Nawaangalia tu.. wenye kujua hawasemi, na wasiojua wanasema sana kana kwamba wanajua.
KUHUSU UKABILA UKWELI HUU HAPA.
Licha ya ushahidi wa wazi kwamba viongozi wa ngazi za juu akiwemo yeye mwenyewe wametoka sehemu mbali mbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Chacha Wangwe ameendelea kutuhumu kwamba kuna upendeleo kwa Wachagga na/au watu wa kaskazini ya Tanzania. Kivuli pekee cha tuhuma hizi potofu ni madai ya uwongo kwamba Wabunge watano kati ya sita wa Viti Maalumu wa CHADEMA katika Bunge la Jamhuri ni Wachagga. Kama wananchi wanavyofahamu, Wabunge Wachagga ni watatu tu na wengine ni Mzanzibari mmoja, Mpare mmoja na Muha mmoja. Aidha Mh. Chacha Wangwe anafahamu kwamba kati ya wajumbe thelathini na sita wa Kamati Kuu ya Chama kuna Wachagga watano tu sawa na wajumbe wa Mkoa wa Kigoma! Aidha Mh. Wangwe anafahamu fika kwamba kati ya wakurugenzi na watendaji wa ngazi za juu wa Makao Makuu wapatao zaidi ya ishirini, Wachagga wako watatu tu. Kwa msingi huo, lengo la kashfa za ukabila ndani ya chama zina lengo moja tu: kuwapaka matope viongozi na watendaji wa ngazi za juu wa chama kwa nia ya kuwadhoofisha na kuwapunguzia nguvu ya kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya serikali na CCM.
Wangwe alikuwa mzigo mkubwa sana kwa chama, hata huko Jimboni kwake hajui kutofautisha kazi ya mbunge na kazi za watendaji wa serikali anaweza kubishana nao hata mahala ambapo hapaitajiki ubishi, Hilo linaeleweka.
Wangwe mwenyewe hajasema kama kweli wakati wa kumuondoa hawakutumia katiba, ni kwamba katiba imefuatwa haswa. Ninachoona hapa ni kama msemaji mmoja alivyosema tumezoeshwa na CCM kuwa ukikosea sijui kuna urasimu gani unatakiwa kufuatwa, hili chama kisiparaganyike. Chama siyo Mtu chama ni wanachama. Kwa CCM Tumeona kulindana hata mpaka tumefikia kukiita majina kama ishirini hivi ya kejeli lakini wameamua kunyamaza na kubaki na fedhea (Hii ni aibu!).
Nafikiri Chadema wameonyesha ukomavu katika masrahi ya chama hawamwangalii mtu usoni potelea mbali hata kama watakosa kiti cha ubunge lakini maslahi ya chama, katiba ya chama inatakiwa kulindwa. Na kama wataendelea hivi hata mwenyekiti wao atafanya kazi akijua kuwa kuna siku nayeye yanaweza kumkuta.
Kama wanajua hawasemi na tuko kwenye eneo la kupata msemaji, basi hawajui, kwani wanachokijua muda wa kukisema ni sasa.
Umetumia kigezo gani kusema kuwa hawajui? kuna mtihani mlifanya au kwa vile wewe una posts elfu kumi? siamini kuwa na posts nyingi ndio unajua,Mnyika ana posts chache au Zitto lakini huwezi kusema hajui kuliko wewe.
mkimaliza wangwe matakuja kusema hata Slaa ni mzigo, nyie mtoto akinyea kiganja mwakikata!wenzenu wanaosha na maji ya baridi, ya moto, sabuni na mwisho wanaweka jiki.
wangapi humu wamesoma signature yangu >? well, hail..........nitarudi !
Hawa wapinzani hawatuwezi, sasa ni fimbo tu, tutawapinga chadema fimbo hapa JF, na kisha tutawachanganya kwenye uongozi na mwisho watu watajua kuwa ccm pekee ndio chama kubwa.
.... ha ha ha haha .. hawa hawaijui ccm....
Niliwaonya hapa hawakusikia.
Kama huijui kazi ya usalama wa taifa sasa umeijua, tumeshawatoa kwenye debate ya EPA, meremeta, na story zingine zote za uzushi na tumewaweka hapa ambako mtagongana hadi 2010 na ccm itashinda kwa kishindo.
"Anasingiziwa" mambo mengi huyu Wangwe yakiwemo uvutaji wa bangi! Wengi humu JF huwa hatupendi kuongelea PRIVATE LIVES zetu ingawa binafsi naamini tena kwa DHATI kuwa PRIVATE LIFE ya mtu ndio mtu mwenyewe. Na inakuwa na umuhimu wa pekee kuifahamu pale mtu huyo anapokamata MADARAKA au UONGOZI wa UMMA.
This guy must be schizophrenic.
Hii ni insult kubwa sana!This guy must be schizophrenic.
Gembe ,kusema kuwa mimi ni mchagga its very wrong.
Usifanye ,usiwaze na wala usiandike kitu kwa hisia ,kuwa eti nami ni mchagga huu ni upotoswaji wa wazi kwani kwanza wewe hata hunijui wala sura yangu huijui.
