Tetesi: CCM wanapita vyuoni kuorodhesha UVCCM waliokosa mkopo

Mwisho wa siku mtasema kwamba CCM imetoea maagizo kuhakikisha wanafunzi wote walio wanachama wa CCM hawatakiwi kupata supp..
Hahahaa sasa watoke vipi...maana agenda ya ufisadi waliizika siku nyingi...
 
Hili timu lumumba hawaligusi
Maana limejaa uhalisia wa kiongozi wa nchi alivyo


"Siwezi kuwapa watoto wa jirani chakula mpaka wangu washibe kwanza" ubaguzi wa wazi wazi ndani jamii inayojiita wamoja
 

uhalali wa hii serikali ya awamu ya tano unatia mashaka. Sina hakika kama CCM walishinda kwa kura halali mwaka 2015
 
Ukawa nunueni tu hizo kadi halafu mkiwa ndani ya uvccm ndiyo tutaimaliza vizuri ccm kwa kutengeneza migogoro isiyoisha
What is UKAWA? It not legally existent neither valid! Stop using that bad name!!
 
huyu je?
msikie huyu
jibu utapata. But kwenye bodi ya mikopo who is UVCCM?
 
Hakuna uhusiano katika kupata Mkopo na itikadi za kisiasa, Mkopo ni haki ya mhitaji anayestahili kulingana na vigezo.
 
Hakuna uhusiano katika kupata Mkopo na itikadi za kisiasa, Mkopo ni haki ya mhitaji anayestahili kulingana na vigezo.
well said mkuu, lakini uhalisia hauko hivyo, UVCCM ndo anaamua mustakabali wa mikopo by now.
 

Ebu taja jambo moja ccm waliwahi kukubali hata kama wangeshikwa red handed just one. Epa, Kagoda, Escrow, Meremeta, Buzwagi Safari za viongozi nje ya nchi n.k wewe kukataa kwamba siyo kweli na wewe unao ushahidi?
 
Wawaajiri kwanza UVCCM wanaosota mtaani tangu mwaka jana kwa kukosa ajira
 
Haiwezekani. Ni uongo mkubwa. Mimi niko ccm lakini sikupataga udhamimi enzi za Sumaye akiwa waziri mkuu.

Wakati huo utawala ulikuwa unaheshimu haki na sheria.

Sio utawala huu wa kibabaishaji.

Ngoja nami niende nikanunue kadi ya hili lichama naweza kupata mkopo, ili niweze kusoma degree yangu ya sociology.
 
Ccm Itashindwa Acha Ijichanganye Watu Wana Hasira Sana
 
Siamini uzi huu kama ni wa kweli.
Ni serikali gani ulimwenguni ambayo yaweza kuwabagua wananchi (wanafunzi) wake katika misingi ya vyama?Unapoenda Hospitali na kumkuta bwana mganga ama Daktari hakuulizi wewe ni wa chama gani kabla hajakutibu?
Huwa anatibu watu WOTE na wa vyama vyote.Maana alisomeshwa na SERKALI si CHAMA!
Labda ni Korea Kaskazini peke yake kuliko na ujinga huo!
Maana hili laweza kuwagawa watanzania VIBAYA SANA!
Siaamini kuwa Rais Magufuli anaweza kuinama (THAT LOW) yaani chini kiasi hicho na ATOE AGIZO ABAGUE na kusema wanafunzi wasio wana CCM WASIPATE mikopo.
Hapo sikubali!
Maana atakuwa amepoteza dira kabisa!
Ndiyo maana siamini.
Na kama wanafanya hivyo labda basi ni BEHIND his BACK yaani nyuma ya MGONGO wake ili kumpaka matope na kumchonganisha kati ya serikali yake na wananchi.
Huko ni kufikiria kwangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…