Cctv video: Kuweni makini mnapokuwa mnarudi majumbani usiku, Anusurika kuvamiwa na majambazi Getini

Cctv video: Kuweni makini mnapokuwa mnarudi majumbani usiku, Anusurika kuvamiwa na majambazi Getini

Niwe na gari nikabwe na boda boda aisee watu wapo chini ningewagonga ukutani kama nasaga sisimizi nyambafu..
Alikuwa n nafasi nzuri sana hasa kwa huyo anayeendesha piki piki, labda aliingiwa na woga wa kuua. Ila aisee huyo jamaa akiiangalia hii clip aache wizi tu.
 
Hii imetokea 10/08/2025, Goba madale karibu na Joy Eslava , mdada alikua anasubiri kufunguliwa geti alisahau remote ndani. Wakati anasubiri, hao jamaa wa boda wakamvamia. aliweza kuwakimbia ila kaumia mkono walimkata na kisu, pia kaumia jicho, vioo viliingia kwenye jicho moja. Asubuhi amesema kuna jirani yake pia amekutwa na tukio linalofanana usiku wa jana yake.

View attachment 3438708

Bodaboda anakatiza pembeni ya gari, kwa mwendo wa kawaida tu hana haraka, hana hofu. Wewe ndani ya gari, unamtazama kwa jicho la haraka unahisi ni mtu wa kawaida, labda anarudi zake nyumbani.

Lakini kumbe ulikuwa umelaghaiwa. Mwenzake aliruka kininja nyuma ya gari, amejibanza kimya, hujatambua uwepo wake,

muda huo unamuoangalia bodaboda au unatumia simu kusubiri geti lifunguliwe, Ghafla – PUU !💥 Jiwe kubwa linatua kwenye kioo kwa kishindo, Kabla hata hujatambua kilichotokea, mkono unapenya dirishani, kisu mkononi.

Hili si tukio la kawaida, ni mtego uliosukwa kisaikolojia, na hata mazoezi ya kurukia angle flani nyuma ya gari ambazo sio rahisi dereva kuona (blind spot)
Aliyevunja kioo ametumwa kulipa kisas sijui ni cha nini
 
Big up Kwa Mda. Amepambana sana
 
Inasemekana wamemjeruhi mkono kwa kisu na vipande vya kioo viliingia kwenye jicho moja.
Mungu wangu😢😢 wezi siyo watu wazuri kabisa, dah! Hawa wakikamatwa siyo wa kuonea huruma kabisa, hata hivyo alikuwa jasiri sana
 
Hivi hakuna teknolojia ya ku zoom mpaka kubaini Muhusika.

Ukiwapata wanawekwa Chemba mahali kwanza ulifikiria cha kuwafanya wewe Mwenyewe maana Polisi mlolongo sana.Utakachowafanya unahakikisha kama ni mauti basi wao ndio watafikia hatua kukuomba kwamba "imetosha tuue tu".
Unafatilia muvi sana mjomba
 
Iko hivyo kwenye story vijiweni info zinzauzwa chap.
“ oya gari la mshkaji gani lile?”
“Ni demu mbona ananitumaga kumfanyia shopping pia”
“Mwanawe atakuwa yuko vizuri”
“Hamna mzee yule yuko single”
“Ndiyo anaishi kwenye ule mjengo pekee yake , duh!!!”
“Ndiyo hivyo, pale ndani kuna nyumba mbili ila si unakumbuka wale wa kina fred walihama na mpangaji hajapatikana bado, kwa hiyo kiufupi pako wazi, mtoto yuko mwenyewe kwenye ule mcompound”
“Dah noma mzee”
“Ha ha ha, nakubali”
Info nyingi za matukio kama haya zinauzwa na wale BODA WANGU this boda wangu that namtuma mpaka kwangu nampa funguo za nyumba anipelekee burger🚮 wake up
 
Kwanza dada apewe maua yake kwa jinsi alivyokuwa na ujasiri wa ajabu na kuweza kuingiza gari ndani na kutoka vizuri bila kuogopa. Ingekuwa hatari sana kwake iwapo alipoingia ndani halafu angetoka nje ya gari ili akimbilie ndani ya nyumba ule uamuzi aliofanya ndio pona yake. Ingekuwa dada mwingine au hata baadhi ya wanaume miguu ingetetemeka gari ingezima na si ajabu hata haja ndogo ingetoka palepale. Hapa mtandaoni watu wote tunajifanya mashujaa kwa sababu tunaanglia VAR ya hilo tukio ila tungekuwa "live" wengi wetu tungekuwa vituko tofauti kabisa na tunachoandika sasa hivi.

Wapo wanaosema kuwa huyo dada angembamiza yule dereva wa boda boda. Ni kweli ilikuwa inawezekana lakini kumbukeni kuwa tukio kama lile huwa linatokea kwa haraka sana bila kutegemea na katika hali kama hiyo kitu cha kwanza kinachokuja kichwani huwa ni kujiokoa kwanza. Ni wachache sana wakiwa katika mapambano kama yale kuweza kupata akili ya haraka ya kujiokoa na wakati huo kuwadhuru hao wavamizi.

Kwa kuongezea tu ikitokea upo kati hali kama ile ukiweza na narudia tena ukiweza kupiga honi "non stop" ni nzuri kwasaba kuu mbili. Moja unawaamsha majirani kwasababu wanajua kabisa kuna tukio lisilo kawaida limetokea na mbili unawachanganya wavamizi kwa sababu wanajua kabisa watu wataamka na wao watashindwa kuondoka sehemu ya tukio kwa urahisi.

Ni mtizamo tu.
 
Kashindwa kumvunja miguu huyo boda hapo. Sema amekuta ni mwanamke. Mi ningemvunja miguu huyo boda au jamaa aliyekuja kuvunja dirisha.
Angemgonga angekwama huyo wa pili angemzibiti kirahisi sana
 
Hivi hakuna teknolojia ya ku zoom mpaka kubaini Muhusika.

Ukiwapata wanawekwa Chemba mahali kwanza ulifikiria cha kuwafanya wewe Mwenyewe maana Polisi mlolongo sana.Utakachowafanya unahakikisha kama ni mauti basi wao ndio watafikia hatua kukuomba kwamba "imetosha tuue tu".
Kuwafira iwe ndio cha kwanza wakati ukitafakari uwapeleke polisi ama mtoni
 
Back
Top Bottom