CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!



du! Hii analysis nimeikubali ni ya kweli, mimi ni mwanaccm ila kiukweli naipenda chadema na ni mojawapo ya wanaccm tuliokuwa na imani kubwa kuwa cdm itakomboa hii nchi, ila sasa kiukweli tumekata tamaaa na matokeo yake ndo kama tunavyoshuhudia
cdm inahitaji kuuchukua huu ushauri kama ulivyo na kuufanyia kazi sambamba na sawia!
 
Naunga mkono CHADEMA kushiriki uchaguzi mdogo wa chalinze kwa sababu zifuatazo
1. ni fursa ya upinzani kuelezea sera zake kwa umma
2. ni fursa ya kujijenga kisiasa kwa changuzi mbali mbali zijazo
3. ni ukomavu kuonyesha inakubalika hata kwa kuweza kusimamisha mgombea eneo husika (fuatilia rekodi ya vyama vinavyoshindwa kusimamisha mgombea maeneo mbali mbali kwa kukosaa mtandao na hata kuungwa mkono katika hatua za awali)
4. ni uwanja muhimu wa kuichachafyaa serikali na chama tawala
5. ni fursaa pekee (kwa aina ya mgombea wa chama tawala uhusiano wake na mtawala) kuelezeaa mapungufu ya kiungozi ya mtawala moja kwa mojaaa.
 
Mimi ninaamini chadema walijipanga, lazima walikuwa na mikakati kam ambayo tumekwisha ishuhudia hasa hiyo ya M4C na operesheni nyingine nakadhalika lakini ukweli ni kwamba matokeo ya mikakati hiyo hayakuwa n aushawishi mkubwa na wakudumu mpk sasa!chadema wanatakiwa kufanya tathimini upya na kuja na njia mbadala(mikakati) ya kujiokoa katika muda huu mfupi!ikumbukwe kwamba mikakati yoyote ya kuijenga chadema inaenda sambamba na mikakati ya ccm ya kuibomoa au kuidhoofisha chadema ndani na nje ya chadema yenyewe!

Watanzania wengi wanaonekana kuchoshwa au kukata tamaa na mambo ya siasa,ni kama hawaoni namna ambavyo wanasiasa wanaweza kuwaleta mabadiliko hivyo wanajiweka pembeni kweny mambo ya siasa na hasa upigaji kura na uongozi wa vyama vya upiznani kuanzia kwnye ngazi za chini,wengi tunazungumza hapa kwenye majukwaa kama haya au kutegemea wengine wawe mstari wa mbele lkn ni wangapi tupo mstari wa mbele ktk siasa za mtaani au kwenye kata zetu,matokeo yake ni kuona kuwa watu ni wale wale wa ccm wakijihusisha na siasa za jana, leo na kesho ndio ha hao wanapiga kura na kufanya maamuzi ya nani atwae dola, ndio hao hao wanapata orientation za siasa!

Pamoja na ugumu wa kupata wafuasi wa wazi wa vyama vya upinzani na kufanya siasa za upinzani katika mazingira magumu haya ya utawala wa ccm lazima chadema itumie mbinu mbadala vinginevyo itakuwa historia tu,ugumu usiwe sababu ya kukata tamaa bali uwe chachu ya kusonga mbele kimkakati zaidi!
 
Hiki chama ni sawa na kundi la misukule hawajui walipo,hawelewi walipotoka wala hawajitambui wanakokwenda, kushabikia chadema lazima uwe na akili za kobe.
Kweli we ni chuki
 
Tatizo la Chadema ukiwakosoa wanakuona adui sielewi kwanini wanaendelea kutumia helikopta kwenye kila chaguzi kwani gharama wanazotumia ni nyingi ukilinganisha na gharama ambazo wangetumia kujenga mtandao ngazi ya chini.
wanachama wengi hawaijui hata Chadema tunaweza kusema wengi ni washabiki ni ukweli usiopingika Chadema inaitaji mwenyekiti mwenye mawazo mampya kwani mazingira ya mwaka 2010 ni tofauti na 2015 ccm watakuja na mgombea mwingine na hoja za ufisadi pamoja bado upo lakini hazitakuwa na nguvu kama za wakati ule
kuna sehemu kama lushoto chadema wana nguvu lakini wanakosa sapoti toka juu ndio maana tunasikia mgombea anashindwa lakini baadae ananyang'anywa ushindi bila chama kusema chochote huu ni udhaifu mwingine wa chadema si ajabu wakashindwa kusimamisha wagombea kwenye majimbo mengine sababu hawajajenga nguvu inayotakiwa kwenye mizizi ya wananchi wananchi wengi wa Tanzania hawaingii kwenye mitandao ukweli ccm imechokwa lakini chadema wameshindwa kutumia nafasi hii kwa faida yao
 

