CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

Kumbe wewe hunijui?!. Basi kwako na wengine wasionijua, mimi ndiye ninayetoa fedha zangu mfukoni, kuigharimia Chadema kujiendesha!, hivyo nina mamlaka yote 100% kujua kila kitu Chadema inachofanya!.

Pasco
Pasco katika ubora wake
 
Last edited by a moderator:
Nafanya Rejea kwa seke seke ya CUF,jee Chadema wako imara? . Kwa 2015 Chadema hawakujipanga, jee kwa 2020 watajipanga? .
Paskali
 
Nafanya Rejea kwa seke seke ya CUF,jee Chadema wako imara? . Kwa 2015 Chadema hawakujipanga, jee kwa 2020 watajipanga? .
Paskali
Wenda wanasubiri uchaguzi wa mihemko tena Mkuu.


Kumchagua mtu kwa kumwelewa nini anakuletea na kumchagua mtu kimihemko vitu tofauti.
 
binadamu wameubwa na kuchwa kwa ajili ya kuweka nywele tu wakati wengine nywele si mhimu sana ila kwenye kichwa kuna ubongo ambao unahifadhi kumbukumbu na kujua mazuri na mabaya,hv ww kama una akili timamu kichwani mwako unaweza kusema kauli kama hiyo kuwa chadema hawajajipanga kwa uchaguzi ina maana kama siasa zinafanywa za upande mmoja upande wa pili wasubili hadi wakati wa uchaguzi hiyo kweli inaingia akilini!kwa kauli yako hiyo ruhusu kila mwezi ruhusu siku moja tu wao wafanye kila cku uone mziki wake!yaani kama lowassa apite tu bila kuongea kitu utaona mafuriko!uoga umewazidi igeni mfano kwa musure mzee wa msoga!
 
Nafuatilia kwa karibu, hii movement ya viongozi wa Chadema huhamia CCM, kama ina uhusiano wowote na Chadema kutokujipanga.

P.
 
CHADEMA wanapitia wakati magumu sana.

Tusubiri tuone wataibuka namna gani, maana wanajificha sana kwenye neno "USALITI" na "WASALITI"
 
Mkuu 50thebe, ni kweli Chadema inapitia wakati mgumu kabisa kuliko kipindi kingine chochote.

Paskali

Hakika

CHADEMA kama taasisi, wanachama, wapenzi, viongozi na hata waandamizi wake sidhani kama walipata kufikiri kuwa wangepitia hatua wanazopitia wakati huu.

Jambo la kustaajabisha, tena la kustaajabisha zaidi ni namna wana CHADEMA wanavyoelekeza shutuma na lawama zao kwa Mwenyekiti wa CCM Mh Magufuli. Maajabu kabisa. Ndugu zetu hawa hawaoni kabisa kwamba wao ndio waasisi wa anguko lao wenyewe.

Mkuu paskal Mayalla wewe ni shahidi. Hapa nchini mwetu vyama vya upinzani havijawahi kupata wepesi wa kukabiliana na CCM. Wakili Lamwai na wenzake walikuwa karibu waiangushe CCM mwaka 1995/96 wakiongozwa na Mh Mrema. Tuliona namna NCCR-Mageuzi ilivyopoteana baada ya uchaguzi ule. Bila shaka watangulizi wa CHADEMA waling'amua kwamba haiwezekani kuing'oa CCM kwa kutumia makapi ya CCM.

Fast forward, kazi ya Dr Slaa kuijenga CHADEMA hususani ujio wa kitu alichokiita "inteligensia ya chama" kilifanikiwa sana kuidhoofisha CCM. From no where, CHADEMA ikakumbatiana na Mh Lowassa. Miaka miwili (2) ya uwepo wa Mh Lowassa ndani ya chama hiki, hakuna anayejua tena ni nini chama hiki kimekusudia kufikia. Watoto wa mjini wanasema 'wamepoteana'.

Mbaya zaidi badala ya chama hiki kuketi kitaasisi na kujitafakari wapi kimeboronga na kifanye vipi kurejesha hadhi na uimara wake, tunasikia malalamiko kuhusu kukandamizwa na CCM. Ni lini CCM iliviacha vyama vya upinzani kufanya kazi za siasa vitakavyo? Waliwezaje waliofikisha CHADEMA kwenye chama kikuu cha upinzani na wanashindwaje waliopo kutunza hadhi hii?

Chama cha demokrasia na maendeleo kitaendelea kupitia wakati huu mgumu kwa muda mrefu ujao, mpaka pale viongozi waandamizi wenye kushikilia maamuzi watakapokiri kuwa wanapaswa kujiongeza ili waweze kushindana kisiasa na CCM.
 
Matokeo ya kushindwa Chadema, sasa ndio yatawaamsha wengi kuwa Chadema haikujipanga, haijipangi, na haitajipanga!, its very unfortunately, kufikia 2020, Chadema will be reduced to almost nothing, hivyo uchaguzi wa 2020 ndio utakuwa rasmi kwa Chadema ni bye bye!.
P
 
Rafiki yangu paschal Mbowe anajipangaje kwa mfano hajui ata theory moja ya mapinduzi/mageuzi duniani acheni kufanya maisha mapesi hivyo na kuiona elimu haina maana hasa zama hizi
 
Sasa Chadema inaanza kujipanga kwa kuonyesha ukomavu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kuwashughulikia wanaoitwa wasaliti, ambapo katika kuushughulikia usaliti wa Zitto, Kitila na Mwigamba, walitumia ujinga!, lakini katika kushughulikia usaliti wa Kubenea na Komu, busara imetumika, Sisemi kuwa safari hii busara imetumika kwa sababu tuu ya Komu being Mkaskazini, bali safari hii busara imetumika, kwa sababu sasa Chadema inakuwa more mature, ule ujinga ujinga katika issue ya Zitto ulikuwa ni utoto tuu, na ujana, sasa inamature katika utu uzima.

Hongera sana Chadema for maturity, sasa mnaanza kujipanga, ila not for 2020, its too little too late, wanaoondoka waachwe wajiondokee, kazi ya kuijenga upya Chadema ya kuendeleza opposition, iendelee katika hatua za awali kwa ajili ya 2025.

P.
 

Naam

Binafsi nimefurahi pia kuona CHADEMA inajifunza kwa vitendo kuachia "ngano na magugu" viote pamoja. Hekima hii imefika kwa kuchelewa. Walau imefika. Ni jambo jema
 
Baada ya Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni super man, nimemkumbuka naomba nimdurusu kidogo, niliwaji kusema nini humu kumhusu mtu huyu.

P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…