Cecil Mwambe ashindwa vibaya uchaguzi Kanda ya Kusini

Hakuna tofauti baina ya Mwambe na Mathew kwa kuwa wote wana kadi za ccm na walihamia CHADEMA si kwa mapenzi ya dhati ya chama hicho bali ni kutokana na hasira za kunyimwa fursa kwenye chama chao! Kiufupi chadema hawajapata viongozi wa kanda madhubuti wa kukivusha chama hicho kwa sababu hata huyo makamu mwenyekiti Baruhani pia hasomeki.

Wanachadema wa Kusini wanadhani wataivusha CHADEMA kwa kumkataa Mwambe eti kwavile ni "mpinzani" wa uwenyekiti wa chama wa Mbowe wasijue kuwa wote Mathew na Mwambe wako njiani kurejea ccm.

K
 
Freeman Mbowe ndiye aliyeuwa CHADEMA. Itachukua muda mrefu sana kwa CHADEMA kufikia nguvu waliyokuwa nayo mwaka 2008-2014
 
Very objective opinion
 
Siyo kila MTU anaweza kuwa mwenyekiti hata kama ni demokrasia
 
Kama membe Leo anaandamwa Na bashiru kisa kutaka kumpinga magu hivi vyama basi tu.
Kwani anampinga Magu Kwenye uchaguzi upi?
CCM Imeitisha uchaguzi wa mwenyekiti?
Ulishawahi kumuona MWANACHADEMA anampinga Mbowe hadharani huku akitaka yeye kuwa mwenyekiti na muda wa uchaguzi ukiwa bado kabisa na akabaki salama?
Ukianza kumsumbua mtu aliyepewa majukumu na uchaguzi ni bado sana maana yake unataka asitekeleze majukumu yake.
Kama unataka kugombea na uko serious kwanini usitulie ukasubiri uchaguzi utanganzwe ukachukue fomu ugombee?
Mimi naona haya ni maigizo ya Membe ili akikatwa kwa kutofuata taratibu aanze kulalamika maana anajua ubavu wa kushinda Hana la sihivyo ni mpango wa CCM kuwapatia CHADEMA au moja ya Chama kikubwa awe mgombea wao azigawe kura za upinzani.
 
Ni kweli Mbowe ni kiongozi mzuri sana, lakini miaka 15 ni tosha sana kwake. Sina shaka na hili.
Your not successful until your successor is more successful than you.
Sasa huwezi kusema mtu nikiongozi Mzuri na hawezi hata kutengeneza taasisi na kuandaa viongozi hio inakua sio taasisi tena..
Maana itakufa haraka Sana Hiyo taasisi Huyu mtu akipatwa na Maradhi au akifariki.
Mafanikio ya kiongozi ni kuweza kuifanya tasisi irun bila yeye kuwepo asipokua hivyo huyu ni mtawala sio kiongozi
 
utaelewa baada ya uchaguzi wa 2020 kwamba aliyeiua CHADEMA ni Mbowe na alifanya hivyo mwaka 2015 makusudi Kabisa.
Ninamashaka pia kama huyu Mbowe sio Mrema namba 2.
Uzuri wa waTanzania kufikiri huwa tunaahirisha na tunasahau haraka.
 
Ila pia tukubaliane na hoja vyama tawala vinapandikiza vibaraka wao kwenye vyama vya upinzani ili kuvisambaratisha na ushahidi upo
 
utaelewa baada ya uchaguzi wa 2020 kwamba aliyeiua CHADEMA ni Mbowe na alifanya hivyo mwaka 2015 makusudi Kabisa.
Ninamashaka pia kama huyu Mbowe sio Mrema namba 2.
Uzuri wa waTanzania kufikiri huwa tunaahirisha na tunasahau haraka.
Porojo hizi zungumza pale mitaa ya Lumumba utashangiliwa sana
 
Nyie CCM kinawauma nini Mbowe kuongoza CDM?
 
Hamia CCM, kule hutakiwi kukohoa nbele ya mwenyekiti, nadhani panakufaa zaidi, huku chadema wewe waachie wenyewe
 
Nashangaa, utafikiri mbowe kapiga kura za maruhani kama ccm, hawa watu wa lumbumba kicwani zero, badala wakaendelee kulamba kende za mwenye kiti wao, wapo humu wanamjadili mbowe
Huyo mbowe anawaingia wapiga kura moyoni? Anayejua atuambie.
 
Ni kweli wanatakiwa kwenye Chama, maana Chama makini kitamhitaji kila mtu. Tatizo ni tabia za wanasiasa uchwara wa Tanzania na siasa zao za kutaka kukomoa. Yaani mtu anashindwa kihalali katika sanduku la kura, bado mtu huyo analaumu na kumtupia lawama mtu mwingine asiyehusika huku moyoni ana nia ya kuhama ili kuwakomoa!!!
Ndipo nikasema waende tu kama ndiyo lengo lao.
 
Hii inamaanisha kwamba chadema kanda ya kusini imechukuliwa na mamluki toka cuf
 
Panapo majaliwa tunasubiri pia kuona hapo mwakani Membe atakapochukua form kugombea nafasi ya kuteuliwa kugombea urais huko kwenu itakuwaje.
We shall see what will happen.

Hata mwaka 2015 alichukua form kugombea hata tatu bora hakufika
 
Asante sana
 
Sikukuunga mkono kwa hiyo miaka 10 au 15 na haitatokea niunge mkono hilo.

Ninachounga mkono ni wazo la kufanya kura ziwe halali; na kama unakubali hilo maana yake ni kwamba umefuta hiyo dhana ya miaka 10/15.
 
Na sisi wananchi tumeamua Mh Magufuli awe Rais wa nchi hii mpaka awe kikongwe zaidi ya Mugabe ,kwani ni wananchi tumeamua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…