LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wanajifanya hawahusiki,mbona hawajiulizi kwa nini wagombea wa CCM hakuna aliyekatwa?au wanamaanisha kuwa CCM ni Mungu asiyekosea?.
 
Sheria gani boss, au unadhani bado watu wako usingizini? Unataka kusema hizo hujuma za dhahiri ndio hizo sheria. Hivi huwa hambadiliki wakati watu wameshastuka nyie bado mnatumia mbinu za kizee kunajisi uchaguzi?
Sidhani kama kuna mbinu zaidi ya chadema kutafuta sababu na maigizo je wangesimama na mpango wao wa kususia uchaguzi mpaka katiba mpya unafikiri Ccm wangefanya uchaguzi bila kukaa na chadema ila ndani ya chadena kuna wenye chama ndio wanaamua na kifupi ccm itaendelea kuongoza kwa kura za chadema!
 
Hivi wale vijana wa ufipa waliokuwa wana shupaza shingo na hash tag ya "SAMIA YUKO WAPI" bado wanasikika huko mtaani kwako?
 
CCM: TAMISEMI IPUUZE MAKOSA MADOGO MADOGO, KUKUZA DEMOKRASIA .

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), kuwaelekeza wasimamizi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kupuuza makosa madogo madogo yaliyotokea, ili kuruhusu wagombea wengi kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumza na wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo vya hahari nchini, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa mfano wa makosa hayo yanayostahili kupuuzwa ni pamoja na wagombea kukosea herufi.

Kupitia mkutano huo uliofanyika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Novemba 12, 2024, Balozi Nchimbi amesema ni vyema TAMISEMI ikaangalia uwezekano wa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kutokana na makosa hayo madogo madogo ili kuhamasisha ukuaji wa demokrasia kwenye uchaguzi huo.

Aidha, kuhusu sehemu kubwa ya malalamiko mengi ya kuenguliwa kuonekana ni ya wagombea wa vyama vya upinzani, Balozi Nchimbi amewatoa shaka Watanzania kuwa, si kweli kwamba wagombea walioenguliwa ni wale wa vyama vya upinzani pekee, bali pia hata wagombea wa CCM wapo waliowekewa mapingamizi ya kugombea.

β€œWaziri wa TAMISEMI tunajua anafuata sheria, lakini ni muhimu kutambua demokrasia yetu hii bado ni changa hivyo tunahitaji muda wa kuendelea kujiΓ­funza…tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI katika nyakati za mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogo madogo ili watu wengi wapate nafasi ya kugombea", alisema Dkt. Nchimbi.

#Ends
 
Attachments

  • VID-20241112-WA0309.mp4
    21.8 MB
CCM: TAMISEMI IPUUZE MAKOSA MADOGO MADOGO, KUKUZA DEMOKRASIA

  • WhatsApp Video 2024-11-12 at 19.23.11.mp4
    21.8 MB
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 19.23.12.jpeg
    73.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 19.23.13.jpeg
    71.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 19.23.13 (1).jpeg
    90.6 KB · Views: 1
Sasa mtu anakosea herufi atawezaje kusaini nyaraka muhimu? Hao ndiyo wanatuletea wahamiaji haramu nchini .....anasain document bila kuisoma.
 
Katafuteni wajinga wa hivyo. Mtengeneze tatizo wenyewe kisha mjifanye kulitatua wenyewe? Kujitekenya na kucheka wenyewe!
 
Wote lao ni moja,hapo ni kutuhadaa tu wananchi,baba moya mama moya,.
 
CCM chama bora sana, kina usikivu na kinatatua changamoto za watu nchini.

Asante kwa kusikiliza na kutatua changamoto hii, haya hima tarehe 27 tukapige kura
 
Eti mwenyekiti wa ccm anaiomba wizara ya Tamisemi

...Tamisemi ni wizara iliyoko ndani ya Ofisi ya Raisi.

..sio wizara kamili kama Wizara ya Fedha, Mambo ya ndani, etc.

..kilichotokea ni Waziri wa Tamisemi kuiomba Tamisemi ....

..Nadhani MAKELELE yamekuwa mengi wanaona haya kuendelea na uchaguzi waliokuwa wamepanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…