CCM: Tunafuatilia mienendo ya viongozi wetu wanaopotosha umma, kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wetu

Leo ndo mmejua kuna Uhuru wa maoni? Mmeanza lini kuhubiri Uhuru wa maoni tofauti na Mwenyekiti wenu? Mbona wengine wakileta maoni tofauti wanapewa kesi za uhaini?
 
Tundu njoo umchukue huyu shoga mwezio kwenye hii picha
 
Kwani wewe kwa akili zako unadhani samia atagombea 2025 labda alazimishwe tu mama ni mchovu yeye mwenyewe anajijua wala hakuwa na wazo la kuwa makamu wa raisi ,lakini cheo cha makamu raisi alikifurahua kwa sababu ni chakula bata tu siyo cheo cha uraisi ,kitu pekee kwa mama ni kumuandaa majaliwa kuwa raisi 2025 hapo atakuwa kaitendea haki tz
 
wachukuliwe hatua kali za utovu wa nidhamu.
awamu ya 5 walikuwa na nidhamu ya hali ya juu sasa wanaonekana wamekosa kabisa nidhamu yaani kila mmoja kaota mapembe!!
yaani hawajali kabisaaaa wanajilopokea tu!!!
nadhani wana lengo lililo jificha.
 
wachukuliwe hatua kali za utovu wa nidhamu.
awamu ya 5 walikuwa na nidhamu ya hali ya juu sasa wanaonekana wamekosa kabisa nidhamu yaani kila mmoja kaota mapembe!!
yaani hawajali kabisaaaa wanajilopokea tu!!!
nadhani wana lengo lililo jificha.
 
Huyu si ndo yule jamaa alikulaga kondoo ...hivi kumbe alipata nafasi ya kuingia mjengoni[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani ujui mjengoni ndiko wanapatikana manguli wenye sifa mbovumbovu top,majangiri ,wauza unga, mabasha, wasagaji ,mafisadi papa , makahaba,nk sifa kuu ya kuwa mjengoni ni kuwa top kwenye mambo mabovu,
 
Wafukuzwe tu mana hakuna namna nyingine.

Gwajima afukuzwe ili abaki kuwa Askofu kwenye kanisa lake kama walivyo akina shoo,Kilaini, Kakobe,Mwingira,.n.k.

Kuhusu Chanjo kuna mambo namuunga mkono Gwajima kuwa tusikurupuke kumchanja mtu yeyete kwa Lazima.
Hilo mama yetu Samia alilisema kuwa itakua ni hiyari. Ni kweli kuwa madaktari wanaodili na magonjwa kama hayo wanapenda fursa za kujipatia fedha kwa kuzunguka nchi nzima kuchanja watu bila kujali hatima ya watu zaidi ya kupata fedha za night allowance.

Hata hivyo Gwajima hakupaswa kulizungumzia nje ya vikao halali au kwenda kumshauri Rais ikulu. Wakati wa Msukuma mwenzake aliufyata mkia hata alipoona nyumba za ibada zinageuka na kuwa matawi ya CCM kwa lazima ili zisifugwe. Leo anataka kurudisha ile tabia yake ya kuwatukana marais waislam wakati makanisa yote yamejengwa vizuri na kuwa na waumini wenye maisha mazuri wakati wa utawala wa Marais waislam.

Wakati wa Nyerere alizuia makanisa ya Kilokole na walionekana kuwa wanakashfu dini nyingine. Vurugu zilikua ni kubwa sana kwenye kupigania haki ya makanisa ya kilokole na walokole walikamtwa kamatwa hovyo. Mwinyi akaje akasema ruksa mtu kuanzisha dini yake.

Mkapa akaja makanisa hayo ya kilokole yakawa na waumini maskini wasio na uwezo wa kumnunulia mchungaji hata baskeli.Akaja Mtu wa Watu JK makanisa yote yakawa na waumini wenye uwezo wa kujenga makanisa yao.

Mengine yakajenga mpaka mabenki, Wakina Gwajima wakawa na Mabodigadi na kununua Helkopta n.k. Wakaanza kujiinua na kumkashifu kwa sababu tu alitoa Uhuru . Wakatumia mitandao kumtukana mpaka Pengo.

Akaja Mwendazake ,watu wakapotea ,wakatekwa,wizi wa kura, watu kupigwa na kuporwa fomu za kugombea, maDC kupiga watu n.k lakini akina Gwajima wakaanza kusifu na kutukuza dhulma kwa sababu za Ukabila na udini.

Sasa wameanza Tena. Hawa akina Gwajima ndio wanaoleta chokochoko zinazolipotosha umma na sio wale wa Katiba inayoliunganisha Taifa.

Hakutakiwa amdhalilishe Rais kwa kumsema hadharani. Alipaswa kwenda ikulu na kumshauri kwani ana hoja nzuri.

Lakini pia suala la afya na imani haliwezi kuwa la wote. Imani ni kwa wanaoamini kweli . Wasioamini wanatibiwa kisayansi.
Kuna mtu hata angechanjwa na maji tu angepona mana anaamini kila ugonjwa akishamuona daktari anapona . Ndio maana biashara ya dawa za makemikali bado IPO juu sana mana watu wanaamini na kuzitumia japo zinatoka huko huko nje kwa wazungu.

Mwenye imani asilazimishwe kuchanjwa lakini mzinzi,mlevi,muuaji kama wanaCCM wengi, washirikina kama wanaCCM wengi, wachawi, wezi kama wanaCCM wengi, mafisadi kama wanaCCM wengi,waongo,waabudu sanamu, wanaobambikia watu kesi n.k. Hawa inabidi Wahubiriwe toba kwanza sio kuishambulia serikali na wapinzani kwa kudhani kuwa wataikimbia hukumu inayokuja.

NB
Haki,Upendo,utu na usawa ni jambo jema hata mtu akifa najufa kwa amani .
 
Kwani hukumsikia mother geto alipo sema raisi hakosei ,tz tumelamba garasa kwa huyo raisi,
Si nyerere wala magufuli alisha wahi kuongea utopolo wa namna hii
 
Acha kuingiza hoja dhaifu ya udini na ukabila wewe! Gwajima hajaongelea dini ya mtu wala kabila la mtu! Hoja yake ni kukataa chanjo kwa lazima na wewe unapswa ujikite kujibu hoja hii! Gwajima hajapingana na Rais kwa sababu wanatofautiana dini wa la kabila.
 
Kwenye nchi unatakiwa uwe na watu manunda wawili Tu ama watatu kama Gwajima , hatuwez kuwa wote makondoo nyanya alaaah
 
Hakuna wa kumfukuza Sukuma gang hiyo
 
Gwajima anapaswa atoke hadharani awaombe Radhi watanzania. vinginevyo atawajibika kwa kauli zake za upotoshaji wakati Taifa lipo ktk mapambano ya janga hili la korona.
 
Umeupiga mwingi sana, hongera sana.
 
Ule uchaguzi mlianguka ipo wazi..... Tatizo ni mfumo wa uchaguzi tu. Kma ni kutumia dola tu, hta angekua Mrema mbona angeshinda kila chaguzi anavyotaka.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…