LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

LGE2024 CCM: TAMISEMI itambue demokrasia yetu ni changa, ipuuze makosa madogomadogo katika hatua ya rufaa uchaguzi Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kwa mfano huo mdogo utagundua Nani alienda Shule kukariri na Nani alienda kuelimika

Hata kwenye Majina yetu Ndio sababu kuna vifupisho mfano ukiandika JK Kikwete Kila Mtu anajua ni mh Jakaya

Mh Mchengerwa tupa mapingamizi yote Tukutane na Hawa Ufipa FC Uwanja wa FISI tuwamalize

Baadae Mlale unono 😀

Ningekuwa na uwezo ningeku-block!
 
13 November 2024

Kwa urefu:

SG ambassador Dr. Emmanuel Nchimbi katibu mkuu chama dola kongwe CCM apigwa maswali mazito na waandishi wa habari kuhusu uwezo na utashi wa TAMISEMI na hisani ya rais aliye Mwenyekiti kutaka walioenguliwa warudishwe kugombea uchaguzi 2024

View: https://m.youtube.com/watch?v=psAJ6FSbM7Y

"Wapo Wanaccm waliowekewa mapingamizi, wapo wa ACT, wapo wa CHADEMA, na majibu ya mapingamizi yalitoka, lakini kwa hatua za rufaa kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Tanzania nilipofanya naye mazungumzo, ambacho tumekiona wapo wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali ambao waliwekewa mapingamizi katika hatua za awali.

Katika maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM, tumeelezana kuwa ni vizuri watu wapate nafasi, hivyo nitumie nafasi hii kutoa wito kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa, tunatambua umefuata sheria lakini ni muhimu kukumbuka kwamba demokrasia yetu bado ni changa, ni muhimu tuzidi kukua.

Tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI, katika hatua ya mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogomadogo ili Watanzania wengi zaidi wapate nafasi ya kugombea. Yapo makosa makubwa, kwa mfano nafasi ni maalumu kwa wanawake lakini amejaza mwanaume"
Kumbe mama mkwe ndio anaamua!
 
Mmekuwa kama watoto haya mmeridhishwa tafuteni sababu nyingine!
Kwamba alichosema Nchimbi ndio tumeridhika? Ccm ndio wametoa maagizo ya uchaguzi kunajisiwa nyuma ya pazia. Hivyo wangepeana maelezo huko huko nyuma ya pazia ya kufuatilia sheria. Pamoja na Nchimbi kujitokeza, bado ni mtu mjinga tu atapoteza muda wake kwenda kushiriki huo upuuzi uitwao uchaguzi kwa mazingira haya.
 
"Wapo Wanaccm waliowekewa mapingamizi, wapo wa ACT, wapo wa CHADEMA, na majibu ya mapingamizi yalitoka, lakini kwa hatua za rufaa kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambaye ni Rais wa Tanzania nilipofanya naye mazungumzo, ambacho tumekiona wapo wagombea wengi sana wa vyama mbalimbali ambao waliwekewa mapingamizi katika hatua za awali.

Katika maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM, tumeelezana kuwa ni vizuri watu wapate nafasi, hivyo nitumie nafasi hii kutoa wito kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa, tunatambua umefuata sheria lakini ni muhimu kukumbuka kwamba demokrasia yetu bado ni changa, ni muhimu tuzidi kukua.

Soma Pia:
Tunaziomba mamlaka hasa TAMISEMI, katika hatua ya mwisho za rufaa kuyapuuza makosa madogomadogo ili Watanzania wengi zaidi wapate nafasi ya kugombea. Yapo makosa makubwa, kwa mfano nafasi ni maalumu kwa wanawake lakini amejaza mwanaume"
Ushemzi, upuuzi, uwenda wazimu. Upumbavu call what may lakini yote yana istahili Ccm
 
Katiba Mpya Muhimu sana kwa ustawi wa nchi na Demokrasia.

Alafu nyie CCM si mnasema mnakubalika, sasa hizi figisu figisu za nini .
 
