Cctv video: Kuweni makini mnapokuwa mnarudi majumbani usiku, Anusurika kuvamiwa na majambazi Getini

Cctv video: Kuweni makini mnapokuwa mnarudi majumbani usiku, Anusurika kuvamiwa na majambazi Getini

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Hii imetokea 10/08/2025, Goba madale karibu na Joy Eslava , mdada alikua anasubiri kufunguliwa geti alisahau remote ndani. Wakati anasubiri, hao jamaa wa boda wakamvamia. aliweza kuwakimbia ila kaumia mkono walimkata na kisu, pia kaumia jicho, vioo viliingia kwenye jicho moja. Asubuhi amesema kuna jirani yake pia amekutwa na tukio linalofanana usiku wa jana yake.



Bodaboda anakatiza pembeni ya gari, kwa mwendo wa kawaida tu hana haraka, hana hofu. Wewe ndani ya gari, unamtazama kwa jicho la haraka unahisi ni mtu wa kawaida, labda anarudi zake nyumbani.

Lakini kumbe ulikuwa umelaghaiwa. Mwenzake aliruka kininja nyuma ya gari, amejibanza kimya, hujatambua uwepo wake,

muda huo unamuoangalia bodaboda au unatumia simu kusubiri geti lifunguliwe, Ghafla – PUU !💥 Jiwe kubwa linatua kwenye kioo kwa kishindo, Kabla hata hujatambua kilichotokea, mkono unapenya dirishani, kisu mkononi.

Hili si tukio la kawaida, ni mtego uliosukwa kisaikolojia, na hata mazoezi ya kurukia angle flani nyuma ya gari ambazo sio rahisi dereva kuona (blind spot)
 
kama ni me, ni uzembe wake hapo, upo ndani ya gari alafu mtu aje na jiwe. Wanaume tusisahau kuwa hata na panga popote. Mimi usiku unikosi na sime kiunoni. Jichanganye labla uje na bastola.

Jiwe lilikuwa kwa ajili ya kupasua kioo, na limerushwa kwa kushtukiza tu.

Yawezekana hao wezi wana mapanga na hata bunduki pia
 
kama ni me, ni uzembe wake hapo, upo ndani ya gari alafu mtu aje na jiwe. Wanaume tusisahau kuwa hata na panga popote. Mimi usiku unikosi na sime kiunoni. Jichanganye labla uje na bastola.
unachekesha sana mkuu
umeangalia video vinzuri umeona huyo jamaa alivyojibanza na kushtukizia

halafu pia haya matukio hayajazoeleka so hata kama alimuona alivyoshushwa alifikili tu ni kama boda kamshusha abiria

ila huyo alikuwa ni mwanamke wanavyosema imesambaa sana kwenye group za whtasaap
 
unachekesha sana mkuu
uneangalia video vinzuri umeona huyo jamaa alivyojibanza na kishtukizia
halafu pia haya matukio hayajazoeleka so hata alimuona alivyoshushwa alifikili tu ni kama boda kamshusha abairia

ila huyo alikuwa ni mwanamke wanavyosema imesambaa sana kwenye group za whtasaap
Hivi hao watu kwa kuangalia kujulikana ni ngumu kabisa et
 
Tunaonaga kwenye muvi wale fbi wanvyosema "stop enhance"
Haya kisimu changu cha tekno kimeishia hapa, wataalamu waichakachue hii number plate tuwakamate....

1754951783096.png
 
Tunaonaga kwenye muvi wale fbi wanvyosema "stop enhance"
Haya kisimu changu cha tekno kimeishia hapa, wataalamu waichakachue hii number plate tuwakamate....

View attachment 3438751
Kwenye cctv huwa kuna option ya Kuzoom, kama namba zitaonekana au kusafisha picha ionekane vizuri itasaidia kuwatabua hata nyuso zao.
 
Unapokuwa kwenye situation kama hii usiogope kuharibu gari kwa kufikiria thamani yake, Tumia gari kama silaha, Piga reverse, piga kona, moja wao akiwa kwenye usawa wako kanyagia kibati.
Kashindwa kumvunja miguu huyo boda hapo. Sema amekuta ni mwanamke. Mi ningemvunja miguu huyo boda au jamaa aliyekuja kuvunja dirisha.
 
Back
Top Bottom