CCM, kwa mtaji wa ukakasi wa suala la Bandari, kaeni mguu sawa kung'olewa!

CCM, kwa mtaji wa ukakasi wa suala la Bandari, kaeni mguu sawa kung'olewa!

Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , usiwe na shaka yoyote na Watanzania ni watu poa, hata uwafanyie nini, ukifika muda wa kuchagua ni kile kile chetu chama numberi uno!.
P
Wenye masikio na wasikie.
Hili swala ni kisu tumboni kwa CCM, hata mimi kada sikubaliani nalo.
Zitapigwa kura za KUIKATAA CCM 2025.
Be warned!
 
Hakuna yeyote anayesema CCM ni malaika, tatizo ni uitoe CCM, umlete nani?.
P
Huo ndio wasi wasi wa CCM, ati nani atakuja badala ya CCM.
CCM imekuwa complacent, and doing things with impunity, utafikiri wako pale daima dumu.
Hili la DP World, mark you, watakuwa chama cha upinzani.
 
Kuing'oa ccm madarakani ni ndoto za mchana ama ni kauli za kujipa moyo tu.

Kama kweli suala la DP World limewagusa njia sahihi ya kupambana na Hilo ni kutunga katiba mpya. Vinginevyo ccm itaendelea kuwepo.
Na wewe kujipa moyo kwamba katiba mpya itaing'oa sisi uoni ka ni uandawazimu??? Yaan ccm wakubali katiba itakayowatoa madarakani kweli na wewe umeona umewaza vizuri??
 
Kinachosikitisha ni taasisi kama Usalama wa Taifa, taasisi za kizalendo na zilizo ndani ya roho ya utaifa wa Tanzania, najiuliza kuwa huu ukakasi hawakuuona na kuuchukulia hatua?
Hao ni usalama wa CCM kiongozi hawako huru kama unavyodhani kwa sababu kwa ufisadi uliloko hapa kwetu walistahi adhabu

Usalama wa taifa kwao ni siyo rasilimali ya nchi yetu

Wanayo vitu wanayo Linda siyo Mali ya watanzania
 
Siyo kwa sanduku la kura na kumwachia DED atangaze matokeo. Labda wang'olewe na usalama wa taifa au wapigane fitna kwa kuvujisha Siri au mahakama ziwe huru ili wang'olewe kisheria au Mungu aamue ugomvi.
Usalama wa taifa ndo shida kubwa Hujawahi jiulize huwa wanafanya nini Hawa watu
 
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi.

Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania.

Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa kutwajulisha wenye nchi juu ya rasilimali kubwa na zinazotaka kubinafsihwa kwa kampuni ya kutoka Dubai DP World.

Suala si kubinafsisha tu, suala ni mustakabali mzima wa kisiasa, na kushindwa kwa serikali kuelezea kwa maneno mepesi na yanayoeleweka juu ya ubinafsishaji huu wa Bandari zetu.

Kama CCM haikuliona hili kuwa suala zito basi sasa ifungue macho, 2025 siyo mbali. Mimi ni kada wa chama, na kwa yote tunyoyaona mitandaoni na maelezo yasiyoeleweka kutoka Wizara husika ya Ujenzi, mikataba inayotuchanganya, bunge linaloitikia ndiyoooo, bila uchambuzi wa kina, basi kwa CCM huu ni mtaji mbaya.

Yote haya hayaleti imani kwa CCM, na huku mitaani inanyooshewa kidole cha lawama.

Mtaji huu wa mikataba ambayo ni kama tumefumbwa macho na wanannchi hawana elimu ya kutosha, CCM itavuna kama inavyostahili.
Huu ni wasiwasi wako tu. Hao hao wanaoandamana nchi nzima wakishaanza kufaidi matunda ya uwekezaji watakaa kimya na kuendelea na maisha.

Msipende kuwajaza wananchi wasiwasi usio na msingi.
 
Huu ni wasiwasi wako tu. Hao hao wanaoandamana nchi nzima wakishaanza kufaidi matunda ya uwekezaji watakaa kimya na kuendelea na maisha.

Msipende kuwajaza wananchi wasiwasi usio na msingi.
Ni ujinga kufikiri watu wanapinga bila sababu za msingi.
Kama kama Kinana na Chongolo wameelewa sijui wewe huelewi nini.
 
Kwa kweli mimi ni mwanachama hai was ccm,lakini Kwa hili la bandari hapana,hats mie nimekwazika sana,watu wamechukia ndio maana huku kwetu wakikuona umevaa shati la kijani wanakung'ong'a.
Hili Jambo limetutia haibu hata sisi wenezi tunapata tabu Sana kushawishi watu kujiunga kwenye kadi za kidigital
 
Back
Top Bottom