Nakuunga mkono asilimia 100. Ikizingatiwa kwamba mwaka 2010 hawakuweka mgombea katika jimbo hilo na ccm wakapeta na kuzoa kura asilimia 90.
 
Kwangu mimi siku zote Pasco ni chizi tuh au futuhi,lakin leo nimeshangaa chizi kuandika vitu vya msingi kama hivi,umemaliza dose au???

Msalimie Nikupateje...
 
Last edited by a moderator:
Chadema kwa kuwa kalenga walishinda kwenye viunga vya kanisa nawashauri chalinze wakashinde viunga vya misikitin,si wameyataka wenyewe??

Waache yawakute
 
Tatizo la Chadema ni kuamini kwamba wamekubalika na wananchi na kwamba 2015 watatinga ilkulu.Hiyo ni ndoto ya mchana na ni ukweli mchungu kuupokea.Viongozi wa Chadema ni wenye jaziba na wasiopenda ushauri wa mtu yeyote yule hasa ushauri huo ukiwa na mwelekeo wa kuwakosoa.Chadema jipangeni!
 
Chadema wanaponzwa na kiburi,ubabe na ubishi hii lazima iendelee kuwatesa chadema ni chama cha watu fulani hao ndiyo wenye maamuzi nacho.
 


Pasco,umeweka analysis yako vizuri,ila kuna issues ndogo ndogo ambazo haujazifanyia reaserch ya kutosha au haujaamua kuyaweka bayana tukayaona.

Je,unadhani Serikali yetu ya CCM imekubali vyama vingi kwa moyo mmoja?
Je,unadhani Serikali yetu itakubali watanzania japo asilimia 70 iwe imejiandikisha by 2015.
Je,unadhani Serikali itakubali kuwe na uchaguzi HURU na HAKI?
Je,TUME zetu zote mbili zinazohusiana na Chaguzi,zinaweza kuwa HURU na HAKI kwenye utendaji wake?

Kama tukiweza kupata majibu ya haya na kila mtoa RUSHWA TUME hizi zikatoa adhabu stahiki basi UPINZANI waweza kuwika na hapa nimesema UPINZANI sababu HAKI na UHURU hauchagui vyama vya UPINZANI,bali vyote vinamatatizo yanayoshabihiana kwenye suala la upatikanaji wa HAKI na UHURU wa kukipigia chama cha UPINZANI.
 
Wewe ni mlevi wa pombe za kienyeji huwa nakudharau sana
 
Chadema kwa kuwa kalenga walishinda kwenye viunga vya kanisa nawashauri chalinze wakashinde viunga vya misikitin,si wameyataka wenyewe??

Waache yawakute
Tapeli la gesi ndani ya Nyumba!!!!! mabomba yamefika kinyerezi wewe tapeli tayari kuanza kutumia kama vipi jiue
 
Hivi Pasco,wajua huko vijijini wengi hawajui haki zao za msingi?Tunaoenda vijijini tunaelewa mengi kuliko mlioko mijini.Kama mtu ananyang'anywa ardhi kwa kumtishia kumuweka ndani na bila hiari anakubali kuitoa ardhi kwa watendaji ili mabwana wakubwa wenye pesa zao wa hodhi maeneo yenye rutuba.

Kama haya hawayajui,je haki za vyama vingi watazijua?Kuna wakati nilikuambia kazi ya waandishi wahabari hasa wewe uliyesoma sheria ni kuelimisha UMMA wa watanzania ambao haki zao za kisheria zilizoainishwa kwenye KATIBA hawazijui,mmefikia wapi?Je,kweli utakuwa na HAKI ya kuwalaumu CDM wakati hata wewe nafasi yako haujaitendea HAKI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…