CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri

CDC Africa: Vipimo vya Corona Virus vinavyotumika Tanzania vinafanya kazi vizuri

Sisi Watanzania tunamsikiliza rais wetu Magufuli
Wataalamu wetu wamepima sample za papai likakutwa na Corona!, hivyo ni kweli zile testing kits ni defectives
P

Testing kits ni defective kivipi? Science ya wapi hiyo? Tangu lini a validated device for human sample ikatumika kwa mapapai, fenesi, mbuzi, nk., ambazo si human being? Mpumbavu hapo ni huyo aliyeipa hiyo device ambayo haikuwa validated kwa tests aina hizo. Ni ujinga wa kiwango cha Flyover kumpandisha beberu kwa mbwa jike kisha ukategemea azaliwe mbogo!!! Hata mimba haitakuwepo, badala yake unaweza kuzua balaa lingine la kiafya. Ni mpumbavu tu atakayeshabikia majibu ya "indeterminate, inconclusive, positive or negative" kutoka kwenye device ya kupima samples za binadamu lakini muhuni fulani anayejiita mwanasayansi akazi"feed" samples za mimea na oil za magari. Shame on him. Ni vema angeificha aibu yake kwa kukaa kimya.
 
Shirika la afya duniani limethibitisha kuwa vifaa vinavyotumika Tanzania ndio hivyo vinatumika Afrika yote na vina ubora unaotakiwa

Taarifa kamili unaweza kusoma hapa

Africa disease centre rejects Tanzania's allegation that its coronavirus tests faulty

Je kwa huu ukimya wa kutangaza nini kinaendelea mitaani naona watu wameamua kutovaa barakoa

Story za vijiweni bila barakoa zimerudi kwa kasi

Watu hawajali tena corona mitaani,Kama kweli ipo basi kuna siku system zetu za afya zinaweza elemewa

Raia chukueni tahadhari sana ya kujilinda ,Tusirahisishe mambo
Kitendo cha watu kuacha kuvaa barakoa mpaka kwenye madaladala ni hatari sana na inatisha.
 
Tatizo la kuchnganya sias, sayansi na kutegemea matokeo mazuri ya kisiasa.

Mama Agela Merkel wa Ujerumani ni Physicist-Mtaalam wa Fizikia.

Lakini katika hili janga la corona amekaa mbali kabisa na kuwaachia mabingwa wa tibabu na afya wapambane na janga hili kwa kuitumia serikali ya Ujerumani.

Matokeo ni ya kuridhisha hata kuliko mataifa makubwa zaidi ya Uingereza na Marekani.
Mkandarasi Jidu acha hizo usimkandie Eng aliye zibeba kampuni zenu
 
Return Of Undertaker,
Kamwambie Ngekasong sisi ni dola huru. Ndio maana kuna tume inachunguza hayo anayosema ni ya kwake na familia yake.
Acheni upuuzi wa kuwaangamiza wananchi . Shule tulifuata nini kama mambo yetu hayatofautiani na watu wasiokanyaga shule ?!. Hebu angalia yanayotokea nchini sasa ?!

Usomi wetu unatoa picha gani nje ya nchi ?!

Odhis *
 
Acheni upuuzi wa kuwaangamiza wananchi . Shule tulifuata nini kama mambo yetu hayatofautiani na watu wasiokanyaga shule ?!. Hebu angalia yanayotokea nchini sasa ?!

Usomi wetu unatoa picha gani nje ya nchi ?!

Odhis *
Jaduong unataka kusema hata kutumia kitengo cha utafiti wa mitishamba cha Chuo cha afya cha Muhimbili ni upuuzi?
 
Return Of Undertaker,

He is rubbish headed, Thanks Ndugu Rais Magufuli, our journey for the greatest tomorrow of ours shall encounter hundreds of battles.
It is a serious mistake to object to a person without having to investigate his or her questions that require scientific investigation

Je Yule kijana Dreva lori wa Kenya, aliyerudishwa kutoka Uganda ambapo alipimwa akaonekana ana maambukizi, na baada ya kurudi kwao Kenya alipopima mara mbili zaidi hakuonekana na Covd,

Hayo sio mashaka ya vipimo vyetu hivi mkuu!!
 
Unakataa kitu kwa ushahidi!!! Siyo kwa maneno.
===
Na ukichunguza CV yake huyo Mkenya unaona kabisa yupo "contaminated" na vinasaba vya kibeberu. Hivyo, siwezi kushangaa namna anavyoiburuza hiyo Bodi ya Africa ya masuala ya udhibiti Magonjwa.
 
