Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
- Thread starter
-
- #21
Chadema ni chama Cha Watanzania wote ambao wamekandamizwa na CCM na kujikuta wakilazimika kuishi bila kutumia ubongo wao na elimu zao
Je, wewe ni miongoni mwao?
Mtu mnafiki anapokuwa Chadema, hujulikana na kubainika mapema mno kwa sababu ubongo wa watu kwenye chama hiko ni ruksa kuutumia
Wewe unachosema, ni kile kile ambacho kwako wewe unaona ni kama kukandamiza mawazo na kubinya uhuru wa watu ilihali Chadema ingali bado inapambana na mambo mengi sana!
Hapa nakubaliana nawe 100%.
Nina mashaka siku ikitokea Chadema wakaingia ikulu, kisha mmoja wa viongozi wao apewe tuhuma zozote, ukihoji tu, basi nao wanaweza kuunda makundi ya wasiojulikana waanze kutuwinda mitaani.
Kama unayaelewa mazingira ambayo chadema wana-operate kisiasa..huwezi walinganisha na ccm kwenye mizani yenye vigezo vinavyofanana..
Mwanazuoni kama wewe ilitakiwa uwe unajua kutofautisha CHADEMA na wanachadema, na washabiki wengineo. Mambo yanafanywa na mashabiki ila unakuja kuchambua taasisi.
Tukiingia kwenye suala la salamu za rambirambi ni kweli ni hiyari ya mtu, lakini kufanya personification ili kuelezea hisia zako nayo inakuwa sio sawa, yeye angetoa salamu zake kisha msemaji wa Chama au kutokana na protokali yao aliyepaswa kupeleka salamu kuwakilisha chama angefanya hivyo. Sasa kuvunja kwake itifaki inaonekana kuna la zaidi yaani ametaka aonekane na kujiweka yeye mbele na anajali kuzidi?
Ila kubwa kuliko yote hatupaswi kutazama hayo, inapaswa tutazame sababu za hizi hasira za watu zimekujaje?
My kaka, ngoja niplay "devil's advocate" kidogo.
Ukisema "maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake" unamaanisha ni nani akiona? ni akina ambao wana mandate ya kuamua maoni haya au kukosolewa huku kuna hila nyuma yake?
Je huyo mtu anayeona au kuamua nini kina hila akikosea na akakosolewa, mizani gani itatumika kuamua kama hayo maoni dhidi yake ni legit?
Nilishasema CCM imeoza lakini CHADEMA sio mbadala wake, CHADEMA ni zaidi ya Ccm kwenye kutokuvumilia maoni tofauti.
CCM ni chama cha hivyo kabisa lakini ukiangalia chadema unavyo endesha mambo yake utagundua chadema na ya hovyo mara 10 ya CCM.
Hii umepiga angle zote za uwanja na kukabia kwa juu yaani kwa kifupi umetoka somo kubwa sana japo wapo watakaokupinga kwa huu ukweli ambao ni ukweli mtupuHamjambo!
CHADEMA wengi wao wanatabia ya udikteta uchwara, ukandamizaji wa uhuru wa maoni hasa yanayokinzana na sera zao.
CHADEMA wanauwezo wa kuingilia uhuru binafsi wa mtu mwingine hata kama havunji sheria za chama, katiba ya nchi na maadili.
Ukitaka ugombane na CHADEMA basi pinga au kosoa sera au jambo lolote unaloliona halipo sawa Kimtazamo wako.
Ni tabia mbaya sana. Ni zilezile tabia za kiccm wanazozilalamikia. Tofauti ni kuwa CCM wanadola alafu upande wa Pili hawana.
Sisi Watibeli tunazingatia sana haki za watu hata kama tunatofautiana mawazo na falsafa.
CHADEMA hupenda wao tuu ndio waongee kumaanisha wao tuu ndio wasikilizwe.
Ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA Kama wao wanavyokosoa viongozi wa vyama vingine. Inakuwa nongwa.
Sio lazima chama chote kimchukie mtu mmoja. Sio lazima. Sio lazima wanachama wote wampende kiongozi fulani. Sio lazima.
Kupenda mtu ni haki ya mtu iliyo ndani ya hiyari yake.
Humu mnaweza kunipenda Mtibeli au msinipende. Hilo lipo ndani ya mipaka yenu. Sio mimi nijisikie vibaya au niwalazimishe mnipende. Huo ni ukatili.
Au wanaonipenda watake kuwalazimisha wasionipenda wanipende. Huo ni ushenzi.
Haina tofauti na mtu anayelazimisha Salamu. Kusalimia ni hiyari ya mtu. Ipo ndani ya uhuru wake.
Mtu kutoa Salamu za Rambirambi kwenye msiba ni hiyari yake.
Mtu kumsamehe mtu mwingine sio lazima ni hiyari yake.
Usishangae siku Tundu Lisu akiamua kusamehe waliompiga Risasi alafu ukaona baadhi ya watu wakachukia, wakamkasirikie wakamuona Msaliti.
Sisi Watibeli hatuumizwi na maamuzi ya mtu mwingine ambayo yapo ndani ya mipaka yake na Hayagusi mipaka yetu.
Hofu yangu ni hii, tabia za kiccm naziona pia huko CHADEMA.
Usitoe kibanzi jichoni mwa mwenzako wakati wewe unaboriti.
Tabia za kiccm, inaletwa hoja na upinzani. Wafuasi wa CCM wanajibu ninyi vibaraka wa wazungu, sijui blah blah.
Wanaccm nao wakileta hoja, wafuasi wa chadema utasikia buku 7 sijui blah blah blah.
Mwanaccm akikosoa chama chake. Anaandamwa na CCM wenzake ikiwezekani kufukuzwa kabisa uanachama.
Mwanachadema akikosoa chadema au viongozi wa chadema, wanachadema wanaanza kelele na kumuita msaliti na majina mengine.
Hatutaki vyama vinavyotaka kusifiwa na kupongezwa tuu. Tunataka vyama ambavyo wanachama wake watakuwa huru kukosoa na kusifia bila kuletewa fujo.
Nimemaliza
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ccm kitaasisi imeizidi zaidi mara 100 Chadema katika kuendesha mambo yake.Wote wapo kwenye Kapu moja.
Angalia hata mambo ya uchaguzi.
Juzi walikuwa na uchaguzi hapa, wapo waliokimbilia CCM kisa kushindwa uchaguzi.
Wapo waliohamia CHAUMMA.
Yaani mambo ni yaleyale.
Hii umepiga angle zote za uwanja na kukabia kwa juu yaani kwa kifupi umetoka somo kubwa sana japo wapo watakaokupinga kwa huu ukweli ambao ni ukweli mtupu
Hila inafahamika, na dhamira njema inaeleweka. Mfano halisi, Lema kajifanya kutoa pole kwa Samia wakati Samia kaua maelfu ya watanzania na kaona sawa. Lakini hila yake iko wazi kabisa kuwa Lema sio wa hivyo, maana aligoma kumsalimia Makonda huko Monduli kwenye msiba wa Lowassa. Kwanini asipewe ukweli wake?🫢🫢😆😆😄
Hao policcm wakifanya hivyo kosa lao linakuwa wapi?
Acheni tabia za ajabu.
Hila ya mtu unaipataje kwenye maoni yake?
Mwamba ngozi huvutia kwake. Katika vyama vya hovyo kwa sasa ni ccm, kuvaa koti la serekali ndio kunasaidia kuficha madhaifu ya ccm.Ccm kitaasisi imeizidi zaidi mara 100 Chadema katika kuendesha mambo yake.
Na chadema isipo dhibiti hawa wanaharakati walio jaa mihemko na matusi inaenda kufa kifo kibaya sana.
Binafsi nimekuwa nikipigwa vita sana pale ninapokosoa jambo lolote kuhusu chademaVyama vyote vinasema hilohilo kwamba vipo kwaajili ya kupigania Watanzania. Hiyo ni siasa.
Ninachokisema ni ile tabia ya vyama kikiwemo Chadema kuwa na tabia ya kukataa ukosoaji na kuwachukulia wakosoaji kama maadui au ccm kumbe wengine hata huo muda wa vyama hawana
Ni kweli ccm ni chama cha hovyo lakini chadema ni hovyo mara mia ya ccm.Mwamba ngozi huvutia kwake. Katika vyama vya hovyo kwa sasa ni ccm, kuvaa koti la serekali ndio kunasaidia kuficha madhaifu ya ccm.
Hila ya Lema iko wazi, aligoma kumsalimia Makonda kwenye mazishi ya Lowassa, lakini Mbowe alisalimiana na huyo Makonda, unataka upewe mfano zaidi wa hila?My kaka, ngoja niplay "devil's advocate" kidogo.
Ukisema "maoni ambayo wanaona wazi kuna hila nyuma yake" unamaanisha ni nani akiona? ni akina ambao wana mandate ya kuamua maoni haya au kukosolewa huku kuna hila nyuma yake?
Je huyo mtu anayeona au kuamua nini kina hila akikosea na akakosolewa, mizani gani itatumika kuamua kama hayo maoni dhidi yake ni legit?
Haya ndio matamanio yako, lakini uhalisia unakataa.Ni kweli ccm ni chama cha hovyo lakini chadema ni hovyo mara mia ya ccm.
Chadema inamapungufu mengi sana .