Very interesting.
Mkuu kwa mawazo haya unadhihirisha kuwa wewe ni mmoja ya watu wasioamini kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa (multiparty democracy) unawezekana Tanzania. Bila shaka "wanasiasa" tulio nao - hao unaowaita "wazee wa fursa" - ni kioo cha jamii yetu. Ndivyo sisi tulivyo. Hivyo, usitarajie wananchi waiondoe CCM madarakani. Wananchi na wanasiasa ni dugu moja.
Kama sijakosea basi, nakupa rai kwamba badala ya kutoa kasoro "ndogondogo" za vyama ni bora zaidi, UKIWEZA, utoe elimu kuhusu vipi tunaweza kutengeneza mazingira ya kuwa na wanasiasa makini wanaoelewa, wenye msimamo na wenye uwezo wa kushindanisha itikadi, sera na mifumo mbadala makini kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Taifa? Demokrasia ya vyama vingi haina maana kama Watanzania wengi hasa wanasiasa hawaelewi maana wala hawawezi kupigania, itikadi, sera, na mifumo mbadala kwa ajili ya mustakbali wa taifa. Kama kweli wote ni watu wa tamaa ya ukwasi tu.
Mimi binafsi, baada ya kuusoma kwa undani mwenendo mzima nchini na katika nchi mbalimbali hasa za Afrika, naamini kwa kiasi kikubwa multiparty democracy HAIWEZEKANI Tanzania. Nilivyoona ni kuwa uelewa wa mambo haya uko chini mno; umasikini na uroho viko juu sana. Wengi wanadhani nchi inatakiwa kuongozwa na mtu (mmoja) maalum "atakayelikomboa au kulivusha taifa". Mtu atakayeabudiwa kama MASIHI! Lakini kwa vile kivuli cha multiparty democracy ni kete muhimu ya dola katika diplomasia ya kimataifa na pia ni "sekta" muhimu ya ajira/ulaji kwa wajanja wengi, basi "uongo" huo utakaoendelea kuwepo mapaka wengi wanyoshe mikono juu.
Kwa upande mwingine kuna "kafaida" kadogo tunapata. Pamoja na ubabaishaji wote unaofanywa na dola, tumeshuhudia jinsi vyama vya upinzani hasa CHADEMA, vilivyoitikisa dola na kutunusuru na maanguko kadhaa. (pulling the nation back from the abyss). Bila hivyo, kuna wakati viongozi walielekea kuvuka mstari katika ufisadi na ukiukaji haki za binadamu wakajikuta wakivutwa shati na upinzani na kujirudi kiasi - pamoja na kuendelea kubisha! Hata ndani ya chama tawala ukiwaambia kusiwe na upinzani kabisa wako wengi watakuwa mashakani. Lakini gharama ya multiparty system ni kubwa mno.