Uchaguzi 2020 CHADEMA, kazeni buti zenu, you are almost there. Adui yuko hoi, ushindi uko wazi mno!

Uchaguzi 2020 CHADEMA, kazeni buti zenu, you are almost there. Adui yuko hoi, ushindi uko wazi mno!

Kwa hiyo uhuru na haki waliyonayo ndiyo maana wagombea wao wameenguliwa, uhuru na haki waliyonayo ndiyo maana vyombo vya habari havimtangazi mgombea wao uhuru na haki waliyonayo ndiyo maana watu wanatoa maoni kwakutumia fekelo. Hivi kutoa maoni hapa kwa kutumia fekelo ndo uhuru na haki tunayotakiwa kujivunia. Kumbe wale wajinga kati ya maadui watatu mmoja wapo ni wewe.
Moja ya mambo muhimu yaliyoanishwa, na kukubaliwa na vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu, 2020, katika MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI YA MWAKA 2020 (Chini ya Kifungu cha 124.A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343), ni

2.1 (f) kutumia vyombo vya habari vya umma kutangaza sera zao kwa kuzingatia Sheria ya Vyombo vyaHabari Sura ya 229, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Vyombo hivyo vinaweza kutumiwa na Wagombea wa Urais na kugharamiwa na Serikali.

Je, una uhakika wagombea wamenyimwa fursa hiyo? Naamini hawavitumii vyombo hivyo kwa sababu wanazozijua wenyewe.
 
Nyie mnadhani CCM ni kama chama chenu kile kiongozi anaamka tu anawachangisha wabunge akiwa na kiu ya konyagi, kuitoa CCM madarakani ni vita kuu ambayo uchumi utaporomoka, watu watapoteza maisha, of which ni very un-nesseary, sasahivi CCM is doing a very good job na watu wanaiunga mkono 100 kwa 100
Wakina nani?
 
Hongera kwa chapisho zuri lenye upako. Binafsi Lissu nilimwelewa kitambo sana na kumchangia pale alipohitaji msaada. Wale wote waliomchangia kuanzia 2017 HD juzi tu kuwatoa Viongozi gerezani kura hizi HAZINA vikwazo
Kitendo cha kuitega Kamati Kuu ya Chama chake kufanya maamuzi, naye kukubali maamuzi ya Kamati kuu kimemuinua sana na kumuongezwa sifa zaidi. Ni dhahiri kaonyesha kwa vitendo yeye ni Mtii na msikifu, sifa kubwa sana hii.
 
Laiti ungeomba CHADEMA ikiingia madarakani ishughilikie mageuzi ya kiuchumi ili kutokomeza maadui watatu (umaskini, maradhi na ujinga) maombi yako yangesikilizwa.

Kwakuwa hamjui hao ndio maadui wakubwa wa Watanzania, usingeomba uhuru wakati ni uhuru na haki waliyo nayo wataenda kupiga kura. Uhuru na haki waliyo nayo wagombea ndio wanatumia kufanya kampeni. Uhuru na haki uliyo nayo ndio umetumia kuleta bandiko hilo.

Unajitambua kweli kushabikia CHADEMA chenye viongozi wenye kila sifa ya uovu, ili wakabidhiwe nchi?
Maradhi ,ujinga na umaskini vimeumbwa na CCM
 
Nyie mnadhani CCM ni kama chama chenu kile kiongozi anaamka tu anawachangisha wabunge akiwa na kiu ya konyagi, kuitoa CCM madarakani ni vita kuu ambayo uchumi utaporomoka, watu watapoteza maisha, of which ni very un-nesseary, sasahivi CCM is doing a very good job na watu wanaiunga mkono 100 kwa 100
Labda wewe na mkeo,mamako na babako
 
Labda wewe na mkeo,mamako na babako

na hawa apa
1601926695016.png
 
Huwezi kufunga mjadala...

Mjadala unaendelea. Wewe ndiye lala maana "mnapendwa" lakini cha ajabu kutwa nzima, mnapiga propaganda ku neutralize mambo ...

sasa mjadala unaendelea aje wakati mna gap la kucover apo ndo mue na sauti, nyie hulka yenu ni ubishi wa konyagi always
 
Magufuli ni takataka hata mke wake na wanaye hawata mpigia kura. hata yeye mwenyewe a ajuwa ila linazimisha tu kwakuwa bado lina mamraka ya kutumia majeshi ila ukweli halina ujaja wala akili ya kutawala hata kijiji.
 
