Hivi kwani CCM mlikosa wanawake mpaka wabunge wenu wengi wa viti maalum ni wachaga kuliko makabila mengine? Ama Kikwete alikosa mawaziri kwenye baraza lake lililopita mpaka akateua wengi wa Kilimanjaro kuliko makabila mengine?
Hivi CHADEMA ilikosa makabila mengine mpaka ikateua wasukuma wengi zaidi katika wakurugenzi na maofisa wake waandamizi katika makao makuu ya chama?
Hivi Mbowe alikosa makabila mengine mpaka akateua wahaya wawili Profesa Baregu na Balozi Ngaiza katika nafasi zake za kuteua wajumbe wa kamati kuu?
Ukabila, ukabila ukukabila. Hata mie Asha leo nikiolewa na Mmakonde mtanivua ungazija wangu kama mlivyomfanyia Maulidah Anna Komu- mlaniwe wanaume nyie.
This is male chauvisism of the highest order. Shame on you Mtanzania
Asha
....
Bi. Asha Abdalla, ...
Binafsi nitashukuru sana kama utatueleza ni vigezo gani mlitumia kuwachagua hao wabunge..
Hawezi kwa sababu alifanya makusudi kwa malengo mahsusi ya kujaribu kunizushia jambo akiamini kwamba ningekaa kimya. Ambacho hakujua ni kwamba hapa JF ukisema kitu unajibiwa, huwezi kujisemea na watu wakakuacha. Wengine tunaamini kabisa ile falsafa kwamba uongo ukisemwa bila kukanushwa mwishowe huonekana kuwa ni kweli. Sasa nimembana hapa hadi kumpa habari zangu personal kabisa tangu nikiwa sekondari amebaki kubwabwaja maneno mengi.
Kitila Mkumbo amewahi kusema uongo zaidi ya mara mbili hapa hapa JF,kwanza ilikuwa GT anasema kuwa mwanasiasa ni Kitila Mkumbo akabisha sana lakini siku akaja kubadili jina kutoka Mwanasiasa na kuwa Kitila Mkumbo hiyo ilikuwa 2007.
Kitila huyo huyo ilisemwa yuko Ulaya na ni UK, akabisha baadaye akawa yuko kwenye shughuli za watu wa ulaya na mikutano kiasi cha kulumbana na Balozi Mwanaidi Majaar.
Mtu mwingine ambaye ni mwongo ni Fikira Duni kila likija jambo anaweka kinga ya kusema ni Udaku na uzushi,GT aliweka hoja kuwa Membe anamiliki kampuni ya vitambulisho na huo mradi una ufisadi akadaiwa ushahidi na kuambiwa aombe radhi kwa kuwa mwongo.
Ikaja habari ya Membe ya kugombea urais 2010 ikasemwa kuwa ni uzushi na kuna habari ya Tido na Suzane Mungi bwana Fikira Duni akaja juu na kulalama kuwa ni majungu, uzushi na udaku, habari ya vitambulisho Jenerali Ulimwengu alipoipata hapa JF akaifanyia kazi hadi sasa anaendeleza libeneke lakini mwanzo ilisemwa ni uzushi iko www.raiamwema.co.tz kwa zaidi ya matoleo manne yanaeleza habari hiyo.
baada ya FD kuonekana anatumia kinga ya udaku kuficha hoja au kuzima hoja hasa zenye maslahi kwake kwani ni rafiki wa Mwikalo anayeshiriki kutuibia kwenye mradi wa vitambulisho,sasa ameamua kubadili jina lake na kujiita Fair Player.
Fikira Duni na Kitila wamezusha mengi kiasi cha kusema kuwa DR.Warioba hana sifa za kuwa mkuu wa chuo cha Mzumbe, lakini vijana wa Mzumbe hawakusema kuwa tupeni ushahidi ndani ya 24 hours tuliwapa miezi na sasa ni miaka wameshindwa kuthibitisha uongo wao.
kwa maneno yangu ya hapo juu nathibitisha na kuwaomba wana JF hasa GT aje kututhibitisha uongo na ubabaishaji wa Msomi wa Udsm Bwana Kitila Mkumbo, kama aliwahi kulikataa jina lake halisi kipi kitamshinda kukataa kumfuata Mrema alipokuwa huko TLP? au akimuona mtu kashuka kisiasa anaona hafai? ni kweli Mkumbo anatabia hiyo ya uongo na ushahidi uko kwenye maandiko yake hapa hapa jamvini,tumemaliza kesi.
