Uchaguzi 2020 CHADEMA kutikisa Dar kwa siku tatu, Uchaguzi Mgombea Urais Tanzania na Zanzibar

Alikuwa
Ni mpango wa MUNGU kuiwezesha chama kulipwa ruzuku kubwa na kujiimarisha toka kwrnye tawi. Bahati mbaya hii iligunfulika na kuzuiwa mikutano ya kisiasa kwacvyama vya upinzani. HILI LINAHITAJI UFAHAMU WA JUU KULIONA
Hakika Chadema ni mpango wa Mungu.Ajiulize swali kingine vipi wale waasi waliohama chama wameshinda kura za maoni walikokimbilia kuhemea?
 
Molemo Media tunakufuatilia kwa zero distance , tuko pamoja sana
 
Hivi hakuna namna ya ku-Skip hiko kikao cha kumtafuta rais? Lissu anatosha, CDM hangaikeni na wabunge tu na viongozi wengine.
 
Ki
Kichwa cha habari cha uzi huu, kwa kweli hakiendani na habari yenyewe! Mikutano hiyo ni ya kawaida sana hasa kipindi hiki cha uteuzi na utia nia kabla ya uchaguzi mkuu utakao tanguliwa na uteuzi wa wagombea wa Udiwani, Ubunge na Urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi yaani NEC hapo tarehe husika itakapofika. Si jiji la Dar-es-Salaam wala Tanzania itakayo zizima wala kutikisika ndugu yangu.
 
 
Hivi hakuna namna ya ku-Skip hiko kikao cha kumtafuta rais? Lissu anatosha, CDM hangaikeni na wabunge tu na viongozi wengine.
Tunafuata taratibu zote kikatiba mkuu
 
Mwenye macho haambiwi tazama.Dunia inajua
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinatoa taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma wa Watanzania kuhusu ratiba ya vikao vya ndani ambavyo vitahitimisha uteuzi wa Mgombea wa Urais na Mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Zanzibar.

Vikao hivyo vya kitaifa ambavyo ni, Kamati Kuu ya Chama, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, vitaketi kwa siku tatu mfululizo na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya Mwaka 2006, Toleo la Mwaka 2019.
Kikao cha kwanza kitakuwa ni Kamati Kuu ya Chama itakayokutana Jumapili, Agosti 2, mwaka huu, itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kikatiba unaoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.16(a) “Kufanya utafiti wa wagombea wa Urais na Mgombea Mwenza na kuwasilisha ripoti zake kwa Baraza Kuu.”

Tarehe 3, Agosti 2020, Baraza Kuu la Chama litakutana katika kikao chake, ambapo litajadili masuala mbalimbali ikiwemo “kufanya mapendekezo ya wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuyawasilisha katika Mkutano Mkuu kwa uamuzi,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.12(a).
Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.12 (n) Baraza Kuu litajadili rasimu ya Ilani (manifesto) ya Uchaguzi Mkuu na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu kwa maamuzi.

Tarehe 4, Agosti 2020, Mkutano Mkuu wa Chama utaketi na kutekeleza kazi zake, ikiwemo “kuteua mgombea wa Urais na mgombea mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais wa Zanzibar,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.10 (c). Halikadhalika, Mkutano Mkuu wa Chama utainidhinisha Ilani (manifesto) ya Chama kwa Uchaguzi Mkuu, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.10 (h).

Vikao vyote kuanzia Agosti 2 hadi 4, 2020, vitafanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Imetolewa leo Jumamosi, Agosti 1, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
 
Hiki chama kinaangalia urais tu hakitapata wabunge,Madiwani na wenyeviti wa kitongozi tutakipaje Nchi Nyerere hiki chama alishakilaani alisema tusifanye Majaribio
 
Ninawatakia Chadema mkutano mwema, wa heri, na mafanikio katika kudumisha demokrasia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…