CCM Mwanza na Mkakati wa Kumpa Makonda Uenyekiti (M) ni Aibu ya Karne

Duru za siri zinaonyesha mkuu wa mkoa msitaafu bwana Paul Makonda anaenda kuwa mwenyekiti wa ccm wa mkoa wa Mwanza kwa kumtoa mwenyekiti wa sasa asiye na faida yoyote bwana Anthony Diallo.

Bwana Diallo alikera wengi alipotoka hadharani na kukosoa utawala wa hayati Magufuli, hivyo wadau wengi wanamuona ni kigeugeu atakayekuja kuponda pia utawala wa rais Samia hivyo lazima ang'olewe mapema.

Kwamba ukikosoa tu cheo huna? Sasa ni siasa gani hizo?
Mama mwenyewe anasemaje?
 
Hii ni aibu kubwa. Eti CCM mkoa Mwanza kuna mkakati unafanywa wakisaidiwa na wapambe toka HQ kuhakikisha uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa anakuwa Makonda iwe isiwe kwani eti yuko karibu na mama jambo ambalo sio kweli na mama mwenyekiti taifa hawezi kuagiza mtu kama Makonda mwenye kashfa kibao kama Makonda ampigie debe.

Msichafue chama kwa kuruhusu mkoa mkubwa kama huo kumpa muhuni aongoze.

Malalamiko ya chini chini sio mazuri maana yanaweza tumika katika uchaguzi mkuu
Wala haishangazi,ndio akili za ccm zilipoishia,hawana jipya,mazwazwa,machawa,waropokaji ndio wanaongoza chama,akili kubwa zinaogopwa kama ukoma ndani ya ccm,ukiwa mtu wa hovyo hovyo,yes man yes man,chawa,ndio unapewa nafasi,watu wenye akili kama Antony Mtaka, wanaogopwa balaa!!
Huyu mwamba ana akili kuriko waziri mkuu,ila siku akijaribu kuiweka nyota yake juu,atazimwa fasta.
 
Vyeti mtu mwenyewe Hana then anataka Uenyekiti labda kwa Ccm kumejaa vilaza Kama yeye wa Darasa la saba Nothing Else
 
Hii ni aibu kubwa. Eti CCM mkoa Mwanza kuna mkakati unafanywa wakisaidiwa na wapambe toka HQ kuhakikisha uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa anakuwa Makonda iwe isiwe kwani eti yuko karibu na mama jambo ambalo sio kweli na mama mwenyekiti taifa hawezi kuagiza mtu kama Makonda mwenye kashfa kibao kama Makonda ampigie debe.

Msichafue chama kwa kuruhusu mkoa mkubwa kama huo kumpa muhuni aongoze.

Malalamiko ya chini chini sio mazuri maana yanaweza tumika katika uchaguzi mkuu
Acha wafu wazike wafu wenzao
 
Yaani nyamitako huyu huyu awe Mwenyekiti wa mkoa wangu wa Mwanza? Over my dead body.
 
Huko CCM uovu ni sifa inayopendwa. Zaidi wanaunganishwa na uovu. Mimi naujua uovu wako, hivyo hutanifanya chochote hata nikifanya uovu gani. Wewe unaujua uovu wangu, basi nami sikufanyi chochote.

Wevi wa Escrow,mmoja alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa CCM. Wengine walikuwa makada.

Mabina aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM,bustoria yake, anatajwa kwamba alikuwa jambazi muuji ziwani, akipora engines za wavuvi.

Kumkataa Makonda kuwa kiongozi wa CCM itakuwa ni kumwonea. Mbona waovu wengi wa CCM vi viongozi huko CCM.
 
Yaani Makonda ampindue Dr Dialo?
Kwani yeye haruhusiwi kugombea? Kura itaamua na si maneno ya kwenye mitandao, kila mtu ana haki ya kugombea nafasi yoyote katika nchi hii irimradi anakidhi vigezo na utaratibu uliowekwa.
 
Makonda anafaa kuwa rais wa nchi hii na waziri mkuu awe Sabaya. Tutaaga umaskini haraka.

Kuwa mwenyekiti wa mkoa ni halali. Naenda kumkampenia
Hao madogo wakipewa nchi watakuwa na utajiri wa ajabu sana hata wakina Elon hawatawafikia na matajiri wa nchi hii watakoma
 
Vijana waliobakia na wanafaa kutuvusha na wana udhubutu chanya kwa maendeleo ya jamii na Mchi yetu

1. Mimi mwenyewe
2. Paulo Makonda
3. Joel Mpina

Japo nature ya dunia ilivyo ukiwa mleta mabadiliko katika famili, jamii yako na Taifa tegemea kukumbwa na kila zaga zaga ikiwemo vimbunga, shutuma, skendo, mitego, n.k
 
Duru za siri zinaonyesha mkuu wa mkoa msitaafu bwana Paul Makonda anaenda kuwa mwenyekiti wa ccm wa mkoa wa Mwanza kwa kumtoa mwenyekiti wa sasa asiye na faida yoyote bwana Anthony Diallo.

Bwana Diallo alikera wengi alipotoka hadharani na kukosoa utawala wa hayati Magufuli, hivyo wadau wengi wanamuona ni kigeugeu atakayekuja kuponda pia utawala wa rais Samia hivyo lazima ang'olewe mapema.
Kama ni Kweli wamedhamiria basi mkt hawezi kumpitisha konda sababu alipendezwa na kutukanwa Kwa Magu kupitia Diallow!!
 
Hii ni aibu kubwa. Eti CCM mkoa Mwanza kuna mkakati unafanywa wakisaidiwa na wapambe toka HQ kuhakikisha uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa anakuwa Makonda iwe isiwe kwani eti yuko karibu na mama jambo ambalo sio kweli na mama mwenyekiti taifa hawezi kuagiza mtu kama Makonda mwenye kashfa kibao kama Makonda ampigie debe.

Msichafue chama kwa kuruhusu mkoa mkubwa kama huo kumpa muhuni aongoze.

Malalamiko ya chini chini sio mazuri maana yanaweza tumika katika uchaguzi mkuu
 
Konda boy alifutwa ktk Ulimwengu wa Roho kisiasa.

Jitihada zozote za kumpambania ktk siasa ni kupoteza muda na raslimali pesa.

Nashauri ATUBU na Aombewe kwanza Ili mambo yaende sawa.

Ameeeen.
 
Tusiongee sana tusubiri mda haudanganyi!
 
Attachments

  • Screenshot_2022-10-21-09-24-30-856_com.android.chrome.jpg
    Screenshot_2022-10-21-09-24-30-856_com.android.chrome.jpg
    139.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom