MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,266
Kwanza naomba uelewe kuwa jaziba katika mijadala ni dalili ya kukosa hoja.Tunashukuru hatimaye umekuja kwenye mjadala licha ya sisi kukualika kwenye mijadala mingi inayohusu gharama za serikali mbili vis a vis tatu. Ni dhahiri sasa tumewakamata vibaya - mnaua chama chetu CCM kwa uroho wa madaraka, na pia muungano. Mnafanya mambo ya kijinga na kuacha ya maana. Hakuna lililo la kijinga kama hili la maboresho ya ccm. Mwalimu Nyerere coined this phrase - ya kijinga na ya maana, na sasa tunaona alikuwa ana maana gani.
Jana Jaji Warioba kaeleza vizuri sana wasaliti wa Nyerere na nani na kwa nini. Ulimsikia upo ulipo?
Sasa mjiandae na hoja yetu juu ya kwanini serikali mbili ni gharama kuliko serikali tatu. Tunaandaa uzi mahususi kabisa juu ya hilo. Tukiwaalika msikimbie.
For now juu ya gharama, jibu hoja nilizojadili kwenye bandiko la huko nyuma ambalo niliku "cc".
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Hii dhana ya kusema kwa maandiko ya jaziba na malalamiko kuwa tunakiua "chama chenu" inaonyesha kimantiki kuwa unapiga debe tupu kwa sababu kama kweli kingekuwa ni chama chako na unawafahamu watu wanaokiua basi ungekuwa tayari imechukua hatua ya kuwafukuza katika "chama chako".
Sina cha kuchangia kwa sasa zaidi ya hiki unachokisoma kwa sababu ninasubiri utuwekee hapa Rasimu Mbadala yenye serikali mbili zilizoboreshwa katika hard copy au soft copy kama ulivyotuahidi.
Siwezi kuanza kuchangia hoja ambayo bado ni hearsay au iliyojengwa kwa mtazamo wa kifikra katika utashi wa kufurahisha nafsi.
Ninasubiri pia audio ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Migiro kama ulivyoahidi kuhusu mabishano ndani ya kikao wakati akiwasilisha "Rasimu mbadala" kwenye Halmashauri Kuu ya CCM.
Majadiliano yenye hekima na busara huwa yanafanyika tu kama kuna nguzo iliyosimama ya kile kinachojadiliwa, kwa maana kuwa kama kuna hoja kamilifu.