Cctv video: Kuweni makini mnapokuwa mnarudi majumbani usiku, Anusurika kuvamiwa na majambazi Getini

Cctv video: Kuweni makini mnapokuwa mnarudi majumbani usiku, Anusurika kuvamiwa na majambazi Getini

Hii imetokea 10/08/2025, Goba madale karibu na Joy Eslava , mdada alikua anasubiri kufunguliwa geti alisahau remote ndani. Wakati anasubiri, hao jamaa wa boda wakamvamia. aliweza kuwakimbia ila kaumia mkono walimkata na kisu, pia kaumia jicho, vioo viliingia kwenye jicho moja. Asubuhi amesema kuna jirani yake pia amekutwa na tukio linalofanana usiku wa jana yake.

View attachment 3438708

Bodaboda anakatiza pembeni ya gari, kwa mwendo wa kawaida tu hana haraka, hana hofu. Wewe ndani ya gari, unamtazama kwa jicho la haraka unahisi ni mtu wa kawaida, labda anarudi zake nyumbani.

Lakini kumbe ulikuwa umelaghaiwa. Mwenzake aliruka kininja nyuma ya gari, amejibanza kimya, hujatambua uwepo wake,

muda huo unamuoangalia bodaboda au unatumia simu kusubiri geti lifunguliwe, Ghafla – PUU !💥 Jiwe kubwa linatua kwenye kioo kwa kishindo, Kabla hata hujatambua kilichotokea, mkono unapenya dirishani, kisu mkononi.

Hili si tukio la kawaida, ni mtego uliosukwa kisaikolojia, na hata mazoezi ya kurukia angle flani nyuma ya gari ambazo sio rahisi dereva kuona (blind spot)
Dah angekanyaga vizuri aue uyo
 
Inamaana hiyo nyumba haina watu kiasi cha kutoka baada ya purukushani zote hizo mpaka geti linavunjwa?.

Ukichagua kukaa mwenyewe hivyo ni vyema pia uwe full nondo zinapotokea shida kama hizi unazimaliza tu kimwamba.
hapo angekuwa shujaa kidogo tu tungeokota maiti mbili.

ndani ya mitaa ya Kabul Afghanistan
 
Goba kuna uhalifu wa kipuuzi sana. Ila askari watawajua wahusika maana huwa ni rahisi sana kuwakamata kupitia connection zao. Mhalifu huwa hatokei mbali na hata akitoka mbali anakuwa na panya wake wa kumpa taarifa hapo kwenye mtaa au kitongoji. Upelelezi wa sura mpya ufanyike.

Mtaani kwetu ninapoishi kulikuwa na matukio ya wizi. Nilitengeneza group ya Whatsapp nikaweka watu wachache ninao waamini tukaunda kamati ya Siri ya ulinzi kujadili scenario. Nikagundua wenzangu kumbe nao matukio ya kukurupusha wezi usiku wa manane au kuanuliwa nguo yamewakuta na wameshapatwa na hali ya sintofahamu kuhusu hali ya usalama wa mitaa yetu.

Basi tukaweka maazimio. Mojawapo ilikuwa ni kuwatazama kwa macho yote vijana wasiokuwa na ramani za maisha wapo wapo tu mtaani wakileta washikaji zao kutoka mbali kuweka vijiwe vya uvutaji bangi na gogovivu.

Tulianza kusimamisha pikipiki kuna siku nakumbuka jirani yangu alinipigia simu kuwa kuna zogo nje. Tukakutana na vijana watatu kwenye pikipiki moja, jirani kawasimamisha kuwahoji wanatoka wapi wakamjibu kuwa yeye kama nani kuwauliza hivyo, kwa bahati nzuri alikuwa ametoka na jirani wengine wanaoishi sehemu moja.

So ndani ya dakika tano wale vijana walikuwa chini ya ulinzi mkali pikipiki yao umewekwa kando. Muda mimi natoka kufika nikakuta kibao kimewageukia.

Aisee walikula makofi wakawa wanaomba msamaha kwa kupiga magoti na kulia kama watoto.

Tukawaambia kama hauishi mtaa husika unafanya nini saa zimeenda kwenye makazi ya watu?

Hawakuwa na majibu, aisee walikula kichapo cha adabu wakaondoka wanatia huruma. Sasa kuna majina yalitajwa pale. Wale vijana walifuatwa makwao. Wakiulizwa kwann wanaalika marafiki zao wa hovyo hapo mtaani wana ratiba gani? Umri wa kuwa kazini wao wanashinda vijiweni.

Biti lilikuwa kali sana. Hapa ninavyoongea mitaa yetu hii vijiwe hakuna hata sehemu moja,ikifika saa tano ukisikia pikipiki ni inamshusha mwenyeji na kusepa. Huwezi kuta mtu kasimama au ana randaranda na si mwenyeji.
 
Hii imetokea 10/08/2025, Goba madale karibu na Joy Eslava , mdada alikua anasubiri kufunguliwa geti alisahau remote ndani. Wakati anasubiri, hao jamaa wa boda wakamvamia. aliweza kuwakimbia ila kaumia mkono walimkata na kisu, pia kaumia jicho, vioo viliingia kwenye jicho moja. Asubuhi amesema kuna jirani yake pia amekutwa na tukio linalofanana usiku wa jana yake.

View attachment 3438708

Bodaboda anakatiza pembeni ya gari, kwa mwendo wa kawaida tu hana haraka, hana hofu. Wewe ndani ya gari, unamtazama kwa jicho la haraka unahisi ni mtu wa kawaida, labda anarudi zake nyumbani.

Lakini kumbe ulikuwa umelaghaiwa. Mwenzake aliruka kininja nyuma ya gari, amejibanza kimya, hujatambua uwepo wake,

muda huo unamuoangalia bodaboda au unatumia simu kusubiri geti lifunguliwe, Ghafla – PUU !💥 Jiwe kubwa linatua kwenye kioo kwa kishindo, Kabla hata hujatambua kilichotokea, mkono unapenya dirishani, kisu mkononi.

Hili si tukio la kawaida, ni mtego uliosukwa kisaikolojia, na hata mazoezi ya kurukia angle flani nyuma ya gari ambazo sio rahisi dereva kuona (blind spot)
Huyu dada alikuwa jasiri na ashukuriwe Mungu akafanikiwa kukimbia.

Hawa majambazi wakikamatwa ni kuwatwanga shaba tu wafe.
 
Mwee mimi ningewakanyaga hao daah wana bahati sana vima hao nina gari si siraha hiyo watu wana boda boda aisee
 
Niwe na gari nikabwe na boda boda aisee watu wapo chini ningewagonga ukutani kama nasaga sisimizi nyambafu..
 
Back
Top Bottom