CHADEMA itajengwa na wenye moyo safi. Waanza kujenga ofisi zao za Majimbo kwa kujitolea

Afu kuna mtu alikuwa anasema eti atahakikisha kufikia 2020 CDM haitakuwepo nchini.....cha ajabu yeye ndo hayupo na CDM inachanga mbuga.... dunia hii aisee!!
 
Hii ni njia mojawapo ya kupata wafia chama.
Ofisi ni mahali pa kupatia wanachama wapya.
Ofisi ni mahali pa kutolea mafunzo kuhusu sera za chama, katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Ofisi ni mahali pa kubandika matokeo ya chaguzi mbali mbali za chama na serikali.
Ofisi ni mahali pa kubandika matangazo mbali mbali ya chama na serikali.
Atakayeguswa na kuchangia ujenzi wa ofisi hizi ni ngumu sana kuunga juhudi aidha kwa kununuliwa au kwa ridhaa.
 
CHADEMA kwa hili napinga nanyi, CHADEMA ina wanachama zaidi ya milioni 1 kila mwanachama akitoa 500 tu (1,000,000 x 500=500,000,000) si zaidi ya ofisi 10 jamani, mnafeli wapi?
Uko sahihi, hayo ndio matamanio lakini uhalisia ni tofauti. Kumbuka kutoa ni moyo, na sio wote wanamudu kutoa.
 
CAG alikagua matumizi ya ruzuku ya Chadema akatoa hati safi, ujenzi huu ni michango ya wanachama sio ruzuku.

yule CAG wa chadema 😂😂,ivi mlimhonga vp akawapa hati safi, mpaka leo sjui ruzuku yenu imetumikaga wapi na ni kodi za wananchi
 
Afu kuna mtu alikuwa anasema eti atahakikisha kufikia 2020 CDM haitakuwepo nchini.....cha ajabu yeye ndo hayupo na CDM inachanga mbuga.... dunia hii aisee!!

mnachanja wap mbuga sasa?
1621858452389.png
 
Umasikini wako wa akili na mali hauwezi kuondoka kwa kuichukia Chadema na pia kuichukia kwako Chadema hakuwezi kukupa uteuzi kama ilivyokuwa enzi za yule dhalim anayeteketea motoni hivi sasa. Utaendelea kutoa comments zako za kipumbavu humu zisizokuwa na mantiki na mwishowe utaendelea kulawitiwa tu kwa hela ya mboga.

kwan wewe ukiipenda chadema ndo ataachia uenyekiti akupe?
 
nitachangia ofisi tatu ujenzi ... kiwango kikiungana na wengine kitafanya kitu.. Aluta continua
 
Nimeona number ya Chadema Karatu tu , naomba za Bunda na Serengeti ... Nachangia hizo ofisi tatu..
 
Itaondoka ila siyo kuondolewa na vyama. Itaondolewa na wananchi wenyewe.

Hao wanasiasa wenyewe ni wale wale. Wazee wa fursa.

Hata leo ikiingia madarakani CHAUMA watahamia huko huko. Ikiingia CHADEMA hao hao CCM watahamia huko huko.
Very interesting.

Mkuu kwa mawazo haya unadhihirisha kuwa wewe ni mmoja ya watu wasioamini kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa (multiparty democracy) unawezekana Tanzania. Bila shaka "wanasiasa" tulio nao - hao unaowaita "wazee wa fursa" - ni kioo cha jamii yetu. Ndivyo sisi tulivyo. Hivyo, usitarajie wananchi waiondoe CCM madarakani. Wananchi na wanasiasa ni dugu moja.

Kama sijakosea basi, nakupa rai kwamba badala ya kutoa kasoro "ndogondogo" za vyama ni bora zaidi, UKIWEZA, utoe elimu kuhusu vipi tunaweza kutengeneza mazingira ya kuwa na wanasiasa makini wanaoelewa, wenye msimamo na wenye uwezo wa kushindanisha itikadi, sera na mifumo mbadala makini kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa? Demokrasia ya vyama vingi haina maana kama Watanzania wengi hasa wanasiasa hawaelewi maana wala hawawezi kupigania, itikadi, sera, na mifumo mbadala kwa ajili ya mustakbali wa taifa. Kama kweli wote ni watu wa tamaa ya ukwasi tu.

Mimi binafsi, baada ya kuusoma kwa undani mwenendo mzima nchini na katika nchi mbalimbali hasa za Afrika, naamini kwa kiasi kikubwa multiparty democracy HAIWEZEKANI Tanzania. Nilivyoona ni kuwa uelewa wa mambo haya uko chini mno; umasikini na uroho viko juu sana. Wengi wanadhani nchi inatakiwa kuongozwa na mtu (mmoja) maalum "atakayelikomboa au kulivusha taifa". Mtu atakayeabudiwa kama MASIHI! Lakini kwa vile kivuli cha multiparty democracy ni kete muhimu ya dola katika diplomasia ya kimataifa na pia ni "sekta" muhimu ya ajira/ulaji kwa wajanja wengi, basi "uongo" huo utakaoendelea kuwepo mapaka wengi wanyoshe mikono juu.

Kwa upande mwingine kuna "kafaida" kadogo tunapata. Pamoja na ubabaishaji wote unaofanywa na dola, tumeshuhudia jinsi vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyoitikisa dola na kutunusuru na maanguko kadhaa. (pulling the nation back from the abyss). Bila hivyo, kuna wakati viongozi walielekea kuvuka mstari katika ufisadi na ukiukaji haki za binadamu wakajikuta wakivutwa shati na upinzani na kujirudi kiasi - pamoja na kuendelea kubisha! Hata ndani ya chama tawala ukiwaambia kusiwe na upinzani kabisa wako wengi watakuwa mashakani. Lakini gharama ya multiparty system ni kubwa mno.
 
Naamini kwenye vyama vingi ila siamini kwa wanasiasa kwasababu wanasiasa lao moja.

Wananchi wanapaswa kulijua hili.

Mfano: Magu hakuwa na tatizo na Lissu ila tatizo lilikuwa Lissu kupita barabarani na kuwazindua wananchi.

Mwanasiasa kukupa wewe ulaji ili usiwasemee wananchi ni rahisi tu kuliko kutatua changamoto zinazofanya mwanasiasa asiungwe mkono na mwananchi.
 
Back
Top Bottom