Wafukuzwe tu mana hakuna namna nyingine.
Gwajima afukuzwe ili abaki kuwa Askofu kwenye kanisa lake kama walivyo akina shoo,Kilaini, Kakobe,Mwingira,.n.k.
Kuhusu Chanjo kuna mambo namuunga mkono Gwajima kuwa tusikurupuke kumchanja mtu yeyete kwa Lazima.
Hilo mama yetu Samia alilisema kuwa itakua ni hiyari. Ni kweli kuwa madaktari wanaodili na magonjwa kama hayo wanapenda fursa za kujipatia fedha kwa kuzunguka nchi nzima kuchanja watu bila kujali hatima ya watu zaidi ya kupata fedha za night allowance. Hata hivyo Gwajima hakupaswa kulizungumzia nje ya vikao halali au kwenda kumshauri Rais ikulu. Wakati wa Msukuma mwenzake aliufyata mkia hata alipoona nyumba za ibada zinageuka na kuwa matawi ya CCM kwa lazima ili zisifugwe. Leo anataka kurudisha ile tabia yake ya kuwatukana marais waislam wakati makanisa yote yamejengwa vizuri na kuwa na waumini wenye maisha mazuri wakati wa utawala wa Marais waislam.
Wakati wa Nyerere alizuia makanisa ya Kilokole na walionekana kuwa wanakashfu dini nyingine. Vurugu zilikua ni kubwa sana kwenye kupigania haki ya makanisa ya kilokole na walokole walikamtwa kamatwa hovyo. Mwinyi akaje akasema ruksa mtu kuanzisha dini yake.
Mkapa akaja makanisa hayo ya kilokole yakawa na waumini maskini wasio na uwezo wa kumnunulia mchungaji hata baskeli.Akaja Mtu wa Watu JK makanisa yote yakawa na waumini wenye uwezo wa kujenga makanisa yao. Mengine yakajenga mpaka mabenki, Wakina Gwajima wakawa na Mabodigadi na kununua Helkopta n.k. Wakaanza kujiinua na kumkashifu kwa sababu tu alitoa Uhuru . Wakatumia mitandao kumtukana mpaka Pengo.
Akaja Mwendazake ,watu wakapotea ,wakatekwa,wizi wa kura, watu kupigwa na kuporwa fomu za kugombea, maDC kupiga watu n.k lakini akina Gwajima wakaanza kusifu na kutukuza dhulma kwa sababu za Ukabila na udini.
Sasa wameanza Tena. Hawa akina Gwajima ndio wanaoleta chokochoko zinazolipotosha umma na sio wale wa Katiba inayoliunganisha Taifa.
Hakutakiwa amdhalilishe Rais kwa kumsema hadharani. Alipaswa kwenda ikulu na kumshauri kwani ana hoja nzuri.
Lakini pia suala la afya na imani haliwezi kuwa la wote. Imani ni kwa wanaoamini kweli . Wasioamini wanatibiwa kisayansi.
Kuna mtu hata angechanjwa na maji tu angepona mana anaamini kila ugonjwa akishamuona daktari anapona . Ndio maana biashara ya dawa za makemikali bado IPO juu sana mana watu wanaamini na kuzitumia japo zinatoka huko huko nje kwa wazungu.
Mwenye imani asilazimishwe kuchanjwa lakini mzinzi,mlevi,muuaji kama wanaCCM wengi, washirikina kama wanaCCM wengi, wachawi, wezi kama wanaCCM wengi, mafisadi kama wanaCCM wengi,waongo,waabudu sanamu, wanaobambikia watu kesi n.k. Hawa inabidi Wahubiriwe toba kwanza sio kuishambulia serikali na wapinzani kwa kudhani kuwa wataikimbia hukumu inayokuja.
NB
Haki,Upendo,utu na usawa ni jambo jema hata mtu akifa najufa kwa amani .
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app