Gembe kwa umakini wako nilitumaini uliisha kuelewa niliposema nilikuwepo na kuona kwa macho yangu. Sijui unataka nizungumzie nini? Katika mambo haya partisanship haisaidii sana. Unasema (waraka)...umesema ukweli wotekuhusu Chadema...It is clear you have made up your mind. Sidhani hata nikieleza itasadia nini. Prejudice ni mbaya sana.
Nadhani kwa wanaofuatilia niliisha kueleza kuwa hatuna la kuficha na wala hatuna la kujibu.Ni swala la mtu kushikilia tu mtizamo wake vs majority. Wakati utakapofika tutatoa yote systematically na wote wenye mapenzi mema wakitaka wanaweza kuja kufanya verification. Lakini upotoshaji kama wa RAI kuwa wabunge wajichotea hela... bila hata kupiga simu kujua walilipwa za nini nadhani ni kinyume na journalistic ethics. Lakini ndiyo nchi yetu ilivyo na wengi wetu tunafahamu sababu ndiyo maana, .. ukikutwa unaoga na kichaa kakimbia na nguo zako huhitaji kumkimbiza uchi, kwani wanaokuona hatatambua kichaa ni nani kati yenu...' Kimya chetu kitafsiriwe na wenye kutafakari katika misingi hiyo.
Dr. Slaa Mbunge wangu makini unayefanya kazi nzuri sana ya ku-audit serikali ya CCM kwa undani mzuri sana....
Kuna mambo ambayo mnayafanya ambayo huwa siwaelewi... mnavilea sana vyombo vya habari na kuvisifu sana vinapotoa mambo ya CCM hata kama hawafuati ethics zao... lakini chama tukufu kikiguswa inasemekana kuwa hao waandishi hawana ethics.
Yapo mengi ya kumtukana Mh. Mkapa... yape mengi yaliyoongezewa chumvi ya Kumhusu Mh. Edward Lowassa, Yapo mengi yaliyoongezewa tena mengine yenye harufu ya Ubaguzi kuhusu Mh. Rostam Aziz, haya yote yakiongelewa vyombo vya habari ni Hodari sana... lakini vikigeuka upande mwingine mambo yanabadilika...
In short ni wazi kwamba walionda kwenye uandishi wa habari wengi uwezo wao ni mdogo... mwandishi mzuri ni yule mtaalamu wa upande fulani... udaktari, ukaguzi, uhandisi, etc... akaongezewa namna ya kuandika... kuliko kufundishwa kuandika tu... bila ujuzi wowote.
Wewe ni muumini vizuri... SIMAMENI kiume siku moja museme UKWELI... tujenge nchi... mambo ya waandishi wa Tanzania kila aliyeguswa alishasema... Mh. Rais naye akawapa jina linalowastahili "MAKANJANJA"... kwa hiyo kweli hili hatuhitaji shule tena... tunaelewa...
Lingine... tunajua haki yako ya kutoa mawazo.... inaminywa na kuwa uko Bungeni kwa tiketi ya CHADEMA, hivyo ukikosana na MBOWE... ukafukuzwa kazi yabidi urudi Karutu...tuanze upya... wengine kwa mbali tunaona kwamba wewe na Zitto munayo siri KUBWA... sana... lakini tusubiri..
Tunachoomba... kuweni MAKINI sana... CHADEMA ikifa... itakuwa sawa sawa na Viwanda vya Mwalimu Nyerere... vilivyouwawa wakati ule wa Mh. Ali Hassan Mwinyi... Rais wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania