CCM ndiyo chama kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika. Nini siri yao?

Wana siri mbili. Mosi, ni mabingwa wa kuiba kura wakati wa uchaguzi na kuzuia wapinzani wao kufanya siasa kwa uhuru. Pili, Tanzania hakuna upinzani makini wala wa maana....
Pia naona CCM wamejitahidi sana kubalance suala la udini ndani yao. Utaona vyama vikubwa vyote vilivyowahi kutikisa. NCCR, CUF na CDM vinakuwa havijabalansi kidini. na ndiyo maana ACT haitafika mbali.

Tanzania dini kwenye siasa ni mwiko lakini lina nguvu sana. Chama kuwa na sura ya watu wote ni muhimu sana.
 
Iko kwenye sanduku la kura
 
🤫
 
Kwann Mchungaji Mtikila hakupa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa Wananchi.
 
Siri yao ni CHAMA TEULE kwa Tanzania iliyoteuliwa na kubarikiwa kwani Nabii Adam(A.S) aliishi Ngorongoro crater......

#SiempreJMT[emoji120]
 
NI KWEI NIMEGUGO

AFRIKA NZIMA SISIEM NDO CHAMA PEKEE AFRIKA KIMEKAA MADARAKANI TANGU ENZI NA ENZI

ILA INADHIHIRISHA KUWA WATANZANIA NDIO NCHI YENYE WAJINGA WENGI AFRIKA
Hatupendi Vita na vurugu.

CCM ni CHAMA cha umajumui wa kiafrika.
 
Iangalie Darfur.....

Mwangalie "Hemedti" Dagalo na mkuu wake wa majeshi hapo Sudan....

Iangalie Kenya na ukabila uliotopea.....

Rwanda ya mkono wa chuma....

Uganda isiyoeleweka....

Burundi yenye kujitafuta.....

Kongo wasiojitambua......

Malawi uliojikita "uzungu" usioendana na lindi la umaskini.....

Zambia iliyotapakaa WALEVI WA POMBE wanaovaa suti na kuongea kiingereza kisichoakisi maisha yao.....

Msumbiji ya mizozo ya Frelimo na RENAMO huku miongoni mwao wakijigeuza kuwa "kikundi cha kigaidi" na kutumia dini.....

Mtanzania si mjinga....

Hapana si Zwazwa.....

Nimekataa UHOBOBO kwa kuamua kuihuisha KADI YANGU YA CHAMA toka kipindi kile nikiwa Mwenyekiti wa tawi wa vijana hapo tawi la CCM Regency mkabala na kaya ya marehemu Kighoma Malima kwa ndugu katibu bwana Chacha......

Miongoni mwa fungu langu la 10 huwa ninaichangia CCM ili nipate radhi za thamani ya uhai.....wewe je?!!!!

#SiempreSSH[emoji120]

#SiempreCCM[emoji120]
 
Kwasababu ya kunyimwa kuongea kingereza na fursa ya elimu
Zambia wanaongea kiingereza kizuri...imebadilisha nini kwa wananchi wao wa kawaida?!!!

Kenya "wanabonga" haswa kuna lipi la ajabu kwa wavuja jasho wa Kibera?!!!

Uganda usiseme kwa "ya malkia"kuna lipi la ajabu hapo ?!!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Agiza Togwa nakuja kukulipia [emoji2956]
 
Agiza togwa hapo nina buku lako hapa....[emoji2956]
 
Ingekuwa ni Kenya ningetafuta sababu, ila hapa Tz watu bado wamelala, hakuna haja ya kutafuta sababu kwani inajulikana. Labda huenda na ujamaa umetuponza.
 
Ujinga na imani za kishirikina zimetamalaki katika jamii ya Watanzania.

Hata ibada za kidini zenye maudhui ya kishirikina (kimwili zaidi) zina nguvu kuliko ibada zilizojikita katika kweli na ukombozi wa roho ya mwanadamu.
 
Siri ni kwamba Tanzania hakuna Upinzani bali kuna waka asali tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…