Huyo Dr. ameongea hayo akiwa nchi ipi

Msipende kurukia taarifa kabla ya kuisoma kwa undani:
Hii Habari imetoka Addis Abeba-Ethiopia kuliko na AU-HQ maanake huyu Dr. Nkengasong amezungumza na Waandishi wa Habari akiwa Addis Ababa makao Makuu ya AU ambako kuna ofisi za CDC!
 
Mzee Kinje wa kule Chato alikuwa anadhania kila mtu ni zwazwa. Alikuwa anaropoka ropoka tu. Ngoja wataalamu wamfyatue tu.

Upuuzi mtupu! CDC ndiyo ‘manufacturers’ wa hizo‘testing kits’? Badala ya mtengenezaji kuja kutetea bidhaa yake, anakuja Dr kutoka CDC kuja kutetea bidhaa ambayo siyo wao waliitengeneza! Huyu Mtaalam Dr kuna kitu kapewa na watengenezaji wenyewe? Dunia inategemea manufactures wa hizi test kits waje watoe maelezo ya kitaalam siyo mtaalam kutoka CDC kutetea bidhaa iliyotengenezwa na watu wengine kwa maelezo yasiyokuwa ya kitaalam..
 
It's like me buying car from a dealer, then three days later finding out the transmission slips at cruising speed of 60km/h. Calling my dealer to complain about a lemon she sold me, only to be told, "we know it's working".
Suffice to say: what an unfortunate example! Shame upon shame.
 
Upuuzi mtupu! CDC ndiyo ‘manufacturers’ wa hizo‘testing kits’? Badala ya mtengenezaji kuja kutetea bidhaa yake, anakuja Dr kutoka CDC kuja kutetea bidhaa ambayo siyo wao waliitengeneza! Huyu Mtaalam Dr kuna kitu kapewa na watengenezaji wenyewe? Dunia inategemea manufactures wa hizi test kits waje watoe maelezo ya kitaalam siyo mtaalam kutoka CDC kutetea bidhaa iliyotengenezwa na watu wengine kwa maelezo yasiyokuwa ya kitaalam..

Mkuu, kwani wenye nia mbaya na sisi ilikuwa ni watengenezaji au waliotoa msaada? Nilisikia akilaumiwa mtoa msaada. Na kama ni hivo, point yako haina maana yoyote!
 
UVCCM wanashangilia kauli ya binti wa Mohamed Ali na kupuuza kauli ya Mkurugenzi wa Africa Center for Disease Control - which is an authority kwenye masuala ya magonjwa… halafu yule binti unaeza kuta ni teja… maCCM mnashangaza sana…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hatari sana kuvamia professional za watu na wewe kutoa majibu ukidhani upo sahihi kumbe upo chaka wanakushangaa na kukudharau tuu mbaya Sana..
 
Hivi vifaa nani aliingiza Tz?
ndivyo vinatumika ktk nchi nyingine?
kama jibu ndio, kwanini Tz tunahisi vipimo sio sahihi?
Kwanini tumeacha kutoa takwimu za wanaougua? waliolazwa na wanaokufa?
Kuna kitu tunaficha au kipo nyuma ya pazia?
Muda ni mwalimu mzuri sana, uongo hutumia lift kwenda juu bali ukweli hutumia ngazi, japo hufika kwa kuchelewa ukweli hutamalaki.
 
Jana usiku mkuu wa shirika pa kudhibiti magonjwa afrika ((CDC) amekanusha kauli ya magufuli kuwa vifaa vilivyoletwa kupima korona vina matatizo
Screenshot_20200508-114145_Chrome.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi Watanzania tunamsikiliza rais wetu Magufuli
Wataalamu wetu wamepima sample za papai likakutwa na Corona!, hivyo ni kweli zile testing kits ni defectives
P
Pascal, Rais aliyekwishachanganywa na siasa hawezijuwa tofauti Kati ya propaganda ya kisiasa, na hali halisi ya kisayansi. Maana ingekuwa hivyo angepeleka sample halisi kwenye maabara nyingine tofauti ili kujiridhisha.

Sasa kwa kuwa alitaka kupiga propaganda alifanya kisichojuzu, Sasa Dunia nzima inatuona, including you, ma hamnazo!!
 
Back
Top Bottom