#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

Chanjo za COVID19 ni jambo la hiari duniani kote. Serikali haiwezi lazimisha wananchi kuchomwa chanjo kama hawataki. Wakifanya hivyo watakuwa wanakiuka na kuvunja haki za binadamu na dunia nzima itawageukia. Huyu ni mshauri mbaya na haufai.
Mimi napenda kukosoa pande zote bila kujali nakosoa CCM au upinzani. Kwa kuangalia mantiki na ukweli.

Mbowe ameonesha udhaifu mkubwa sana katika kauli hii.

1. Ameonesha anapendelea udikteta kuliko demokrasia ya kuwapa watu uhuru wa kuamua.

2. Ameonesha haelewi maadili ya kitabibu yanayokataza watu kupigwa chanjo bila kukubali.

3. Ameonesha hana washauri wazuri wanaoweza kumshauri katika mambo ya kitaalamu kabla ya kuyatolea matamko ya wazi.
 
Mb
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeomba huduma ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali...
Mbowe na elimu zake amefika wakati amepwaya sababu yeye asichukulie Ni mwelewa kuliko watanzania tulio baki. Akachanje familia yake ndipo aje kusema kwa niaba ya walio tayari na siyo wananchi. Akanywe mifaru John yake huko.
 
Hapo wanaharibu.
Wewe sio mtu wa kuandika sentence mbili kwenye jambo nyeti kama hili......hebu dadavua mwenyekiti ameharibu wapi......??

Mbona WHO inainisha kuwa chanjo ni lazima na sio hiari....sasa kama rais Samia ameamua kufuata muongozo wa WHO kwanini anapingana na utaratibu huu......??
 
Mdogo mdogo watazikubali tu, mtu akiwa na safari hapa hawezi kukwepa
Ni kweli. Siyo safari tu ila hata kadiri siku zinavyosonga mbele watu wataelewa somo. Kuna wengine mpaka waone mtu wa karibu kafa ndiyo wanajua hatari ya ugonjwa. Lakini kusema watu wachanjwe kwa lazima sio.

Kabla hawajanza kuchanja mimi nilikuwa nazingojea kwa hamu baada ya kuona watu wanavyokufa. Basi siku moja kazini nikaitwa kuulizwa kama nataka ku-book chanjo.

Cha kwanza walichoniambia ni kuwa siyo lazima hata kidogo. Mimi nikawaambia yaani mngejua nilivyokuwa nazisubiri!
 
Chanjo za Corona zinaweza kuwa lazima kwa Chadema kwa sababu ni mwiko kuhoji wazo la Mwenyekiti ila sio watanzania wote.
Wee mzee umejitokeza tena kwa ile ID yako siyo? Udini utaakuua wewe mzee mzima hovyo!
 
Tusubiri mwitikio wa wananchi
Ukisoma huko mitandaoni, Hakuna anayemuunga mkono Mbowe......suala la Chanjo kila mtu afanye kwa utashi wake tu,ukipata dili kwenda nje utalazimika kuchanja tu,ila kama ni mtu wa Mwanza, Mbeya,Dodoma itakuwa ngumu, labda na private sector baadhi ya makampuni yaseme lazima kwa wafanyakazi
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeomba huduma ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali..
VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA WAWE WA KWANZA KUPATA CHANJO NA TUONE PICHA ZAO NA VIDEO WAKICHOMWA.MBOWE AWE MSTARI WA MBELE
 
Hapo wanaharibu.

Mkuu, ninachokubaliana nawe hapa ni kimoja:

Chadema hawakuwa na haja ya kuingia kwenye marumbano haya. Haswa ikizingatiwa umuhimu wa chanjo hizi kwa mtu unaishia pale tu yeye anapochanjwa.

Ni wazi kuwa hizi chanjo baadaye zitakuwa ni lazima. Itakuwa kama ilivyoanza kwa barakoa. Baadaye huingii kwenye ofisi ya watu, bus, dukani, hospitali, ndege nk bila barakoa.

Alichofanya Mwamba nadhani itakuwa ni katika kufanya sehemu yake ya uelimishaji. Kuonyesha umuhimu wa chanjo hizi ulivyo kwa maisha ya watu. Serikali wanapaswa kuwa wawazi hivi. Kumbuka serikali haijawahi kukiri mtu kufa kwa Corona tokea April 2020.

Zingatia, hata ng'ombe asiyetaka kurejea zizini kuliko salama hupata bakora vile vile.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mbowe kapotoka hapa kuna makundi ya kuchanja binafsi na familia yangu hatupo

Wakawachanje wabibi na wababu huko na watu wenye Ukimwi na kisukari
 
Naunga mkono hoja ya Mbowe, chanjo ya Corona iwe ya lazima, mnaosema hiari bado Corona haijawatembelea ndio maana.
 
Wakati chanjo hizi zinadaiwa kuleta madhara, si vema kulazimisha watu wachanje kwani usalama wa hizi chanjo teyari umeonyesha utata hata huko nje.
 
Wakati chanjo hizi zinadaiwa kuleta madhara, si vema kulazimisha watu wachanje kwani usalama wa hizi chanjo teyari umeonyesha utata hata huko nje.

Wakati chanjo hizi zinadaiwa kuleta madhara, si vema kulazimisha watu wachanje kwani usalama wa hizi chanjo teyari umeonyesha utata hata huko nje.
Kweli kuna baadhi ya nchi chanjo imeleta madhara.....lakini uhiari wa kutoa chanjo hauoni kama itarudisha nyuma juhudi za serikali na umoja wa mataifa kupambana na janga hili....pamoja na kuitia hasara serikali kutokana ughali wa gharama za uagizaji hizo dawa.......???
 
Huyu ana zeeka vibaya sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…