Kwamba alichosema Nchimbi ndio tumeridhika? Ccm ndio wametoa maagizo ya uchaguzi kunajisiwa nyuma ya pazia. Hivyo wangepeana maelezo huko huko nyuma ya pazia ya kufuatilia sheria. Pamoja na Nchimbi kujitokeza, bado ni mtu mjinga tu atapoteza muda wake kwenda kushiriki huo upuuzi uitwao uchaguzi kwa mazingira haya.
Chadema walikurupuka hawakujipanga kwa uchaguzi kuna uzi nilileta ukafutwa nilishuhudia chadema wakitafuta wagombea barabarani kisa mtu waliyepanga kumchukua bila kumtaarifu kachukua fomu Act wazalendo kwa muktadha huo chama makini kinaweza fanya hivyo lazima upate wagombea wasio na sifq sitahiki!
 
Huhitaji kujiandaa kwenye hizi chaguzi za kishenzi. Na hiki kinachoendeshwa na Tamisemi hakina mahusiano na cdm kutokujiandaa. Usidhani hatujui tatizo liko wapi. Namna pekee ya kuonyesha cdm hawakujipanga sio kuwakata kwa hila, bali ilikuwa kuwaacha washiriki ili wananchi waamue kwenye box la kura.
 
Je sheria isifuate mambo yaende kiholela!
 
Je sheria isifuate mambo yaende kiholela!
Sheria gani boss, au unadhani bado watu wako usingizini? Unataka kusema hizo hujuma za dhahiri ndio hizo sheria. Hivi huwa hambadiliki wakati watu wameshastuka nyie bado mnatumia mbinu za kizee kunajisi uchaguzi?
 
IMG_3539.jpeg
Ni Samia Tena na Demokrasia, Aagiza Wagombea Walioenguliwa kwa Makosa Madogomadogo Majina yao Yarudishwe

Na Joseph Bulebe, Dar es salaam

Rais Samia Suhuhu Hassan ameendelea kuonesha ulimwengu na watanzania kwa ujumla kuwa demokrasia ndo kitu cha msingi katika uongozi wake unaofuata utawala bora na demokrasia.

Katika hali ambayo haikutegemewa na wagombea wote waliokuwa wameenguliwa kisheria na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa makosa madogomadogo, Rais Samia ameamuagiza Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengelwa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kwa makosa madogo madogo kama kukosea mwaka wa kuzaliwa, eneo analotoka, tarehe nk.

Akiongea leo na waadishi wa Habari, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Balozi Emmanuel Nchimbi amesema Rais Samia amemugiza kumwambia waziri wa TAMISEMI wagombea wenye makosa hayo warudishwe katika kinyanganyilo cha uchaguzi ili kulinda demokrasia changa inayokuwa katika nchi yetu.

Hii sio mara ya kwanza Mh Rais anaonesha ukomavu wa demokrasia nchini katika mambo ya siasa.

Mara tu baada ya kuingia madarakani Mh Rais aliruhusu mikutano ya siasa ya wazi iliyokuwa imekatazwa na mtangulizi wake.

Hakuishia hapo Mh Rais aliunda tume ambayo pamoja na mengine ilipendekeza kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo tayari imeundwa, kuondoa pingamizi ya zuio ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ambalo nalo limeondolewa.

Mh Rais katika kuonesha demokrasia zaidi aliwaondolea kesi mbalimbali wapinzani mahakamani kama vile Mwenyekiti wa CHADEMA na makamu wake pamoja na kuwarudisha nchini wapinzani wote waliokuwa wamekimbia nchi kipindi cha awamu ya tano.

Kama hiyo haitoshi Rais amewakaribisha Ikulu Wapinzani na kuongea nao na chini ya utawala wake wapinzani wanaalikwa karibia kila tukio la kitaifa na dhifa mbalimbali za kitaifa.

Huyu ndo Rais Samia, Mwanamama wa kwanza katika nchi ya Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki anayeipeleka nchi ya Tanzania katika kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa kidemokrasia zaidi.

Kongole kwako Rais Samia kwa kulinda demokrasia nchini kwa hali na Mali sasa wagombea waliokuwa mmeenguliwa mkutane katika kampeini tarehe 20/11/2024.
 
Danganya Toto, kwenye hadhara wapatie huko uvunguni wanyime. Mungu anawaona kwa usanii wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom