Pre GE2025 CHADEMA msiweke Wagombea kwenye haya Majimbo na CCM pia haya Msiweke ili kujenga Bunge lenye nguvu baada ya 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ktk hao wote hakuna kijana (below 35 yrs) hata mmoja. Sasa vijana unataka waingieje kwenye siasa ikiwa unataka wazee waendelee kuwa wabunge?

Tuache uchawa tuige mifano ya vijana wa SA, Senegal, na Niger.
 
Yani unapangia wananchi wakumchagua. Punguza kuabudu watu. Kwanini wewe usigombee ubunge?. Umebaki kumpigia Kafulilia Kampeni. Acha hizo
 
Sasa unabishana na ukweli wewe? Kuna mtu wa Kumtoa Majaliwa Luangwa?
Luangwa ndio wapi?. Jifunze kuandika vizuri. Halafu usipende kuwatukuza watu kijinga. Eti nani wa kumtoa Majaliwa Ruangwa!. Una tatizo.
 
Esther Matiko, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, ni wana Ccm lakini mtoa mada amewaweka upande wa Upinzani.

..Bunge litakalotufaa linapaswa kuwa 55% kwa 45% kati ya kambi ya serikali na kambi rasmi ya upinzani.
 
Esther Matiko, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, ni wana Ccm lakini mtoa mada amewaweka upande wa Upinzani.

..Bunge litakalotufaa linapaswa kuwa 55% kwa 45% kati ya kambi ya serikali na kambi rasmi ya upinzani.
Sina hizo taarifa kama wao ni WanaCCM
 
Yani unapangia wananchi wakumchagua. Punguza kuabudu watu. Kwanini wewe usigombee ubunge?. Umebaki kumpigia Kafulilia Kampeni. Acha hizo
Yaani kwenye orodha yote hiyo umemuona Kafulila tu?
Halafu Mimi sina Chama kaaa ukijua, Nasijawahi kumpigia debe mtu wa Chama chochote
 
Majimbo 21 uwaachie chadema ili iweje?,jambo hili haliwezi kujiridia asilani abadani
 
Sina hizo taarifa kama wao ni WanaCCM

..na taarifa kwamba wamefukuzwa Chadema huna?

..kwamba wako ndani ya bunge kwa msaada wa serikali na Ccm kinyume na matakwa ya Chadema hilo pia hufahamu?
 
Ni siasa za kijinga kutokuweka wagombea kwenye demokrasia. Mtu yeyeote ana haki za kushiriki uchaguzi. Kikubwa hapa kama wadau ni kupigania chaguzi huru bila kujali chama. Malalamiko mengi ni wizi wa kura . Tusijadili mambo ya kijinga mengine
 
NEC na polisi hakikisheni msikae karibu na CCM.

Wakurugenzi wa wilaya hakikisheni ajira zenu sio za raisi wa ccm
 
Chadema kupata hawa Wabunge ni ndoto hata hivyo.
 
Sasa unabishana na ukweli wewe? Kuna mtu wa Kumtoa Majaliwa Luangwa?

Umeanza kuwa na uelewa lini? Isije ikawa upo sekondari unasoma!!

Majaliwa mwaka 2020 kwenye uchaguzi huru asingeshinda, ndiyo maana aliwatumia majambazi kumteka na kumpiga mpinxani wake ili atangazwe amepita bila kupingwa.

Hao wabunge bandia uliowaorodhesha hapo juu, karibia wote walitumia uovu wa namna hiyo. Wananchi bado wana hasiri dhidi yao. Kwenye uchaguzi huru, kwenye hiyo orodha, wa kuweza kuwa wabunge, hawatazidi nusu.
 
Ngoja tuone 2025 itakavyokuwa
 
Mkuu kwani unadhani Kuna mtu wa kumahinda Majaliwa?
 
Chadema nawapeni huu ushauri Bure Kanisa na kama hamtauzingatia msije kusema hatukuwaambia haya,

Lazima Muwe na area of concetration.

Ushauri wa Bure kabisa huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…