CDF Muhoozi: Kuanzia sasa, yeyote atakayemtangaza Bobi Wine kuwa kiongozi wake wa kisiasa lazima 'afutwe'

CDF Muhoozi: Kuanzia sasa, yeyote atakayemtangaza Bobi Wine kuwa kiongozi wake wa kisiasa lazima 'afutwe'

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba amesema Kiongozi wa Chama cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi Ssentamu Bobi Wine ameanzisha vita na taifa lake hivyo kwa namna yoyote ni lazima wamkamate.

Kaine.png

Kupitia mtandao wa X Muhoozi amechapisha akisema kuwa amesikia kuwa Bobi Wine amejificha chini ya choo lakini kwa namna yoyote ile atakamatwa na kuwajibishwa.

“nimesikia Kabobi(Bobi Wine) anajificha chini ya choo, ameanzisha vita na nchi ambayo sasa hivi anajaribu kuikimbia atalipia kila kitu alichofanya” amesema Muhoozi

Ameongeza kuwa haijalishi Bobi Wine yupo ndani ya nchi au lah kwa namna yoyote na kwa faida ya maslahi ya kiusalama na Jumuiya ya Madola inabidi afungiwe kufanya siasa kabisa.

Muhoozi amesisitiza kuwa “Kuanzia sasa, mtu yeyote atakayemtangaza Robert Kyagulanyi (maarufu kama Bobi Wine) kuwa kiongozi wake wa kisiasa lazima afutwe”

Bobi Wine mwenyewe amedai kuwa kwa sasa yupo mafichoni baada kudai kuwa anatafutwa na majeshi ya nchi hiyo kwa kile alichoeleza kuwa wamedhamiria kumtesa.
 
Anasema anamtafuta Bobi Wine kwa manufaa ya Jumuia ya Madola.

Anaongea kama Iddi Amini. Amini nae alikuwa anasema ameikalia British Empire.

Akishika nchi huyu mtoto wa Mu7 nae atakuwa Iddi Amini. Yani Mu7 na Waganda hata hawajajifunza.

Ulipigana kuondoa Amini ili ukistaafu umrudishe Amini kwa saab tu ni mtoto wako! Hatujifunzi.

Na hatuna principle. Hakuna kitu Mwafrika anakikataa in principle. Muda wote mazingira yeyote, hicho kitu Mwafrika anakisimamia, hakuna.
 
Dikteta Saddam Hussein alikuwa na watoto kama akina Muhozi moja akiitwa Udey na mwingine akiitwa Qussey lakini siku ya siku ilipowadia walipelekwa kwa mabikra 72 wenye macho kama mayai.

Hii dunia ina mwenyewe, sasa huyu mjinga amefunikwa na mapepo anajiona mungu mtu lakini siku inakuja asiyoijua naye atabakia historia tu.
 
Ifike muda waafrika waache kushiriki kupiga kura kwenye chaguzi zenye abrakadabra. Waganda wanaona kabisa kumuondoa museven kidemokrasia ni shughuli pevu yule mzee kuachia madaraka kwa kura. Toto lake hilo nalo lina kiburi
 
Marais wa Ki Afrika wakishinda kura zaidi ya 71% to 98%, LAZIMA wawaogope waliowapatia KULA/KURA!
MAAJABU YA DUNIA!
Screenshot_20260127-021750~2.jpg
 
Nepotism, brutality, savagery, killings, torture, corruption, greedy, an order of the day in Africa...
Screenshot_20260127-021806~2.jpg
 
Back
Top Bottom