CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hahahaaa!
Watoto warembo kama hawa wanapatikana CCM tu!
JamiiForums-1839830178.jpg
 
Hii namba 4 na 7 unatoa wapi? Kwanini nyie watu mnapenda kuongopa na kupanikisha watu? Hivi hata kama viongozi wetu wawe mbumbumbu, ndio wakodishe Bandari kwa faida sifuri?
Wewe unaongea nini? Hujui kama tumekopa trillion zaidi ya 1 World Bank? Na hiyo pesa imeshafanya kike kinachodaiwa kitafanywa na DP World, sasa kama sio uwendawazimu huo ni nini?

Pia hawa waty wameridhiana kupewna misamaha ya kodi kwa mapato wanayoingiza wao, sasa si ukausome mkataba..?!
 
Ambacho hawashtuki hii CCM iliyokaa hapo, ipo tofauti kabisa na CCM iliyopo nje, yaani kuna malalamiko makubwa sana kiufupi wanajitafuna wenyewe, wakija kushtuka itakuwa too late sana
Hakuna malalamiko yeyote huku nje sisi tupo tunaendelea na maisha yetu nyie ndio mnayakuza.
 
...
Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake. ...
Jibu hilo linatosha kuibua hisia kuwa kikao hicho kilikuwa cha upande mmoja wa kuwaburuza Wajumbe wa Halmashauri Kuu kukubali yaliyofikishwa kwenye Kikao hicho.

Kama uamuzi huo, wa Halmashauri Kuu ya CCM, kuwa IGA haina dosari na Serikali ichukue hatua ya kuelimisha umma, CCM isubiri matokeo ya uelewa wa Wananchi, wapiga kura, kwani 2024 na 2025 ni kesho tu.
 
Piga Ua.
IGA yenyewe imedai makubaliano hayo yawe yameridhiwa na vyombo vya juu vya nchi vinavyotoa ridhaa za uwekezaji Nchini...ikiwepo Bunge. Vilevile na Chama kilicho na hatamu...

Bunge letu lina Wabunge wa CCM na ni dhahiri wakati wanapitia yale walikuwa hawana Taarifa kamili, yaani vielelezo vya kutosha! Ikiwa ina maana Chama hakikukaa kama chama kujadili, kuchatua, kumega kukataa au kukubali mkataba huo na kuzua sintofahamu kwa baadhi ya walipopelekewa (nyaraka) ad-hoc Wabunge bungeni....ati leo hii ndio wamefanya hivyo? After the Fact? Halafu waseme iko sambamba na 59-92 ya Ilani ya Chama....Who cares


Suala hili limewashindwa CCM(wenzangu). Na tulipofikia ni kukaa pembeni kutafakari na kujitathmini. Na wakati tunafanya hivyo...Kiongozi yeyote yule anayeweza kuongoza Nchi wa Chama chechote kile cha siasa apigiwe Kura ya Ndio tuondoke madarakani kwani ni dhahiri tumeshindwa.
Haiwezekani chama tawala kikawa na lengo baya kwa nchi nzima. Huwezi kujenga SGR kwa trilioni 14 halafu uikoseshe mzigo kwa hoja nyepesi za kipuuzi za kina Mwabukusi.
 
Wakiona maswali kama haya wanatafuta chaka la kujificha na kubadili mada 😂😂
Yani hawa ni kubadili njia za kuwahoji yayale wanayoyasema maana hawa ni wahuni wajinga wenye interest za kidini na Upwani hakuna lingine zaidi ya hilo.
 
Back
Top Bottom