Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu


Unataka haya yaendelee?

 
Nmeupenda tu ushauri wa mzee, kuna maeneo vyama vya upinzani vinafeli. Ni kama mbwa flani mwenye njaa anabweka sana ila akishashiba analala tu asubiri njaa iume tena aanze kelele
 
Rafiki zangu wakubwa kutoka upinzani nilioongea nao wanasema kuandamana ni upuuzi na haitabadili chochote. Wanasema hawashiriki. Wanadai kuwa ushauri mwingi waliokuwa wanatoa kwa vyama vyao kuhusu masuala ya uchaguzi ulipuuzwa na kushindwa huku vibaya ni matokeo ya kupuuzwa kwa ushauri wao. Pengine huu ni muda wa vyama vya upinzani kujitathmini zaidi wapi walikosea.
 
Madelo ga wiza

Napenda kuwasihi watanzania wote hasa wana jf kutijihusisha na maandamano ambayo kumsingi na batili na ni uchu wa madaraka kwa viongozi wetu.

Sitafurahi kuona wanabodi wenzetu wakisota rumande bila sababu yenye tija kwa taifa letu hili lililobarikiwa amani

Tanzania ni nchi inayo pokea wakimbizi ba sisi hatutaki kuwa hao wakimbizi abadani.

Ni wengi wameonya juu ha hatari hii lakini nimeona nitumie elimu yangu kwa faida yako wewe unayepanga kuandamana,fikiria kuna maisha baada ya hapa.

Usikubali kamwe kutumika kisiasa!!

Kumbuka akili ni nywele ........!

Asiye sikia la mkuu......!

Then poleni sana kwa kupoteza mjipange tena 2025

#magema jr
 
Ni upuuzi kushabikia raia wasio na hatia wakipigwa kisa kudai haki zao.

Mbona Lissu alipotua Dar watu walifanya maandamano ya amani na hakuna vurugu ilitokea? Kwani mkiacha waandamanaji wakusanyike kwa amani mnakosa nini?

Hili bara kweli lina laana
Vyama vipo 21
hapo vimeandikwa ACT na CHADEMA
Vyama vingine sisi atuandamani tunasubiri wenzetu wenye uchungu zaidi na nchi wafe ili sisi tukombolewe..
 
Sawa
Si wengine umri mdogo
Bado hatujala mema ya nchi
 
shughuli ya kesho ni nzito saa moja nitapata supu na chapati tatu pale kimboka bar buguruni.
 
Sidhani kama CDM na ACT wangekua na uwezo wa kuzuia uchaguzi...hapo unawalaumu bure tu.
 
Nmeupenda tu ushauri wa mzee, kuna maeneo vyama vya upinzani vinafeli. Ni kama mbwa flani mwenye njaa anabweka sana ila akishashiba analala tu asubiri njaa iume tena aanze kelele
Ajabu Sana.
 
Mkuu ingia barabarani kesho. Kwangu mimi maandamano ni kupotezeana muda tu. Wacha tukatafute riziki za kula familia zetu..

Kwa vizazi vijavyo huu ni wakati wa kuwatengenezea njia. Maisha ni mafupi ,dunia ni mtihani tu . Kila mtu atakufa . Starehe zina mwisho.
Future kwa vizazi vijavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…