Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo kufanya maandamano ya amani Nov 2, 2020 kupinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu

Naomba nyie viongozi wa ACT-CHADEMA mje na wake zenu, watoto wenu, ndugu zenu wengine pamoja na michepuko yenu pendwa...
 
tutaandamana mpaka tume huru ipatikane kwa faida ya wote.
 
Kwa vizazi vijavyo huu ni wakati wa kuwatengenezea njia. Maisha ni mafupi ,dunia ni mtihani tu . Kila mtu atakufa . Starehe zina mwisho.
Future kwa vizazi vijavyo


Sawa mkuu, Nyie andamaneni...
 
Dah naumia kukosa upinzani bungeni ila hii message ya kwenye picha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
udakutz_-20201101-0001.jpg
 
TAARIFA MUHIMU SANA!!!

Watanzania tuishio nje ya nchi (TANZANIA DIASPORA) tumeanza kuandamana kupinga UCHAFUZI uliofanyika juzi hapo nyumbani Tanzania!

Hawa ni ndugu zetu kutoka Ulaya ya Kaskazini (Sweden 🇸🇪, Norway 🇳🇴 na Denmark 🇩🇰) ambao tayari wameanza maandamano yao nje ya Ubalozi wetu uliopo Stockholm, Sweden...

Watanzania tuishio nchini hapa Ufaransa 🇫🇷 tunaandaa maandamano hayo kesho Jumatatu, November 2, 2020 nje ya Ubalozi wa Tanzania 🇹🇿 nchini Ufaransa 🇫🇷.

Maandamano yataanza saa 2 asubuhi na kumalizika saa 6 mchana!

Baada ya maandamano, WAZANZIBARI tuishio nchini hapa, kwa kuongozwa na Balozi wetu (BABU MZANZIBARI), tutazindua Ubalozi wetu (Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar nchini Ufaransa)... Ofisi za Ubalozi wetu zipo mitaa ya TROCADÉRO, karibu sana na mnara wa EIFFEL...

Kwa niaba ya Wazanzibari wote waishio nchini hapa Ufaransa, mimi, BABU MZANZIBARI, Balozi wa Zanzibar nchini Ufaransa, natumia fursa hii kuwakaribisha ndugu zetu Watanzania waishio nchini hapa, katika uzinduzi wa Ubalozi wetu!

Usafiri, kula, kunywa ni kwa gharama yangu mwenyewe!...

Kwa kauli moja, tumekubaliana kuwa hatuitambui serikali haramu ya John Pombe Joseph Magufuli! Hatuitambui serikali haramu ya Hussein Ali Hassan Mwinyi!

Rais wa Zanzibar tunayemtambua ni Maalim Seif Sharif Hamad aliyechaguliwa na wananchi wa Zanzibar!... Na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunayemtambua ni Tundu Antipas Lissu, aliyechaguliwa na Watanzania!...

Mungu ibariki Zanzibar yenye mamlaka kamili, Mungu ibariki Tanzania!... 🙏🏾

👉🏾👉🏾👉🏾 Sambaza ujumbe huu umfikie kila Mtanzania mpenda haki!...👍🏾
Yani nyie ndio makichaa kabisa em tulia uvae barakoa uko, mnatuhamasisha tuvuruge amani huku kwasababu hamtakuwepo hapa eeh, endelea kuota..
 
CHADEMA na ACT—Wazalendo tunautangazia umma na wanaopinga kuvurugwa kwa Uchaguzi Mkuu kushiriki Maandamano ya Amani kesho Jumatatu ya Tarehe 2/11/20. Madhumuni ya Maandamano ni kudai kurudiwa Uchaguzi Mkuu chini ya Tume Huru ya Uchaguzi.

Maandamano yataanzia sehemu 2, kundi moja litaanzia Buguruni Sheli kuchukua barabara ya Uhuru mpaka Kariakoo, Msimbazi Road mpaka fire, Morogoro road, Bibi Titi mpaka Ofisi za Tume

Kundi lingine litaanza Ubungo Bus Terminal kuchukua Morogoro road mpaka fire kisha Bibi Titi kuelekea Ofisi ya Tume.

Wajumbe wa Kamati Kuu mnaopenda kushiriki maandamano tafadhali mtachagua kati ya maeneo hayo. Maandamano yanaanza saa mbili kamili asubuhi kuelekea Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu JK Nyerere Conference Center. Viongozi Wakuu wataongoza Maandamano hayo.

Humu JF ni mitandao mingine ya kijamii, kaulimbiu ya wafuasi wenu ilikuwa "Lissu kaza kwa spana", kinyume chake ni ninyi. Sasa hayo maandamano yatakuwa yenu viongozi na familia zenu, labda mwalipe vibaka wa kuwasindikiza. Hao pia wakiona Jeshi la Polisi watayeyuka kama barafu kwenye joto.

Kila la kheri na hayo maandamano
 
Nyie wenzangu na mimi msifuate mkumbo kuweni makini mtakuja kutolewa sadaka.

Angalia Ugali wako na familia yako.

Hakuna chama chochote ulimwenguni popote kitakachokuletea Ugali nyumbani kwako.

Hakuna Rais yoyote atakaekuletea Ugali nyumbani kwako.

Msifikiri mtawekewa mabomba majumbani mwenu, ukifungua bomba la Maji yanatoka Maziwa freshi.

Hao wanaotaka kukutumieni hawatoonekana.

Hao wanaotaka kukutumieni, usishangae baada ya miezi michache wamerudi/wamejiunga chama tawala.

Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Hivi wewe ndugu una uhakika gani sijapiga kura?

Nimepiga kura na nimeona wizi mkubwa mbele ya macho yangu

With this convinction naandamana kesho kiroho safi....nitakae uwawa ni mimi,sitaki ushauri wako!

#Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana
. Naomba kesho ufe kweli usipokufa wewe Ni mnafiki au jitoe hadharani uuelezee umma ulivoona kura ikiibiwa mbele ya macho yako
 
The guilty are afraid. Wezi wanaogopa maandamano. Wameleta watu wao wa propaganda hapa JF. Wapenda haki wote twende tukawaonyeshe kuwa dhuluma iliyofanyika 28 Okt haikubaliki. CCM jifungieni katika vyumba vyenu. Hamlazimishwi kuandamana.
Mkuu utaanzia pale buguruni au ubungo?
 
Mambosasa ameleta mtu feki studio kusema kuwa amepangwa kuchoma petrol stations hapa jijini DSM.

Hatutishiki. Tutaandamana tu
 
Hii matando mbona haifungwi vizuri?
 
Back
Top Bottom