Pre GE2025 CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mkuu 2025 litakuwa ni pigo kubwa sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali ya CCM kidiplomasia na kiutawala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,042
Reaction score
3,674
No reforms, no election ni mfupa mgumu sana kwa CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa kitaifa October 2025.

Kama serikali ya CCM italazimisha kufanya uchaguzi pasipo ushiriki wa chama kikuu cha upinzani Tanzania yaani CHADEMA basi litakuwa ni pigo kubwa sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan kidiplomasia hasa katika nyanja ya demokrasia kimataifa.

CHADEMA kutoshiriki kabisa uchaguzi mkuu mwaka huu pia litakuwa pigo kubwa sana kwa 4Rs za Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea katika hadhima yake ya utawala bora.

Ikumbukwe kuwa bajeti ya serikali inategemea misaada kutoka katika mashirika, taasisi za kimataifa na nchi za nje.

Hivyo ikiwa CHADEMA hawatashiriki kabisa uchaguzi mkuu mwaka huu, litakuwa ni pigo kubwa sana kidiplomasia kwa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali ya CCM.

CHADEMA wanatakiwa kusimamia msimamo wao wa no reforms, no election bila kutetereka kabisa, maana bila CHADEMA, ushiriki wa vyama vingine una athari finyu kuelekea mageuzi ya kiutawala na siasa Tanzania.
 
Tanzania ina vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vitashiriki uchaguzi sasa chama kimoja cha siasa ndo kinaathiri nini??

Msijipe umuhimu msiokua nao uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea punguzeni utoto.
 
Hujitambui wala hujielewi umekurupuka kutoka usingizini kuja kuharisha hapa jukwaani , no reform no election maana yaka hakutakuwa na uchaguzi kama hakuna reform sasa chadema wanaweza kuzuia uchaguzi wao kama nani? kuna vyama vingi sana hatuwezi kumsikiliza mpumbavu mmoja tu kuzuia uchaguzi wa nchi nzima klwa tamaa zake za kijinga tu wala asiposhiriki hakuna athari zozote kwani kipindi hiki ni kama hakushiriki tu umeona kuna athari gani nchi imeshindwa kufanya nini kwakukosa kwao kuwa bungeni maana walibanwa mbavu na jpm balaa wakawa wanatoa ulimi tu chadema ni genge la kihuni hakuna chama hao
 
No reforms, no election ni mfupa mgumu sana kwa CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa kitaifa October 2025.

Kama serikali ya CCM italazimisha kufanya uchaguzi pasipo ushiriki wa chama kikuu cha upinzani Tanzania yaani CHADEMA basi litakuwa ni pigo kubwa sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan kidiplomasia hasa katika nyanja ya demokrasia kimataifa.

CHADEMA kutoshiriki kabisa uchaguzi mkuu mwaka huu pia litakuwa pigo kubwa sana kwa 4Rs za Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea katika hadhima yake ya utawala bora.

Ikumbukwe kuwa bajeti ya serikali inategemea misaada kutoka katika mashirika, taasisi za kimataifa na nchi za nje.

Hivyo ikiwa CHADEMA hawatashiriki kabisa uchaguzi mkuu mwaka huu, litakuwa ni pigo kubwa sana kidiplomasia kwa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali ya CCM.

CHADEMA wanatakiwa kusimamia msimamo wao wa no reforms, no election bila kutetereka kabisa, maana bila CHADEMA, ushiriki wa vyama vingine hauna athari yeyote kuelekea mageuzi ya kiutawala na siasa Tanzania.
Team Mbowe watashiriki🤣🤣
 
Tanzania ina vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vitashiriki uchaguzi sasa chama kimoja cha siasa ndo kinaathiri nini??

Msijipe umuhimu msiokua nao uchaguzi utafanyika na maisha yataendelea punguzeni utoto.
Hakuna hanayejipa umuhimu, ngoja uchaguzi ufanyike na CHADEMA wasishiriki, baada ya hapo taswira ya Tanzania kimataifa itakuwa na sura mpya na ngumu sana, vile vile hii itamtia doa hata Rais Samia.
 
inamtia doa gani? kwani muhula huu unaoisha kuna chadema bungeni? mbona mamboi yanaenda na hakuna doa lolote? niutoto tu huo mnaofnay hamko serious
 
hujitambui wala hujielewi umekurupuka kutoka usingizini kuja kuharisha hapa jukwaani , no reform no election maana yaka hakutakuwa na uchaguzi kama hakuna reform sasa chadema wanaweza kuzuia uchaguzi wao kama nani? kuna vyama vingi sana hatuwezi kumsikiliza mpumbavu mmoja tu kuzuia uchaguzi wa nchi nzima klwa tamaa zake za kijinga tu wala asiposhiriki hakuna athari zozote kwani kipindi hiki ni kama hakushiriki tu umeona kuna athari gani nchi imeshindwa kufanya nini kwakukosa kwao kuwa bungeni maana walibanwa mbavu na jpm balaa wakawa wanatoa ulimi tu chadema ni genge la kihuni hakuna chama hao
Hilo ni bunge kibogoyo hamna mtu ana muda nalo, hata Rais Samia sidhani kama analikubali ni vile tu alirithi kutoka kwa Rais Magufulu.
Athari za CHADEMA kutoshiriki uchaguzi mkuu zitakuwa ni kubwa sana usidharau waliopo ndani ya serikali wanalitambua hili.
 