Chacha Wangwe.
Ni mpambanaji mkubwa na anaonewa na Mbowe kwa sababu ni mkweli na muwazi, viti maalum mkoa wa Mara haukupewa kiti hata kimoja wakati mkoa wa Mara hasa TARIME ndio waliopiga kura nyingi kwa upinzani,sielewi Mara haikupewa mbunge mmoja wa viti maalum, wamekwenda kuwapa wachagga watupu,CUF wametoa viti maalum kutokana na kura zinazopatika kwenye mkoa mfano mkoa wa TANGA wamempa mtu kutokana na kura nyingi walizopigiwa,Pemba wamewapa viti maalum kwa kura walizopata,basi wangewapa Sumbawanga kwani Musoma mnawachukia,mchukieni WANGWE kama mlivyomchukia DR.Warioba lakini kazi zao mnaziona. wangwe kapata kura nyingi Tarime kumshinda Slaa, Zitto hadi ALFU.
Nakushukuru kwa kuleta ushahidi wa wazi,kumbe jamaa hakuwa mkweli hapa hapa jamvini? wazungu wanasema' liers should have good memory' labda alipitiwa hakujua mpo wazee wa data na kumbukumbu.
Mie nimetaja mashahidi wangu wa kuthibitisha hilo na shahidi namba moja nimemtoa upande wao Zitto KABWE akasema atamleta imekuwa kimya, nina mashahidi zaidi ya watano, tena siku zote the burden of evidence mounts the defence'side hiyo ndio sheria.
Chacha alishika nafasi ya juu sana kwenye CHADEMA, anapokuwa na claims kama hizi ni lazima zifanyiwe uchunguzi wa kina kabla ya kuzidismiss kuwa ni uzushi au ni umamluki.
Mfano swala la kusema kuwa amefanya vikao vya siri na Kabourou ni ridiculous.Kwani katiba ya CHADEMA inawakataza viongozi wake kukutana na wanachama wa vyama vingine?
Sio Kabourou tuu aseme na kwa RA alipokutana naye Kilimanjaro Kempinsik room namba 210 kwa masaa manne walienda kufanya nini?
Utajitahidi sana kumtetea na wewe Ballile acha mchezo huo na gazeti lako.
Kumbe hivyo tena hii ni hatari ama kweli.........!kwa hiyo mtu akiwa let say NCCR ni marufuku kuwa na maongezi na mtu wa CCM?
hilo lipo kwenye katiba ya chadema?
Kumbe hivyo tena hii ni hatari ama kweli.........!kwa hiyo mtu akiwa let say NCCR ni marufuku kuwa na maongezi na mtu wa CCM?hilo lipo kwenye katiba ya chadema?
yumkini ni pandikizi la kukidhoofisha chama period!
kwa jinsi tunavyoifaham historia ya wangwe sikubaliani na wewe hata kwa sekunde mbili,,,Mapandikizi ndani ya chadema yapo mengi sana lakini sio wangwe...wangwe amekua diwani siku nyingi sie tuna mfaham kwa muda sana na itikadi na misimamo yake inaeleweka...CHADEMA lazima wakubali kubadilika na sio vizuri kumchukia mtu anaewaambia ukweli...mkiendelea hivyo hatutaona tofauti yenu na CCM ambao huweza hata kumuua mtu anaesema ukweli
What matters here je yale anayoyasema yana uzito gani?Haijalishi mtanzania majira au Tanzania Daima!Wangwe aje hapa na kusema kuwa ni kwanini Tangu issue ya Buzwagi hajawahi kuongelea suala la madini kama ilivyokuwa awali.
Barrick North Mara walikutana naye na kikao kiliendeshwa na Teweli sasa anapaswa kujua kuwa watu walikuwa wanamfuatailia kila kona ya njia zake na hata account ya mkewe ambayo ndio imekuwa ikitumika kuingizia hayo mafungu kutoka kwa mafisadi please lets be realistic na wa kweli .
Hivi Chacha leo ni mtu wa kwenda kujitetea kwenye magazeti ya majira na Mtanzania kweli ....Hamuoni tatizo hapo ?