Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Hayo maisha ya kuamka ndipo ujue utakula nini utakufa nayo.
Achana naye huyo njoeni tumukomboe! Tukipatikana hata wachache tukikaza wengine watatuunga mbele kwa mbele!
Mabomu ya machozi na maji ya pilipili tutayakabili kama chachandu!
 
Sidhani kama CDM na ACT wangekua na uwezo wa kuzuia uchaguzi...hapo unawalaumu bure tu.
Hapana. Siwalaumu bure.

Walijua uchaguzi huu usingekuwa wa HAKI na HURU mapema sana. Dalili na mipango ilikuwa wazi kwamba hapatatokea uchaguzi huru.

Walichotakiwa kufanya CHADEMA na ACT-Wazalendo ni wao pia kuandaa mbinu za kuzuia uchafuzi huo kungali mapema kabisa. Na kama huamini ninachoandika humu, humu ndani ya JF niliwahi mapema kabisa kuhimiza wazuie uchaguzi kufanyika. Hili sio jambo geni kulizungumzia hapa, nimelipendekeza siku nyingi sana.

Sasa mkuu wangu 'Proved', hebu niambie: ni kipi bora na rahisi kutekelezwa: Kuzuia uchaguzi huko huko unakofanyika kwenye vituo vya kupigia kura huku ushahidi wa uchafuzi huo ukiwepo na wananchi wakiushuhudia, AU kukataa matokeo ya uchafuzi huo, huku mshindi akishatangazwa?

Maandamano ya sasa hatawezi kamwe kubadili uhujumu huu uliokwishafanyika. WaTanzania ni wagumu sana kuwashawishi wafikie ngazi ya maandamano inayoweza kuleta mabadiliko ya uchaguzi huu. Na hata ikiwezekana, itakuwa ni kwa gharama kubwa sana.
 
Yajayo yanafurahisha , wakati wa kufunga kampeni Kawe , watu wao walituletea taarifa katikati ya mkutano kwamba Tume imemuandalia Magufuli kura mil 12 , na haraka Lissu akauhabarisha umma , si umeona kura alizopata Magufuli ?
Pangekuwa na mipango na mikakati kabambe ya awali ndani ya chama, taarifa hiyo ndiyo ingekuwa chachu ya kuzuia uchafuzi mzima huko huko kwenye vituo vya kupigia kura. Huko hakuna polisi wa kutosha kurusha mabomu na risasi.
Na muhimu zaidi, wananchi wenyewe ndio wangekuwa mashuhuda wa kuona uharifu uliopangwa na serikali na CCM.

Sio mara ya kwanza kusikia maneno haya rafiki 'Erythro': :Kuzuia Uchaguzi usifanyike bila kuwepo mazingira ya kuwa uchaguzi HURU na HAKI.
Au nasema uongo rafiki yangu?
 
Nilikuwa nasubiri muda ufike tuingie barabarani lakini nashangaa hadi sasa kimya ikumbukwe mimi ni miongoni mwa yule jamaa sauti yangu ilisikika sana jana kwenye ile video ya Mavunde nikiwa na hasira

Watani zangu mnataka kuniambia ni kheri mimi ccm nimejaribu kupaza sauti kuliko nyinyi mmejifinya nyuma ya keyboard
Nawakumbusha tu kuwa sisi sio TANZANIA NI TANGANYIKA

NENO TANGA kwa lugha ya kigogo ni kuwakusanya mifugo ambayo haina ushirikiano imezagaa HAINA UMOJA
Ningeshangaa kama tanganyika kungekuwa na maandamano

WATANI VIPI nikweli nyie waoga,hivi lissu leo ametoka hata nje kwenda Kariakoo

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1784][emoji1784][emoji1784][emoji1784]
Nipo Chamwino nasubiri[emoji857][emoji857][emoji857][emoji857]
 
Nilikuwa nasubiri muda ufike tuingie barabarani lakini nashangaa hadi sasa kimya ikumbukwe mimi ni miongoni mwa yule jamaa sauti yangu ilisikika sana jana kwenye ile video ya Mavunde nikiwa na hasira

Watani zangu mnataka kuniambia ni kheri mimi ccm nimejaribu kupaza sauti kuliko nyinyi mmejifinya nyuma ya keyboard
Nawakumbusha tu kuwa sisi sio TANZANIA NI TANGANYIKA

NENO TANGA kwa lugha ya kigogo ni kuwakusanya mifugo ambayo haina ushirikiano imezagaa HAINA UMOJA
Ningeshangaa kama tanganyika kungekuwa na maandamano

WATANI VIPI nikweli nyie waoga,hivi lissu leo ametoka hata nje kwenda Kariakoo

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1784][emoji1784][emoji1784][emoji1784]
Nipo Chamwino nasubiri[emoji857][emoji857][emoji857][emoji857]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu kwnza sababu ya kumzomea Mavunde ni nini na wewe ni ccm?

Pili, hakuna mtz wa kuacha shughuli zake za kujitafutia mia mbili mia mbili kisha aende kuandamana
 
Nipo shamba tangu mapema sana kutayarisha mbegu zangu hivyo nataka kujua hayo maandamano yameanza na kama yameanza yamefika eneo gani mpaka muda huu

Wenu mpenda amani
katika ujenzi wa taifa!
 
Ndugu yangu posho za ubunge ufaidi na familia yako, baada ya kukosa uniingize mimi barabarani nikale mkong'oto wa Polisi . Chukua familia yako itangulize mbele. Mimi najua uchaguzi umeisha kifuatacho ni kuchapa kazi.
Hahahaah labda wana toa per dm
 
TAARIFA MUHIMU SANA!!!

Watanzania tuishio nje ya nchi (TANZANIA DIASPORA) tumeanza kuandamana kupinga UCHAFUZI uliofanyika juzi hapo nyumbani Tanzania!

Hawa ni ndugu zetu kutoka Ulaya ya Kaskazini (Sweden [emoji1236], Norway [emoji1189] na Denmark [emoji1087]) ambao tayari wameanza maandamano yao nje ya Ubalozi wetu uliopo Stockholm, Sweden...

Watanzania tuishio nchini hapa Ufaransa [emoji632] tunaandaa maandamano hayo kesho Jumatatu, November 2, 2020 nje ya Ubalozi wa Tanzania [emoji1241] nchini Ufaransa [emoji632].

Maandamano yataanza saa 2 asubuhi na kumalizika saa 6 mchana!

Baada ya maandamano, WAZANZIBARI tuishio nchini hapa, kwa kuongozwa na Balozi wetu (BABU MZANZIBARI), tutazindua Ubalozi wetu (Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar nchini Ufaransa)... Ofisi za Ubalozi wetu zipo mitaa ya TROCADÉRO, karibu sana na mnara wa EIFFEL...

Kwa niaba ya Wazanzibari wote waishio nchini hapa Ufaransa, mimi, BABU MZANZIBARI, Balozi wa Zanzibar nchini Ufaransa, natumia fursa hii kuwakaribisha ndugu zetu Watanzania waishio nchini hapa, katika uzinduzi wa Ubalozi wetu!

Usafiri, kula, kunywa ni kwa gharama yangu mwenyewe!...

Kwa kauli moja, tumekubaliana kuwa hatuitambui serikali haramu ya John Pombe Joseph Magufuli! Hatuitambui serikali haramu ya Hussein Ali Hassan Mwinyi!

Rais wa Zanzibar tunayemtambua ni Maalim Seif Sharif Hamad aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar!... Na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayemtambua ni Tundu Antipas Lissu, aliyechaguliwa na Watanzania!...

Mungu ibariki Zanzibar yenye mamlaka kamili, Mungu ibariki Tanzania!... [emoji1488]

[emoji1485][emoji1485][emoji1485] Sambaza ujumbe huu umfikie kila Mtanzania mpenda haki!...[emoji1474]
Diaspora wawap awo mana me nipo England sjaskia iyo kitu na tuna umoja ambao hua tuna share info zote kupitia uongozi wetu na kama juzi tumekubaliana tuje home kwenye kuapishwa mh na mm kesho nasafiri kuja uko
 
Kuna Vita kubwa imeanza.Vita ya kudai haki.

Mimi ni muumini wa kudai na kusimamia HAKI.vita ya kudai haki sio vita ya kutoa kafara,ni inayotaka mashujaa.Sio vita ya kufuata Mkumbo ni vita ya kutafuta ushindi.Najua kila mtu anaweza kuwaza lake ila ujumbe wangu kwa Watanzania ni huu;

"Ndugu zangu,rudini katika nyumba zenu,mkakae na wake zenu na watoto zenu na familia.Nyoeni vichwa vyenu mkafanya maombelezo na kulia kwa ajili ya nchi yenu.Msile wala Msinywe chochote mpaka Jua litakapokuchwa.Ombeni na Salini katika imani zenu.Lieni kwa uchungu mkuu na kisha kesho muamke na kuendelea na maisha yenu.Hii vita sio ya kwenu."

Vita inahitaji mashujaa wenye nguvu na ujasiri.Nendeni ndani mwenu mkalale.

Nawatakieni kila la heri
 
"Wajumbe wa kamati kuu watakaotaka kushiriki"
Yaani wao wana option ya kushiriki. Kwao ni lazima coz wao ndio wameibiwa na sio wananchi.
Hahahaha watakao taka wakiwa busy wabaki tuu
Watoto wa wakulima ndo waende wakandamane mandamano yaso na kibali wachapike kwa kukiuka sheria
 
CHADEMA na ACT Wazalendo tunautangazia umma na wanaopinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu kushiriki Maandamano ya Amani kesho Jumatatu ya Tarehe 2/11/20. Madhumuni ya Maandamano ni kudai kurudiwa Uchaguzi Mkuu chini ya Tume Huru ya Uchaguzi.

Maandamano yataanzia sehemu 2, kundi moja litaanzia Buguruni Sheli kuchukua barabara ya Uhuru mpaka Kariakoo, Msimbazi Road mpaka fire, Morogoro road, Bibi Titi mpaka Ofisi za Tume.

Kundi lingine litaanza Ubungo Bus Terminal kuchukua Morogoro road mpaka fire kisha Bibi Titi kuelekea Ofisi ya Tume.

Wajumbe wa Kamati Kuu mnaopenda kushiriki maandamano tafadhali mtachagua kati ya maeneo hayo. Maandamano yanaanza saa mbili kamili asubuhi kuelekea Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu JK Nyerere Conference Center. Viongozi Wakuu wataongoza Maandamano hayo.



Ushauri wangu kwa Jeshi la Polisi.
1.Kuhakikisha inazikamata familia za hawa wahamasishaji wa haya maandamano ya kidhalimu
2.Kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma za pesa wanazopokea viongozi hawa kusababisha vurugu nchini
3.Kuangalia upya hivi vyama na kuweka mkakati wa itisha uhaguzi wa huru ndani ya hivi vyama ili wale viongozi wanaongangania madaraka waondoshwe.
Wanachama wengi wa vyama vya CHADEMA na ACT hawakubaliani na uhuni wa viongozi wa juu wa vyama hivi.Hivyo serikali kupitia msajili wa vyama aitishe mikutano ili tuweze kupata viongozi wazalendo.
4.Kufuta vyama vyenye mrengo wa Ushoga amabavyo ni kinyume na mila na desturi za watanzania.
 
Mtu mwenye shughuli ya kufanya na anawaza familia itakula nini. Hawezi kupata muda wa kuandamana.

Maisha ya kuwaza utakula nini tushayavuka, hata hivyo... Nyerere asingejitoa ungeendelea kuwa utumwani we kiumbe!
 
Basi na wewe jitoe leo basi
Sii kila dai ni haki unapaswa kujua hilo
Na si kila interest ni national interest zingine ni personal interest zinazowekwa kwenye kivuli cha taifa ili kupata support hao wote wapiga kelele walikua viongozi walifanya nn kikubwa mpa watu waingie barabaran
 
Back
Top Bottom