inamtia doa gani? kwani muhula huu unaoisha kuna chadema bungeni? mbona mamboi yanaenda na hakuna doa lolote? niutoto tu huo mnaofnay hamko serious
Hakuna doa? Wakati nchi imeingia kwenye kashfa ya kuingiza wabunge kwa kughushi? Hakuna doa kwa sababu nchi haina utawala bora, ingekuwa nchi zenye mihimili imara, spika angepigwa chini.
 
inamtia doa gani? kwani muhula huu unaoisha kuna chadema bungeni? mbona mamboi yanaenda na hakuna doa lolote? niutoto tu huo mnaofnay hamko serious
Hili Bunge halina hali kwa watu ndiyo maana hawana muda nalo, vile vile serikali iliyopita ilipitia wakati mgumu sana kidiplomasia kutokana na uchaguzi wa 2020.

Rais samia alipoingia madarakani alikuja na 4Rs usifikiri zilikuja tu ni kwa sababu ya doa la mtangulizi wako na ndiyo maana hata huko kimataifa ameenda na hizo 4Rs, bila chama kikuu cha upinzani kushiriki uchaguzi mkuu mwaka huu hizi 4Rs zitakuwa zimepata doa kubwa sana.
 
Diplomasia Kimataifa ?!!!!!

Tuache uzuzu na tufuate Rule of Law for the benefit ya wenye nchi (Watanzania) na sio kuangalia watu huko wanasema nini au watasema nini (after all wananyea Diplomasia na Rule of Law kwa kutumia Loopholes wakiongozwa na chizi Trump) Kwahio if Trump is doing some funny stuff na hio ndio template (idol wa demokrasia) ni bora tukashinda kesi zetu wenyewe wananchi...

Na kwa hilo bora wananchi tuache kutegemea wanasiasa pekee bali kufanya yale ambayo USA walijaribu kuyafanya na Tea Parties (kushinikiza wawakilishi majimboni na kuwaambia ukweli kila wanapoharibu na sio kusubiri kila baada ya miaka 5)
 
hujitambui wala hujielewi umekurupuka kutoka usingizini kuja kuharisha hapa jukwaani , no reform no election maana yaka hakutakuwa na uchaguzi kama hakuna reform sasa chadema wanaweza kuzuia uchaguzi wao kama nani? kuna vyama vingi sana hatuwezi kumsikiliza mpumbavu mmoja tu kuzuia uchaguzi wa nchi nzima klwa tamaa zake za kijinga tu wala asiposhiriki hakuna athari zozote kwani kipindi hiki ni kama hakushiriki tu umeona kuna athari gani nchi imeshindwa kufanya nini kwakukosa kwao kuwa bungeni maana walibanwa mbavu na jpm balaa wakawa wanatoa ulimi tu chadema ni genge la kihuni hakuna chama hao
Unakuta ukirudi jioni kuna watu wanakupokea na kukuita baba 😂😂😂😂
 
Hakuna hanayejipa umuhimu, ngoja uchaguzi ufanyike na CHADEMA wasishiriki, baada ya hapo taswira ya Tanzania kimataifa itakuwa na sura mpya na ngumu sana, vile vile hii itamtia doa hata Rais Samia.
Taswira gani? Mnachekesha sana Magufuli aliwafinya nini hakikuendelea?? Yaani hyo utoto na uhuni wa Lissu ndo watu wakae wasikilize? Halafu si mmesema mtazuia kwa mabavu sasa unaomba omba nini kwa Samia?

Nimekwambia happy juu tuna vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vinashiriki uchaguzi na hakuna kitu mtafanya narudia Tena acheni UTOTO!
 
inamtia doa gani? kwani muhula huu unaoisha kuna chadema bungeni? mbona mamboi yanaenda na hakuna doa lolote? niutoto tu huo mnaofnay hamko serious
Hivi unajua unacho kiandika au unaandika kama Bashite?
 
Taswira gani? Mnachekesha sana Magufuli aliwafinya nini hakikuendelea?? Yaani hyo utoto na uhuni wa Lissu ndo watu wakae wasikilize? Halafu si mmesema mtazuia kwa mabavu sasa unaomba omba nini kwa Samia?

Nimekwambia happy juu tuna vyama Vya siasa zaidi ya 12 na vinashiriki uchaguzi na hakuna kitu mtafanya narudia Tena acheni UTOTO!
Athari za chama kikuu cha upinzani kutoshiriki uchaguzi mkuu ni kubwa sana kuliko hivyo vyama 12 kushiriki uchaguzi.
 
Nimeshangaa leo kuona wasanii amabao siku zote wako CCM eti wanajidai kuwa walikuwa wanachama wa Chadema sasa wameamua kuhamia CCM , yaani CCM wanahangaika kama kuku aliyekatwa kichwa.
 
  • Thanks
Reactions: M45
Nimeshangaa leo kuona wasanii amabao siku zote wako CCM eti wanajidai kuwa walikuwa wanachama wa Chadema sasa wameamua kuhamia CCM , yaani CCM wanahangaika kama kuku aliyekatwa kichwa.
Wasanii Tanzania hawana athari yeyote katika siasa, ni ufinyu wa maarifa kutumia mbinu za namna hii.
 
Back
Top Bottom