu yataungana kwa pamoja, yaamue kufanya jambo moja, chini ya uratibu mmoja.
Ajiandae. Kuwa kiongozi wa watanganyika maana yake ni kusimamia mali zao, lakini sio kuzigawa kwa ndugu na marafiki zako. Ni