Hii imetokea 10/08/2025, Goba madale karibu na Joy Eslava , mdada alikua anasubiri kufunguliwa geti alisahau remote ndani. Wakati anasubiri, hao jamaa wa boda wakamvamia. aliweza kuwakimbia ila kaumia mkono walimkata na kisu, pia kaumia jicho, vioo viliingia kwenye jicho moja. Asubuhi amesema kuna jirani yake pia amekutwa na tukio linalofanana usiku wa jana yake.
Bodaboda anakatiza pembeni ya gari, kwa mwendo wa kawaida tu hana haraka, hana hofu. Wewe ndani ya gari, unamtazama kwa jicho la haraka unahisi ni mtu wa kawaida, labda anarudi zake nyumbani.
Lakini kumbe ulikuwa umelaghaiwa. Mwenzake aliruka kininja nyuma ya gari, amejibanza kimya, hujatambua uwepo wake,
muda huo unamuoangalia bodaboda au unatumia simu kusubiri geti lifunguliwe, Ghafla – PUU !💥 Jiwe kubwa linatua kwenye kioo kwa kishindo, Kabla hata hujatambua kilichotokea, mkono unapenya dirishani, kisu mkononi.
Hili si tukio la kawaida, ni mtego uliosukwa kisaikolojia, na hata mazoezi ya kurukia angle flani nyuma ya gari ambazo sio rahisi dereva kuona (blind spot)