Ni Samia Tena na Demokrasia, Aagiza Wagombea Walioenguliwa kwa Makosa Madogomadogo Majina yao Yarudishwe
Na Joseph Bulebe, Dar es salaam
Rais Samia Suhuhu Hassan ameendelea kuonesha ulimwengu na watanzania kwa ujumla kuwa demokrasia ndo kitu cha msingi katika uongozi wake unaofuata utawala bora na demokrasia.
Katika hali ambayo haikutegemewa na wagombea wote waliokuwa wameenguliwa kisheria na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa makosa madogomadogo, Rais Samia ameamuagiza Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengelwa kuwarudisha wagombea wote walioenguliwa kwa makosa madogo madogo kama kukosea mwaka wa kuzaliwa, eneo analotoka, tarehe nk.
Akiongea leo na waadishi wa Habari, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Balozi Emmanuel Nchimbi amesema Rais Samia amemugiza kumwambia waziri wa TAMISEMI wagombea wenye makosa hayo warudishwe katika kinyanganyilo cha uchaguzi ili kulinda demokrasia changa inayokuwa katika nchi yetu.
Hii sio mara ya kwanza Mh Rais anaonesha ukomavu wa demokrasia nchini katika mambo ya siasa.
Mara tu baada ya kuingia madarakani Mh Rais aliruhusu mikutano ya siasa ya wazi iliyokuwa imekatazwa na mtangulizi wake.
Hakuishia hapo Mh Rais aliunda tume ambayo pamoja na mengine ilipendekeza kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo tayari imeundwa, kuondoa pingamizi ya zuio ya mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ambalo nalo limeondolewa.
Mh Rais katika kuonesha demokrasia zaidi aliwaondolea kesi mbalimbali wapinzani mahakamani kama vile Mwenyekiti wa CHADEMA na makamu wake pamoja na kuwarudisha nchini wapinzani wote waliokuwa wamekimbia nchi kipindi cha awamu ya tano.
Kama hiyo haitoshi Rais amewakaribisha Ikulu Wapinzani na kuongea nao na chini ya utawala wake wapinzani wanaalikwa karibia kila tukio la kitaifa na dhifa mbalimbali za kitaifa.
Huyu ndo Rais Samia, Mwanamama wa kwanza katika nchi ya Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki anayeipeleka nchi ya Tanzania katika kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa kidemokrasia zaidi.
Kongole kwako Rais Samia kwa kulinda demokrasia nchini kwa hali na Mali sasa wagombea waliokuwa mmeenguliwa mkutane katika kampeini tarehe 20/11/2024.