Mungu wa Israeli amesikia kilio cha Watanzania cha miaka mingi.

Mungu wa Israel ameona mateso ya watu wake na sasa ameshuka mwenyewe kuja kutukomboa.

Mungu kampiga upofu wa fikra na ufahamu adui. Nguvu na manlaka yao siyo kitu tena. Havina msaada kwao. Haviwezi kuwaokoa na anguko kuu la kushindwa.

CHADEMA na Tundu Lissu ni zana tu za ukombozi wa nchi hii anazotumia Mungu. Lakini ukweli ni kuwa yeye mwenyewe Kristo simba wa Yuda yuko kazini anaokoa!

Adui ameshaona na amenusa kushindwa kwake. Yuko so desparate.

CCM na Magufuli ni kama simba aungurumae kumtafuta yeyote aliyekaa kihasara na mwenye hofu ili amle.

Lakini kiukweli ni kuwa, CCM na Magufuli wala siyo simba bali wanaigiza usimba.

Kama hujagundua kuwa unachosikia sio sauti ya simba, bali ni ya kumuigiza simba, basi unaweza kuanza kutimua mbio kumkimbia simba - mbuzi.

Sisi tuko serikalini. Ni wazalendo katika kambi ya adui. Tunawahakikishia kuwa adui kwa ndani ameshakwisha habari yake. Mnavyomwona kwa nje ni fabrication tu, MSIOGOPE. Songeni mbele!

Mungu yuko pamoja nanyi. Sisi huku tunawapa habari zote kwa kadiri tunavyozipata na zilivyo. Tu wadogo sana, lakini tunajua kila kitu.

Mna siku zisizozidi 23 kuanzia leo ku - revisit mikakati yenu ya ushindi. Nawahakikishia tena robo tatu (3/4) ya machinery za kidola zinawaunga mkono tukiwemo 99% ya watumishi wa umma.

Tuko upande wenu. Nasi tunahitaji kuwa huru. Tuko tayari kusaidia kumwangusha Farao wa Misri iwe kwa kutaka ama bila kutàka.

Mpango mzima uko kwenye vituo vya kupigia kura. Angazieni uko. Mikakati na nguvu zote zielekezwe huko. Ishu haiko kwenye kampeni na nyomi.

Tundu Lissu hata asipofanya kampeni, anashinda unless mshindwe kuweka mikakati thabiti kwenye vituo vya kupigia kura.

Njooni na mkakati wa kudhibiti kura za kila kituo cha kupigia kura ili kuhakikisha kuwa kura zinakuwa halisi zilezile zilizopigwa.

Hakikisheni mnaweka mawakala kila kituo, wanaapishwa kwa wakati, wanaingia vituoni na wanapata nakala ya matokeo kwa kila kituo cha kupigia kura.

Msifikiri sana kuhusu fedha kwa sababu fedha haiwezi na haijawahi kufanya kila kitu kwa mwanadamu.

Tazameni, wao wana fedha nyingi kuliko maelezo. Lakini mbona haziwapatii upendo na kila kitu wanachokihitaji? Fedha kwao imeleta uhasama na mgawanyiko kuliko kufikia lengo lao.

Wekezeni kwenye kile watu wanachohitaji. Watu wako tayari kwenda kwenye vituo kuwa mawakala wenu hata bila malipo ili mradi waufikie ukombozi wao.

Watu wamechoka. Watu hawako huru. Watu wamefungwa na wako gerezani. Watu wanahitaji kufunguliwa.

Mungu mwenyewe yuko kazini kujibu kilio cha watu.

Pokeeni heshima hii ya pekee aliyowapa Mungu kupitia mja wake Tundu Lissu ili kuwatoa watu wake kwenye utumwa wa Misri wa zaidi ya miaka 57.

Hili ndilo jukumu alilopewa Tundu Lissu.
Ok.
 
Back
Top Bottom