Acha kupotosha .
Zemarcopolo, Mchelea Mwana, Mgagagigikoko, Kubwa Jinga,
Bahati mbaya mmesikia kile ambacho sikusema na kile ambacho nilisema hamkusikia, na hili ni kosa langu kwa sababu inaonekana nilichagua vibaya maneno yangu kiasi kwamba nikaeleweka vile ambayo sikutaka nieleweke.
Hakuna ubishi kwamba Mhe Wangwe hana maelewano na viongozi wenzake wa kitaifa na hata ndani ya kambi ya upinzani bungeni. Sasa hili huwezi kusema kwamba sio tatizo.
Natambua pia nguvu na umuhimu wa Wangwe katika chama chetu. Huyu ni kiongozi jasiri sana mwenye historia ya mapambano ambayo ni muhimu sana kwa siasa za upinzani katika bara la Afrika. Hakuna kiongozi mwingine wa CHADEMA aliyekumbana na misukosuko na mabavu ya serikali ya CCM kama Wangwe na akayashinda.
Kwa hiyo ni bahati mbaya kwamba nilitumia neno mzigo, lakini kwa kweli nilichomaanisha ni hilo la yeye kushindwa kujenga maelewano na viongozi wenzake ambayo ni muhimu sana. Kwa wale wanaopenda maendeleo ya Wangwe kisiasa kama mimi ni muhimu sana wakampa darasa la interpersonal relationships. Ni vigumu sana kufanikiwa kisiasa bila kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wenzako. Haiwezikani wewe peke yako tu uwe sahihi na wenzako wote hawapo sahihi. Nafikiri naeleweka.
Baada ya kusema hayo naomba nieleweka kwamba, pamoja na kutambua udhaifu wa Mhe Chacha, mimi sio miongoni mwa wanachama wa CHADEMA wanaunga mkono kusimamishwa kwake uongozi. Ninapinga hili kwa sababu kusimamishwa kwake hakuiongezei CHADEMA tija yeyote zaidi ya kuturudisha nyuma katika jitihada zetu za kujenga chama mbadala kwa CCM. Ninapinga pia kwa sababu timing yake sio nzuri ukizingatia kwamba mwaka huu tuna uchaguzi ndani ya chadema. Someni tena reaction yangu kuhusu statement iliyotolewa na CHADEMA, kuna kitu ambacho nilikisema na hamjakinyaka au mlikipuzia.
Hata hivyo ninawapa the benefiti of doubt wajumbe wetu wa kamati kuu kwa sababu ninaamini kwamba walichuja vizuri pros na cons za maamuzi yao kabla hawajafika walipofika. Ninaamini pia kwamba wajumbe wa kamati kuu walimpa kila nafasi ya kujirudi mhe Wangwe lakini ndio hivyo tena ilishindikana na iliwalazimu kufanya maamuzi magumu kama viongozi wa chama.
Kitila.
Wanaounda kamati kuu wamechaguliwa na Mbowe hili halina ubishi, ni Mbowe aliyewapa nafasi hizo Baregu na Ngaiza na wengine, ni sawa na kusema waziri Pinda,Ngereja na waziri Membe ambao wamepewa ulaji na JK waitwe na kuambiwa watoe maamuzi ya yaliyo na maslahi na JK au maslahi ya JK yanahatarishwa na mtu let say Sumaye, unafikiri jibu litakuwaje?
Chacha Wangwe.
Ni mbunge pekee katika Chadema aliyeshinda kwa ushindi mkubwa kwenye ubunge kwa wastani wa asilimia 65 hadi 70 hakuna mbunge yeyote wa upinzani Tanzania Bara aliyepata kura hizo, huko kote kapita kwa kishindo na kama angeenda kwenye Uenyekiti angechukua, kusema kuwa hana interpersonal skills ni kumkandamiza kwa vile wewe Kitila, Mnyika, Tundu Lissu, Zitto mko upande wa Mbowe ambao unaitwa upande wa wasomi, ndio maana mzee Halimoja amekuwa akitukanwa na upande huu kwa kujaribu kuwa na mawazo halisi, haiwezekani Wangwe akawa mzigo na mjinga wakati ameshinda kwa kishindo kikubwa jimboni kwake.
Kama mliuvumilia mzigo wake kwanini msisubiri hadi mwezi wa nane yaani mwezi mmoja tu wakati wa uchaguzi wa mkuu wa chama? kwa akili zangu ndogo inaonekana miezi saba aliyokaa madarakani kama makamu amejijenga kiasi mnaogopa kuwa akiingia kwenye mkutano mkuu kama makamu anaweza kuchukua uenyekiti.
Chadema kwa hili mmedhihirisha kuwa sio chama bali ni platform ambayo watu wanaitumia kufikia malengo yao,
kama vikao vya faragha wakufukuzwa ni Zitto Kabwe ambaye wote mnajua kuwa ana ukaribu mkubwa na JK kuliko Mbowe.
Wangwe amepunguzwa kasi au amefungwa spidi gavana na wenye chama chao.