CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Si huyo aliyefukuzwa?

Aliyeitwa ahojiwe baada ya mahojiano akatangaza kawaweka walimhoji mfukoni kwa maana ya kuwa amewatosha?

Au membe yupi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kifupi BM kwishney ! CCM ni taasisi kubwa sana kuweza kutingishwa ba mtu mmoja na kakikundi kake, eti sijui nani, eti ninihii mbobezi ! Ngoja aone hao nanii wabobezi watakavyo lalanae sambamba ! EL aliyepata kura milioni sita 2015 mwenyewe ali surrender 🙌 itakua kidagaa huyu !
 
Tujifunze kwa lowasa, sumaye, na wengine wa Aina hiyo.sio rahisi kutolewa nje ya mfumo wa maisha uliouzoea na ukaendelea kuishi kwa amani ndo maana wengi huwa wanageuka wahaini kutokana na hasira ila Mambo yakikataa kabisa huomba kurudi kwa huruma.

CCM Kama chama kikubwa chenye wanachama wengi na kinachofuata kanuni na taratibu katika uendehaji wa shughuli zake wanatokea wanachama wenye viburi, dharau na kujiona wao ni wakubwa ndani ya chama. Ni suala la muda tu tutaambiwa alipeleka barua Kama Saba za kuomba msamaha Kule lumumba ama atastaafu siasa.

NARUDIA TENA USIGOMBANE NA BABA YAKO..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM ni taasisi ambayo haiyumbishwi na mtu au watu,kuwepo/kutokuwepo kwa membe and his colleagues hakukifanyi chama kuyumba,membe and the alike ni kama jani kwenye nyumbani,je likindondoka nyumba itavuja?,CCM ina mifumo imara sio kama CHADEMA ambayo inamuabudu only one person

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM imebaki jina tu mnachofanya ni kununua wenye akili timamu toka CDM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichoandika mwenye Uzi ndicho ninachoamini. Ataomba msamaha atapewa muda Wa matazamio kisha atarudishwa
 
kwan TISS ni mali ya ccm, hadi asigombee urais kupitia chama kingine au kupitia hiyo hiyo ccm?
kwani ukiwa TISS huruhusiwi kuwa rais?
"kwa uelewa wangu mimi TISS hakuna kustaafu mpaka ufariki"
 
Akiomba msamaha wakati amekubali kushindwa ningekuwa mimi ni kachero mbobezi ningeondoka na nyama niwe kipande B.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu chukulia mfano wa samaki.

Unamtoa kwenye maji mengi unamuweka kwenye maji kidogo aishi humo unafikiri ataishije?

Ndo anachoenda kuishi BKM, na wote wanaoliwa vichwa au wanaojiondoa ndani ya ccm.

Kukutoa kwa nguvu ndani ya mfumo uliokulea, ukauishi maisha yako yote, ukauzoea Sana Ni sawa na kukukaba shingo ili ukose pumzi hapo kuna mawili matatu. Upambane kujinasua, ukubali kufa, ama umuombe msamaha aliyekukaba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom