CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

CHADEMA mjitafakari msiwabeze wahamaji, wana hoja za msingi. Adui wenu mkuu sio CCM! Lazima mbadilike

Siasa zifanyikie wapi wakati zime katazwa? Akili za wajinga bwana hata mbumbu anaunafuu
 
Endelea kujitoa fahamu hakuna binadamu anaetaka kujihatarishia maisha yake kisa Nassari kavamiwa serikali mjitafakari mnyonge akichoka anageuka muhasi Ipo siku kiziwi atasikia kipofu ataongea hakika yote yatapita "hakika Mungu usimama nao wasimamiao haki amri kuu kupita zote pendaneni" pole Joshua Nassari
 
CHADEMA mnakoelekea siko acheni kiki na matukio fanyeni siasa,

Yaan chama kinachotegemea kushika dola ndo kinafanya mambo haya

Mtu kafanikiwa kutoroka wakaua mbwa

Hili kanusho lako umefanyia ofisi za hapo lumumba?

Very low hivi bila utafiti unapata wapi ujasiri wakubweka kama kilaza?
 
Mku Paskali Siasa za upinzani ni ngumu sana kwa nchi za Afrika yaani kuwa mpinzani ni adui mkubwa wa watawala hivi ukijiuliza Kesi walizonazo Viongozi wa Chadema ni za nini kama sio vile zikishatimia mbinu nyingi za kuwarubuni ikashindikana na mwisho inaanza kutumika nguvu kuwaumiza kwa njia kesi ambazo wanaozifungu wanashindwa mahakamani.
Kwa ufupi tuu chadema kiko makini kwani naamini wanaowapokea kutoka upande mwingine ni mwanachama kama vinavyofanya vyama vingine ktk nchi hii na tukumbuke kuna watu ambao sio rahisi kurubunika kwa vyeo au fedha ili kutimiza usaliti. Na hii tasisi ina misingi imara ndo maana wenye nguvu ya kila kitu anajitahidi kuonyesha na kusimamia mabaya kuhusu hiki chama lakini Mwenyezi Mungu ana batilisha hujuma juu yake penye wengi wenye mema na Nchi yao Mungu yupo na kuwapa mwongozo
 
Kaka Pascal Mayalla, nakubaliana na hoja yako. Lakini, ugonjwa mkubwa uliobaki na kuwasumbua CHADEMA ni kuwepo kwa Lowassa na kundi lake. Kundi la Lowassa likiondoka kwa kuhamia chama kingine au kuanzisha chama chao, CHADEMA itarejea kwenye njia yake. Hakika, uwepo wa Lowassa na kundi lake ni jambo gumu sana kwa CHADEMA kwakuwa inakuwa na muda mwingi wa kujibu tuhuma kuliko kujijenga.
Mnachekesha sana. Mahakamani hamumpeleki kama kweli mna hoja. Mmekalia kurudia kelele.
Chenge ambae ameguswa na karibu kila kashfa kubwa mpaka makinikia/mikataba mibovu ya madini,rada, escrow; yuko salama, CCM kimya na nyie kimya. Bungeni anapewa mavyeo. Unafiki gani huu. Na wapo wengi.
Kama ni hoja mliishakaukiwa. Tafuteni nyimbo nyingine.
 
I must admit ni ushauri makini sana, target ni ikulu haikupatikana mpe kijiti mwingine.

Ktk siasa ni kweli hela ni muhimu sana but it's not everything you need to win an election. Ni kweli kwamba ni lazima uwe na hela au support ya wenye hela kufanikiwa ktk siasa.

So pale unapoona hufanikiwi na hela zipo inabidi utoe kijiti kwa mwingine na km hana hela tafuta support ya wenye hela. Mbowe ameshatoa mchango mkubwa upinzani ila amefika mwisho, ampe kijiti mwingine.
 
Masawala ya vyama yana pande 2 kwa ujumla wake
Kuna wanaokipenda cha chao kwa mapenzi ya kweli hivo wanakua na uvumilivu wa kukubali yoyote yanayotokea mradi tu wamekipenda chama
2 kunakupendwa mtu yoyote au kiongozi yoyote yeye sio kwa sababu ya chama ni ushabiki tu alionao kwa wananchi au wanachama wake.
sasa inapokuja tokea mfarakano inabaki wanaokipenda chama kutetea upande wao tu wa chama na inapotokea tena mtu au kiongozi kaharibu basi mashabiki wake humtete yeye mpendwa wao sio chama tena na ndivo ilivyo katika lawama
Badala ya kujilaum mlipoteleza mnaumlaum aliyewalezesha.
 
