Utaratibu mbaya sana huu. Tume ya uchaguzi inapaswa ikishamtangaza mgombea kuwa amepita, iwe amepita kweli.
Sijui wenye mamlaka ya mapingamizi wanawezaje kuwa na sababu na uthibitisho wa mapingamizi katika muda wa masaa 24!!?![emoji15] Hili linawezekana kwa mgombea mmoja tu wa chama kilicho madarakani kutumia vyombo vya serikali kuandaa mapingamizi yenye mashiko tokea form za wagombea wengine ziliporejeshwa!!
Lissu kwa kupitishwa jioni ya saa 1, anapata wapi ufahamu wa mapingamizi kutoka kwa wenzake au dhidi yao na kujiandaa kwa majibu mujarabu na uthibitisho??
Isiwe tu ukipingwa kwa tuhuma, mzigo wa kujiondoa kwenye shutuma na ukosaji uwe ni kwa aliyewekewa pingamizi bila muda wa kutosha kutafuta majibu au kuomba uthibitisho kutoka kwa mweka pingamizi. Jambo hili linapaswa kufanywa katika mfumo kama wa mahakama!!