CCM na Serikali jibuni hoja za Humphrey Polepole, msimzime kidola

Hapa kwa tabia ya CCM mwenyekiti wao huwa wanamuacha apite bila kupingwa, huwa wanatoa form moja tu kwa ajili ya kuomba nafasi ya kugombea urais, labda kama kwa Samia wataenda kinyume na huu utaratibu wao waliojiwekea siku za nyuma.
 
Kama Samia anamalizia tu kipindi cha awamu ya tano ya Magufuli na hii sio awamu yake basi ataruhusiwa kugombea tena kwa vipindi viwili, mwaka 2025 na mwaka 2030.
Swali hili ilitakiwa Polepole alijibu!
 
Siyo lazima ajibiwe. Wanaweza kuamua kukaa kimya au hata kumjibu kwa vitendo. Serikali na chama ni kubwa kuliko yeye
 
Iyo tafsiri ya Awamu umeitoa wapi?

ZANZIBAR kuna Awamu ya 8 saivi Polepole amewai kuwa hadi mwenezi wa CCM ulimsikia wapi akihoji hayo?

Mwambie Polepole kuna matokeo ya kumdharau Amiri Jeshi Mkuu.

Kama anataka kuyapata Safari hii atayapata!
Pole pole ni kiroboto pro max na mnafiki
 
Akimaliza kutekeleza ilani ya awamu ya tano ndio ataanza kutekeleza awamu mpya ya sita kutoka 2025 hadi 2035 kama akipata ridhaa ya chama chako na akachaguliwa na wananchi?
Anapumzika. Amemaliza hawamu yao ya tangu 2015-2025. Kilichotokea ndo hivyo kikatiba imempasa kumalizia safari waliyotuhaidi sisi wananchi Akiwa yeye kama msaidizi na Dreva mkuu katika ilani ya kurasa 303 ya 2020. Dreva kapata tatzo katkati ya safari Msaidizi kashika usukani kukamilisha mkataba wetu 2025 bila kubadri wala kuathiri masharti ya mkata wetu na wao ya Mwaka 2020.

Kuomba ridhaa ya kuwa dreva wetu 2025-2030 hiyo ni kwa utashi wake wala katiba haimlazimishi....ni kama vile ambavyo Mh.PM au VPresident anaweza kuomba nafasi hiyo hili kuongoza hawamu ya sita, wala sioni kama pana tatzo lolote lile, huu mpira zaidi unarushiwa kwetu kupima namna alivopokea usukani ..alivyotuendesha na kumaliza au kukamilisha safari ya mkataba wetu wa 2020. Hilo ni kubwa sana kwa maana kati ya 2020 na 2025 ni mkataba mmoja na wananchi uliosainiwa, na hivyo hapawezi kuwapo excuz ya kiutendaji katika huo urithi wa ilani ya 2020-2025, Ndicho kipimo chetu.

Haiwezekani tumeambiwa wakati tunapanda Bus Mbezi terminal kwamba ndani ya hili Bus kuna vinywaji baridi bure ...kisha tunafika mwisho wa safari Dodoma tuambiwe amjapewa Soda wakati wa safari yetu kama tulivyohaidi kwa sabbu Dreva alibadrishwa Nooo!!! Safari ni ile ile, Bus ni lile lile, mkataba ilani ni ile ile 2020-2025. (Tuachane na haya). Ila kiutaratbu na hili polepole haliwahi kuliongea kwamba kiutaratibu (sio kisheria) hawamu ikimaliza inaondoka na viongozi wake wa ngazi za juu wakapumzike...kisha ije safu mpya(sina uhakika..

Ila nlisikia ni kwa mujibu wa ccm utaratibu ambao pia mi nafikiri ni mzuri pia), hili ukiamua kuinanga serikali ya awamu iliyopita....yaani unainanga haswa kwa mapungufu yake, kuliko unainanga wewe Rais, kumbe makamu wako ndo huyo alikuwa makamu wa awamu iliyopita, au wewe ni Rais this term, na awamu iliyopita ulikuwa ni Waziri mkuu. Kiukweli huu ni mkanganyiko ambao unaweza kuleta kukosa uwajibikaji au kuendeleza mabaya yaleyale (on negative side) yalokuwapo wakati unahudumu kama Vp...au PM etc. On other side is good if the Gorment is fully transparent and responsbly to voters with unquestionable entagrity.
 
...
Watake wasitake, Samia kisheria anamalizia muda uliobaki wa awamu ya tano, kama akitaka kugombea tena 2025 ndio ataianza awamu ya sita, hii ni sheria inavyosema sio kelele.
... Katiba inasema endapo rais "aliyerithi" atarithi pungufu ya miaka mitatu, atakuwa na haki ya kugombea na kuchaguliwa zaidi ya mara moja; i.e. mihula mwili max. Ila endapo atarithi zaidi ya miaka mitatu atakuwa na haki ya kugombea mara moja tu; Samia anaangukia hapa.

Do you know why? Pungufu ya miaka mitatu itahesabiwa anamalizia kipindi cha mtangulizi wake; zaidi ya hapo ni muhula wake mwenyewe. Hivyo, kwa kuwa Samia amerithi zaidi ya miaka mitatu, kikatiba huu ni mhula wake mwenyewe; hamalizii muda uliobaki wa awamu iliyotangulia; na amebakiza mhula mmoja tu (2025 - 2030) endapo atagombea na kuchaguliwa.

"Endapo Makamu wa Rais anashika kiti cha Rais kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(5) kwa kipindi kinachopungua miaka mitatu ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara mbili, lakini kama akishika kiti cha Rais kwa muda wa miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea nafasi ya Rais mara moja tu. " Katiba ya JMT, 40(4).
 
Akimaliza kutekeleza ilani ya awamu ya tano ndio ataanza kutekeleza awamu mpya ya sita kutoka 2025 hadi 2035 kama akipata ridhaa ya chama chako na akachaguliwa na wananchi?
 
CCM NA SERIKALI JIBUNI HOJA ZA POLEPOLE, MSIMZIME KIDOLA.

Na Yericko Nyerere

Kinga uliyonayo ni kwa muda tu, hakuna kinga ya kudumu, Hata Job Ndugai na wenzake kinga walizojiwekea kipindi walipokuwa kwenye dibwi la
Kwani "awamu" maana yake nini? Nyere alifanya kwa miaka 24 lakini inahesabika awamu ya kwanza. Kumbe awau siyo miaka Bali aingiapo Rais mpya. Rais Samia ni wa awamu ya sita.
 

Mwalimu Nyerere alitawala kwa miaka 24 kwanini hatusemi rais wa awamu ya kwanza na ya pili na nusu? Mwinyi angekuwa wa awamu ya tatu na nusu.
 
Bila shaka wewe ni mvuka bahari.
 
Mambo ya marehemu Nkuruzinza wa Burundi ,alikatalia madarakani kuwa miaka 5 ya mwanzo ilikuwa ya mpito kwa hiyo haihesabiwi.
 
Unahangaika Sana Kupigania Uhai wa Mwendakuzimu urudi, haiwezekani
Yule Kwa SASA Yuko Motoni
 
Kama Samia anamalizia tu kipindi cha awamu ya tano ya Magufuli na hii sio awamu yake basi ataruhusiwa kugombea tena kwa vipindi viwili, mwaka 2025 na mwaka 2030.
Yaaa lkn akishindanishwa na wengine ndani ya chama chake. Siyo Kama mgombea pekeee.
 
Makamu wa Rais anaongoza Kama Rais au Kama Makamu wa Rais?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…