Leo kwa hii way foward nimekuunga miguu na mikono mheshimiwa!!Hapa unafiki tuache umesema ukweli tupu. Mnyonge tumnyonge ila haki yake tumpe. Pascal sometimes unakuwaga hueleweki ila kwa leo hapo way foward hakuna ulichobakiza na kama viongozi wa CDM wako huku wakiifanya hii ndio blue print yao ikulu wanaiona mapema ila wakishupaza shingo kama wamekula dawa ya kuharisha ndio wataendelea kupiga kelele kama kasuku na kuiona ikulu kwenye picha.
Waandishi akiwamo Paschal wanaogopa kuiambia serikali ukweli, inapovunja sheria, katiba ya nchi. Kuzuia vyama kufanya siasa. Hata maombi kwa Lissu, kumtolea damu, yalizuiliwa eti ni mkutano wa siasa. Lakini mkullu alipotumia shughuli ya kutoa kamisheni JWTZ, kufanya siasa hakuna aliekosoa. Inapominya uhuru wa habari KIMYA.
Na sasa hataki kusikia katiba mpya wala angalau tume huru ya uchaguzi. Waandishi wetu wapo kimya halafu eti wanajifanya wana nguvu/uhalali wa kuishauri CDM? Watz tutaacha lini unafiki.
 
Umeongea ukweli but subiri matusi kitoka kwao maana hawa jamaa wanajua kutukana had balaa..... Hususani hiyo namba sita utatukanwa sana
 
Misingi ya ubaguzi ni mtazamo tu na kutumika na wanasiasa kugawa watu. Kama ilivyosasa, je ni kweli Rais anaendesha na kuteua kwa ubaguzi wa kikanda au ukabila?. Nadhani, historia iko wazi, inategemea wapi viongozi wa vyama wamechaguliwa na kuonekana kupata wafuasi wemgi kwa asili yao. Je Mbeya, Songwe, Iringa, Mwanza (2010-2015), na arusha nako ni ukabila? Kusemwa kusemwa kuwa kuna chama cha ukabila, udini na ukanda ndio chanzo cha kuanza kubaguana. Hii mitazamo ya kibaguzi ndiyo itakayotuletea ubaguzi wa wazi kwa sababu kuna voingozi wanakua wataamini hivyo. Maana kwa sasa kila chama kinalalamikiwa kwa ubaguzi unaweza kuwa wa kikanda, ukabila, udini. Dhana hii inamharibia hata Rais kwani watu badala ya kuangalia weledi, wanasikilizia aliyeteuliwa ametoka wapi? wakuu wa taasisi wengi wanalalamikiwa kutoka kanda ya victoria. Ni dhana potofu, itatumaliza siku zijazo.
Msingi wa Chadema ulijengwa katika ukanda na ukabila kama ambavyo msingi wa Cuf ulivyojengwa katika udini na Upemba kwa maana hiyo vyama hivi lazima vitajimaliza vyenyewe na kamwe wasiisingizie CCM!!
 
Misingi ya ubaguzi ni mtazamo tu na kutumika na wanasiasa kugawa watu. Kama ilivyosasa, je ni kweli Rais anaendesha na kuteua kwa ubaguzi wa kikanda au ukabila. Nadhani, historia iko wazi, inategemea wapi wa vyama wamechaguliwa na kuonekana kupata wafuasi wemgi kwa asili yao. Je Mbeya, Songwe, Iringa, Mwanza (2010-2015), na arusha nako ni ukabila? Kusemwa kusemwa kuwa kuna chama cha ukabila, udini na ukanda ndio chanzo cha kuanza kubaguana. Hii mitazamo ya kibaguzi ndiyo itakayotuletea ubaguzi wa wazi kwa sababu kuna voingozi wanakua wataamini hivyo. Maana kwa sasa kila chama kinalalamikiwa kwa ubaguzi unaweza kuwa wa kikanda, ukabila, udini. Dhana hii inamharibia hata Rais kwani watu badala ya kuangalia weledi, wanasikilizia aliyeteuliwa ametoka wapi? wakuu wa taasisi wengi wanalalamikiwa kutoka kanda ya victoria. Ni dhana potofu, itatumaliza siku zijazo.
Viongozi wa Chadema katika mikoa uliyotaja 85% wanatokea mkoa mmoja wa kaskazini. Hata mbunge wa ilemela katika mwaka ulioutaja alitokea mkoa huo huo wa kaskazini!
 
Mkuu umewashauri kwa nia njema subiri waje wakulipe matusi!
420b4af01d92f2a503a08a91436f2a67.jpg
 
Back
Top Bottom